You are what you eat
Usagaji mzuri wa chakula una uhusiano wa moja kwa moja na ubora wa afya yako. Hakuna ubishi kuwa usagaji wa chakula ukiwa mbovu, hutapata choo ipasavyo na ukosapo choo ni dalili ya matatizo mengi ya kiafya mwilini. Chakula unachokula ndicho kitakachoamua hatma ya tumbo lako na ndicho kinachoathiri afya yako.
Mfumo wa usagaji chakula, ambao unapita kwenye utumbo unaokadiriwa kuwa na urefu wa futi 30, ndiyo wenye suluhisho la matatizo mengi ya kiafya yanayotukabili kuliko vile ambavyo tunaweza kudhani. Utumbo unapokuwa msafi, afya nayo huwa nzuri.
Katika makala ya leo, tutajaribu kukumbushana kwa kutoa vidokezo muhimu vya kuzingatia katika kufanikisha usagaji mzuri wa chakula utakao kuwezesha kupata choo sawasawa kwa na utumbo msafi utakaopitisha virutubisho muhimu vinavyohitajika na mwili wako:
VYAKULA ASILIA
Pendelea kula vyakula bora na asilia kuliko kupenda kula vyakula vilivyosindikwa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu. Mfano, maharage ya kupika mwenyee ni bora kuliko ya kwenye makopo, halidhalika nyanya za kutayarisha mwenywe ni bora kuliko za kwenye makopo. Jaribu kula kila kitu kikiwa ‘fresh’ na asilia kadri uwezavyo.
UTAFUNAJI
Usagaji wa mzuri wa chakula tumboni huanzia mdomoni mwako. Hakikisha unatafuna sana chakula kabla ya kukimeza. Mate yako yanavimeng’enyo muhimu ambavyo husaidia usagaji wa chakula na kupambana na ‘bacteria’. Watu wengi huwa hawatafuni chakula, kitendo ambacho hufanya usagaji wa chakula kuwa mgumu kinapofika tumboni.
ULAJI MATUNDA
Ndani ya tumbo lako kuna mfumo unaotegemea sana ulaji wa matunda na mboga na vinapokosekana vitu hivyo, kunakuwa hakuna uwiano mzuri. Tunashauriwa na kusisitizwa sana kula matunda na mboga mboga kwa wingi, ambazo siyo tu hulinda mwili, bali pia ndiyo kichochoe kizuri cha usagaji chakula tumboni.
UNYWAJI MAJI
Watu wengi wanapenda kunywa kahawa na soda, wengine ndiyo huwa vitu vyao vya kwanza kutia tumboni kila asubuhi. Vinywaji hivyo hukausha maji mwilini na hivyo kupunguza nishati ya mwili. Tunashauriwa kunywa maji ya kutosha kila siku ambayo ndiyo msingi mkubwa wa kuupa mwili nguvu na kusaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni.
SAFISHA TUMBO
Njia nyingine bora ya kuwa na utumbo msafi ni kusafisha utumbo mpana kwa njia ya ‘enema’, hasa kwa wale wenye matatizo sugu na ya muda mrefu ya kutopata choo. Enema siyo tu husafisha utumbo, bali huondoa hadi sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa huru na maradhi mbalimbali.
Ili kujua mwenendo wa utumbo wako, unapaswa kufuatilia haja zako. Kwa kawaida mtu anayekula mlo wake wa kila siku kawaida, anapswa kwenda haja chapo mara moja kwa siku na mara nying huwa kila baada ya kula.
Iwapo unakula milo yote mitatu kila siku lakini hupati choo kwa siku mbili hadi 3, elewa kabisa una matatizo makubwa ya kiafya, kama hayajajitokeza yako njiani. Kwa hali hiyo, huna budi kufanya kila uwezalo uondoklane na tatizo hilo upate choo kama kawaida, tena cha kutosha.
(kumradhi wasomaji wangu kwa kuchelewa wiki hii kupost makala yenu, nilipitiwa)

No comments:
Post a Comment