Monday, July 20, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Bow wow:kumbe dogo amejikunja na mademu sita wakiwemo hawa
Ishu ni malavi davi, yanamhusu kila mtu kwa sababu ndiyo sanaa kiranja katika maisha ya binadamu. Ukisema hayakuhusu that means mambo yako siyo mazuri! Ebwana dah!

Ni dogo aliyekulia kwenye Hip Hop na akaanza kusanya noti akiwa na umri wa primary school kabla ya kuibukia kuwa tajiri wa mfano kwa wajasiriamali wengine.
Ni mapenzi sasa, dogo alitimiza umri wa miaka 18 miaka minne iliyopita na inahisiwa kwamba alianza sanaa ya mapenzi akiwa U-18.

Amekwishatoka na mademu sita ambao wanatambulika, wa kwanza ni Dolicia Bryant baadaye akaanza kumegana kisela na mwanamuziki Ciara mwaka 2005 kabla ya kupigana chini mwaka 2006.

Alipoachana na Ciara, dogo alihamishia jeshi kwa Paula DeAnda mwaka 2007, akazinguana naye na kugeukia kwa Angela Simmons ambaye alijikunja naye from 2007 up to 2008.

Kipindi akiwa na Angela Simmons, ‘bwa mdogo’ alionesha ujuzi kwa kucheza nje-cup na mwanadada Melody Thormon kwa maana hiyo in a same year, aliwatumia watatu ukimuongeza na Paula DeAnda. Hata hivyo, tangu mwaka jana (2008) dogo amejituliza kwa mrembo Karrine Steffans.

Jina lake kamili ni Shad Gregory Moss, alizaliwa Reynoldsburg, OH, Marekani Machi 9, 1987. A.K.A zake nyingine ni bow weezy,
bow wizzle na hapa juzi kati alitangaza kusain out katika game ya Hip Hop kwa maelezo kwamba kila kitu alichokihitaji anacho.

Pesa anazo, umaarufu anao wa kutosha! Dogo matata eeh! Msomaji kama unapenda kufahamu usiano wa zamai na sasa wa staa yeyote wa kiwanja tuandikie ujumbe mfupi(SMS) ukilitaja jina la muhusika kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173, e-mail:mcgeorge2008@gmail.com. Pamoja sana.

**************************************
MB Dog
Nembo ya wanamuziki wenye sauti za hamasa nchini, Mohamed Mbwana ‘MB Dog’ amefiwa na mwanaye wa kike, Suhaila Mohamed aliyekuwa na umri wa miaka saba.
Suhaila alifariki dunia last weekend, usiku wa kuamkia Jumamosi nyumbani kwa staa huyo Mabibo, Dar es Salaam baada ya kuzidiwa na shambulio kali la malaria.

Insider wetu alitupasha kwamba kabla ya kifo hicho, Suhaila alikuwa arrested by malaria 4 almost mwezi mmoja na kwamba alilazwa Amana Hospital kwa wiki tatu kisha aliruhusiwa kurudi nyumbani ambako alimudu ku-survive kwa wiki moja tu kabla hajaitikia wito wa Mungu.

Mpendwa wetu Suhaila, alizikwa kwenye makaburi ya Mabibo Hostel, Dar juzi (Jumamosi). Hili ni pigo kubwa kwa mwanetu MB, sisi Abby Cool & MC George over the weekend kwa niaba ya readers wetu, tunatoa pole nyingi kwake. Mungu amempenda zaidi.
********************************************

Hizi ni hasira za fans wa...hip hop
Tulistop kuendelea na debate yetu kuhusu Hip Hop kutokana na kifo cha Mfalme wa Pop duniani, Michael Jackson ‘King MJ’ ambaye ali-pass away Juni 25, 2009 Los Angeles, Marekani.
Tutazidi kumkumbuka mtu mzima MJ, alifanya mengi kwenye muziki ndiyo maana pamoja na mambo kibao yaliyokuwa yakizungumzwa kuhusiana naye enzi ya uhai wake lakini inapozungumziwa kazi yake kila mtu anapiga saluti!

That’s for Michael! Baada ya makala yaliyopita kuhusiana na Hip Hop, wadau wengi walituma sms wakichangia yale waliyonayo. Cheki wanavyomwagika;

Easy E aliweka Cul kichwani nae sio mwana HIP HOP na alipenda sana mademu, Ice T aliweka rolers kichwani nae siyo mwana Hip Hop.

**********************
HIP HOP inazidi kufifia au kufa, Bongo wengi imani zao haba, hawajui Hip hop ni nini? Hip Hop haiuzi wala hailipi, pia katika Radio stations, Hip hop haipigwi sana kama R&B na nyinginezo. Kila time ni mapenzi tu.
I am MC Luggy, from Geness High School, Makambako. napenda sana Hip Hop kwa sababu ina ujumbe.
***********************
Hey man, siwafagilii artists wanaojifanya wafuasi, wanaleta makuzi instead of playn their parts! Nimeipenda topic! It’s me Shady!
*********************
Hey ebwana dah! Mc George na Abby Cool sina cha kuongea but i’m waiting mnachokuja nacho katika safu yenu ya Ze real kuhusu Hip Hop! Ni kweli Hip Hop ni harakati siyo watoto wa mama wana wave kichwani! Wanauza sura then wanajita wana-Hip hop.
Barks hapa niko pande za Mbeya City
********************
Wengime wanachana Hip Hop kwa kuwa sauti zao hazina mvuto kwenye R&B. HIP HOP ina nguzo tano baab! Nawashauri wana-Hip Hop wazidumishe ili Watizedi waache msemo kwamba Hip Hop ya ukweli ipo America.
Mussa Kibiki wa Mafinga Iringa.

Hayo ndiyo baadhi ya maoni ya wafuasi wa game ya muziki wa Hip Hop. Cheki na sisi wiki ijayo ili ufahamu tutashuka na ishu gani nyingine.
*************************

Fid Q Yupo next door na fans wake
Staa wa Hip Hop mwenye vocal yenye ujazo mkubwa, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amesema kuwa ameamua kujiweka karibu na fans wake ili kuboresha utendaji kazi wake kimuziki.

Fid Q ambaye anatambaa na a.k.a kibao kama vile Ngosha the Don, Jeshi la Mtu Mmoja alisema kuwa katika mpango huo wa kuwa next door na fans wake, ameanzisha kona ya kuwasiliana nao kwa njia ya sms.

“Hiyo ni fan base yangu, kujiunga unatuma sms yenye neno FIDQ kisha unaituma kwenda nambari 15522,” alisema Ngosha the Don na kujazia: “Huduma hii ni kwa wateja wa mitandao ya simu za mkononi nchini, Tigo, Zain na Vodacom pekee.”
**************************************

Eti Michael Jackson hakuwa rijali!!!
Shoga ambaye pia alikuwa mpenzi wa Daktari wa ngozi wa marehemu Michael Jackson, Arnold Klein ameibuka na kudai kuwa, nyota huyo eti hakuwa rijali kwasababu alikuwa hana uwezo wa kupata watoto.

Katika mahojiano na tovuti moja ya Marekani, shoga huyo, Paul Gohranson alisema kuwa, ‘MJ’ (Michael Jackson) alipoteza uwezo wa kuzalisha mbegu za kiume baada ya siku moja baba yake kumpiga teke la kwenye korodani.

Gohranson aliendelea kudai kuwa, hali hiyo ilisababisha marehemu amuombe daktari wake (wakati huo) Dk Arnold Klein amchangie mbegu zake za kiume ili aweze kupata watoto na kuwa baba.

“Nilimuuliza Arnold kwanini Michael Jackson hatumii mbegu zake za kiume, akanijibu kuwa, (Michael) alikuwa hana uwezo wa kupata mtoto, “ alisema Gohranson.

“Arnold alinielezea matukio mawili ambayo baba yake alimpiga kwenye sehemu zake nyeti.”

Akaongeza: “Katika tukio la kwanza, wakati Michael alipokuwa mdogo, baba yake alimnyanyua kwa mguu mmoja na kuanza kumpiga.”

“Dr Klein alisema kuwa, MJ alimwambia kwamba wakati huo baba yake hakudhamiria kumpiga sehemu zake za siri, lakini alipompiga alisikia maumivu sana.
“MJ alianza kulia wakati baba yake alipozidi kumsema huku akiziminya korodani zake kwa nguvu.”
********************************
compiled by mc george

No comments: