Saturday, July 18, 2009

MOJA YA VYANZO VYA UCHUMI MBOVU NI UVIVU

Ndugu zangu na marafiki zangu, na maadui wangu pia kama mpo.
Nawasalimuni. Nimetembea nchi nyingi ulimwenguni humu. Nikagundua kuwa
kati ya watu wanaochapa kazi sana, waasia ukiondoa waarabu wanaongoza
kuwa na bidii sana. Nadhani ndio maana japo wachina ni wengi, mpaka
wengine wanachapa kazi huku daa tena wengine hapa daa ni makonda na
machinga wazuri kuliko wetu, wote hao hawafi njaa. Wazungu, hasa wale
wa scandnaviana countries nao wanashikilia nafasi za juu kuchapa kazi.
Walatin amerika sio wachapa kazi saana, lakini wao wamebarikiwa, wana
mvua nyingi na mamisitu makubwakubwa. Hivyo, tunaweza kusema wao wana
neema kubwa saana.
Sisi waafrika, tuna umasikini na resources (rasilimali tunazo za
kutosha kuendelea). Nadhani umasikini tulionao unasababushwa kwa kaisi
kikubwa na uvivu. Watu wengi wanapata mshahara lakini kazi waliyofanya
ni kidogo. Huenda ndio maana mishahara yetu ni midogo pia. Kazi pia ni
kidogo.

By Yona Mrao

1 comment:

Anonymous said...

uvivu unaweza kuwa factor,lakini udogo wa mshahara kwa bongo si kutokana na kazi kidogo hapo nakuomba uchunguze upya.nakubaliana na wewe wachina na waasia wengine wanapiga kazi lakini mishahara mfano china sijui kama unaijua vizuri.kuna sababu nyingi zaidi ya uvivu zinazotuletea umaskini.japo wavivu waache pia