Friday, July 17, 2009

Waraka wangu juu ya maisha ya ulaya

kaka,heshima yako..!

nimesoma makala yako kwenye blog yako jinsi mwanafalsafa alivyoelezea juu ya maisha yalivyo magumu ulaya,mi napingana nae kimtazamo,kwa sababu mwanafa anaposema maisha ya ulaya ni magumu lazima awe ameyalinganisha na sehemu nyingine(bara jingine tofauti na ulaya)aliyokaa,hapa namaana kwamba kujua ugumu au urahisi wa mahali ni lazima uweke uwiano wa sehemu zaidi ya moja ndio utajua wapi pagumu na wapi ni pepesi.

mwanafalsafa amekuja ulaya hana zaidi ya miezi6,inavyoonekana kabla ya kuja ulaya alikuwa akipaota kuwa ulaya ni kama peponi na hilo ndio kosa kubwa alilofanya...mimi nataka nimweleze kwamba,kuishi ulaya tena hasa uingereza(sio mradi ulaya)kuna afadhali kubwa saana kuliko kuishi nchi yoyote ya africa,ulaya kuna opportunity nyingi saana,watu tumefanikiwa sana kimaisha tofauti na tulivyokuwa tukiishi tanzania,nakupa mfano mmoja wa uzuri wa ulaya....mtu unatoka tz unakuja ulaya ukiwa huna baba,mama,shangazi wala ndg yoyote wa karibu,unafika ulaya na unayaanza maisha kivyako,unaenda kwa egency(kutafuta kazi) bila kushikwa mkono na mtu yoyote na tena unakutana na wazawa nao wanataka hiyo hiyo kazi unayoitaka wewe na mwisho wa siku unaipata wewe hiyo kazi,tofauti na bongo ambapo vijana wengi wamesoma na wana degree zao lakina wapo mtaani kwa kuwa hawana watu wa kuwashika mkono.

hivyo kaka,mi nataka kuwaambia vijana wenzangu kuwa,kama kuna mtu mwenye nafasi na uwezo wa kuja ulaya basi na aje tu ila kubwa ni kuwa ajue anakuja kufanya nini,hili la kujua unakuja kufanya nini ndio vijana wengi wa kitanzania hatuliweki kichwani,wabongo wengi wanakuja ulaya wakijua wanakuja kusoma na mwisho wa siku wanapoteza kila kitu,yaani ni kwamba kama unakuja ulaya lazima uweke nia ya ulichokifuata mara tu utakapofikisha miezi 2,kama unania ya kusoma basi inabidi usome kweli na usitume hata senti tano nyumbani(bongo) ili siku ya mwisho urudi na vyeti vyako ukatafute kazi,maana kama umeamua kusoma itabidi ufanye kazi ili upate pesa ya kujilipia fees na chumba(tena kichumba kama stoo,maana kinaingia kitanda cha single au mchange watu wawili mchukue chumba double),hapo utasoma na utarudi na vyeti vyako nyumbani au unaweza kuomba skilled visa kwa kuwa ukiwa na vyeti vya kuanzia degree unaruhusiwa kutafuta kazi na kuishi hapa hapa nchini.....na kama umekuja na huna nia ya kusoma basi lazima lazima uhakikishe unaweka lengo la hicho kitu unachokitaka na akika kuwa kwa ulaya hakuna kinachoshindikana na mifano ipo mingi saaana,wapo walioamua kuoa wanawake wenye uraia wa hapa ili nao wapate unafuu na mteremko ktk maisha yao na wamefanikiwa,wapo waliojidai ni wakimbizi na wakafanikiwa..........HIVYO KUBWA KULIKO YOTE NI KUJUA UNAKUJA ULAYA KUFANYA NINI,KWA MAANA UKIWA ULAYA UNAONA SIKU ZINAKUMBIA KULIKO BONGO HIVYO HUTAKIWI KUPOTEZA MUDA KABISAAAA!

Huu ni mtazamo wangu baada ya kuishi Uingereza miaka kadhaa - Mdau

10 comments:

PM said...

Sasa kuna haja gani kwenda ulaya? Watu tuko bongo na tunakamua kama kawa, bongo mswano bwana! nani kakwambia bongo hamna madili? nini ulichonacho wewe huko ambacho unadhani sina? Nina nyumba nzuri, gari, na watoto wanasoma, so maisha ni wewe mwenyewe. Mtu kama unajua chanel zilipo, huna haja ya kwenda ulaya kuhangaika wakati life iko hapa hapa bongo! ULAYA, ULAYA, NIKAFATE NINI ULAYA WAKATI HAMNA KISAMVU WALA MGAGANE!

Anonymous said...

Kusema Ukweli MwanaFA is a peace of crap' anaposema maisha ya ulaya magum anamaanisha maisha bongo marahisi?? huku maisha ni wewe unavyoyachukulia,i mean ukiambua kuishi maisha ya raha fanya kazi na sio kuuza sura kwenye blogs na kuandika mashairi ya bongofleva, Ulaya ukibeba box unaweza kulipa pango (rent) na ukawa unaishi maisha standard including usafiri, ukilinganisha na bongo mtu ukibeba box pale kariakoo huwezi kununua hata baiskeri au kupata mlo kamili, mimi watu wanaotaka kuja Ulaya pia nawaalika sana ila wajue tu kwamba ukitaka kufaidi ulaya fanya kazi kwa bidii, acha utozi, Starehe fanya mara moja kwa mwezi, kumbuka ulipotoka na cha msingi usifuate marafiki ambao hawajui kilichowaleta hapa ni kipi, Obviously marafiki wa MwanaFA kila mtu anawajua ni wa style gani so no doubt

Mtazamo wa Mwana FA hauna tofauti na mtu anaewaambia watu wabaki vijijini maana mjini maisha magum lakini anasahau kwamba mjini atleast opportunities zipo tofauti na kijijini ambako ni 100% broke streets

Ni mtazamo wangu na ni kitu cha kawaida kutofautiana mitizamo na bila shaka utayaweka mawazo yangu

Anonymous said...

ndio nakuunga mkono kwa asilimia 100. hilo lipo wazi maisha ya viwanjani huwezi kufananisha na bongo bwana khamisi ishu ni kwamba watu wamekuja bila visa au passport(si shauri mfanye hivyo0 lakini wamefanikiwa na wametulia kwa hapa afrika ya kusini kuliko wangekuwa hapo bongo!!! maisha ya kiwanja ni kiwanja tu!!!

Anonymous said...

Nimekaa Ulaya miaka 20 sasa, kwa hiyo naweza kusema najua vizuri maisha ya Ulaya. Kwanza kabisa Ulaya hakuna ubabaishaji, kazi mtindo mmoja. Kama wewe u mvivu wa kazi, utalala na njaa kwa vile hakuna kula kwa jirani. Pili, Ulaya kuna uhakika wa maisha (kutegemea ninchi gani unaishi). Katika nchi niliyopo mimi, nina uhakika wa matibabu,makazi, usalama, pensheni ya uzee na watoto wangu wote wamekwenda shule mpaka ngazi ya chuo kikuu. Ukulinganisha hiyo point ya mwisho ni kuwa Ulaya kuna unafuu sana kama tayari upo kwenye system yao. Kama haupo, sijui, lakini sidhani kama ni rahisi hivyo...afadhali urudi Tz ukapige dili!

Anonymous said...

Hawa wote waongo bwana mwandishi maisha ulaya magumu kweli kama anavyosema mwana fa,kama una uwezo kusoma bongo wewe soma uko hapa uje kutembea lkn kama unakuja kubangaiza njoo sema maisha sio rahisi kabisa, nani kakwambia kazi zinapatikana kwa urahsi eti uanenda kwa agency unapata kazi mzungu ananyimwa nani kakwambia? hiyo ilikuwa miaka iliyopita asilimia ya watu wenye maisha rahisi ni waliojilipua, wenye karatasi za hapa na waliooa wabongo, me niko hapa mwaka 12 ,wakati ule tulipokuwa tumekua sisi ilikuwa rahisi unaweza kujilipua au kutafuata mtu ukaoa kwa bei poa, sasa hivi kuo au kuolewa kwa makaratasi si chini ya pound 6000-5000 , mtu umekuja uku kwa ki hela cha kiinua mgongo cha wazazi wako au umepata tu pesa twako bongo umekuja uku,kujilipua haman siku hizi kusoma na kufanya kazi mwiho masaa 20 hadi wakati wa likizo ndio ufanye zaidi, hayo masaa 20 yatakutosha kulipia nyumba na kula bado ujaenda shule nauli bado aujalipia bills ndogo ndogo na ukoo mzima unakutegemea, zamani tunafanyia majina ya watu kazi, nani atakupa jina lake wakati na yeye ana kazi anataka kupata benefit acha hiyo wanafunzi ku renew visa siku hizi uwe na hela za kutosha kwenye account yako, wanaoenda ireland kujiwasha akuendeki cku hizi wanacheki finger prints,na hao watu wanaowaambi njoo uku ukifika hatakaa na wewe week mbili ya tatu anakuona mzigo na hivi kazi hakuna ndio basi, me nawashauri ndugu zangu angalieni maisha bongo ukishindwa nenda nchi za kueleweka canada au australia uku USA,UK na EUROPE YOTE akufai mtaishia kujutia hela zenu za nauli mngefanyia vitu vya maana.......

Anonymous said...

inaonekana wote mnaoongea shule hamna hilo moja cha pili bongo it's a land of opportunity sana ila u have to hustle to get that opportunity. Ila ulaya mnaosemea nyie cio labda kama ulaya unafanya kazi ya maana hapo sawa sasa wewe unabeba box na unajisifia humu kweli, kazi za ulaya ni za kulipa rent, chakula na nguo but no future hilo lazima mlijue mimi niko state na nnaona maisha cio na kuko juu kuliko hiyo ulaya yenu

PM said...

Nyie wabeba box hapo juu mnanichekesha kweli!! Sasa kuna haja gani ya kuja ulaya wakati ni lazima mtu utoil ili mambo yawe safi, wakati bongo watu tunakamua na tumekunja nne??!! Nyie naona mnapenda tu kushangaa weupe na majengo, hamna zaidi. Bongo tambarare bana, acha asikwambie mtu. Nyie bebeni mabox, migongo ikipinda rudini home tuwape ajira.

Anonymous said...

Mie namshukuru Mungu nilifika England kwa lengo la kufanya elimu yangu nimeimaliza na sasa naelekea nyumbani kwa kuwa ninaamini nitaitumia elimu yangu vizuri katika nchi yangu kuliko UK.
Mie nimekuwa UK kwa miaka 2 ila kusema ukweli maisha ni magumu na isitoshe kama umekuja kwa student Visa labda uvunje sheria ya zaidi ya masaa 20 ila kama ukifanya kwa sheria zao zinavyosema lengo halitotimia kabisa.
Muanzishaji wa maada hii anajisahau kuwa watu wanafikiria ni jinsi gani utakapoitumia elimu yako uliyoihangaikia kwa muda mrefu. Uko ulaya mzungu hana heshima na elimu uliyoipata UDSM, Mzumbe,SAUT nk.
Kama uwezo wa kihandisi,kihasibu,uwalimu nk.tunao na tunahitaji kutumika katika field zetu sasa kama ulaya hazipo na tunazinguliwa si bora turudi nyumbani tukatumike katika nchi yetu(Tanzania itaendelezwa na wenye moyo na nchi yao)
Ulaya watu wanajidai na kupiga kelele, kama una elimu na pia uwe na bahati ya kupata kazi ya maana,
kwa watu ninaowafahamu wengi wamemaliza elimu na makaratasi wanayo ila wanafanya kazi za ajabu ajabu mtu ana MBA ila mlinzi wa majengo na kukesha usiku mzima wapi na wapi.
Mhandisi na madesa yote yalivyomtesa kitchen porter(kuosha vyombo majikoni), mfagizi wa barabara nk.

Mie ushauri wangu kama unakuja UK kusoma njoo ila uwe na udhamini wa kutosha ili umalize elimu kwa wakati na ukaanze kuitimia na kama una uwezo rudi nyumbani mapema kabla umri haujakuacha. Unaweza kuja kuwa disappointed bure huko mbele ya safari.
Tunahitaji kuyazungumza haya mambo kwa kirefu. Tukumbuke katika mitazamo huwa tunatofautiana na kuheshimu mawazo ya watu.
Wengi wameongea ila kila mtu ana muono wake katika hili ila kwa waliochangia hapa kama watu saba kabla yngu hawayapendi maisha ya hizi nchi za kibepari.
Nitaandaa nami waraka mdogo wa kuuelezea Umma ni jinsi gani tutumike katika nchi yetu ili angalau hata kama hatutakuwepo miaka 50 mingine ijayo ila kuwe na tofauti ndani ya nchi yetu

Mdau akiwa njiani na wiki moja kurudi Bongo rasmi.

Anonymous said...

jamani mnaodai ulaya ni bora kuliko bongo ni waongo na wanafki...mwenyewe niko UK nalipiwa ada ya shule na matumizi yote na wazazi ila maisha ya huku ni magumu asikwambie mtu hakuna cha kula bata wala nini...kwanza utampata nani wa kwenda kula nae bata? kila mtu yuko bize na maisha na kazi yake muda anaopata mtu anajisomea...nimeona watu wamemaliza ma masters yao na wazungu hawakupi kazi wanpeana wenyewe kwa wenyewe we unaedai wazungu wananyimwa unapewa wewe kwasababu wanaona unanguvu ya kubeba boz kuliko huyo mzungu wao na wao wanachohitaji kazi yao ifanyike...watu wanamaliza shule wanaishia kupiga kazi za kifagio(cleaning), kuchambisha wazungu au kuwa walinzi hzo ndo kazi zao hamna la maana na hela zenyewe huzioni zinaishia kwenye rent na bills yaani kama hela za mashetani zinatoweka unapigika na kazi na hupati hela ya kusave so my brothers and sisters tusiwadanganye wenzetu kama mtu unataka kuja kusoma huku akikisha unafull sponsorship atleast unaweza ukawa na amani la sivyo hali ya huku inaogopesha!

Unknown said...

tumesikia mashauri yenu tutafanyia kazi