Wednesday, July 15, 2009

Je ni kweli Muziki wa Bongo Fleva Unakaribia Kupoteza Utamu Wake?


KUANZIA mwanzoni mwa miaka ya 2000, ubongo wa wa vijana wengi wa Tanzania ulikuwa umejaa muziki wa Bongo Fleva. Unapowaona wamekaa vijana zaidi ya mmoja, basi mazungumzo yao yalikuwa ni juu ya muziki huo. Hata mavazi yao, matamshi yao yalikuwa ni ya kibongo fleva. Suruali kubwa inayoacha makalio wazi, fulana kubwa na hereni kifuani. Hiyo ndiyo ilikuwa staili ya kukuonyesha kuwa wewe ni mwana BongoFleva. Lakini wakati muziki huo unachukua chati, mwanamuziki mkongwe na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo 'Mjomba' alisema kuwa muziki huo ni sawa na Big G itafika kipindi utaanza kupoteza utamu.

Katika miaka ya hivi karibuni maneno hayo ya Gurumo kama yanaanza kutoa mwanga, kwani hali iliyouwa awali katika muziki huo inaanza kupotea. Muziki huo umeanza kupoteza umaarufu wake kwenye vinywa vya vijana. Wengi waliokuwa na ndoto ya kuwa wasanii wa Bongo Fleva wameanza kurudi nyuma, huku wengi wao walioingia wanatoka. Mavazi ya kibongofleva na swing (miondoko) ya kibongofleva yamepotea na wale ambao waliyatoa mawazo yao shuleni, sasa wameanza kuyarudisha. Je ni kweli Muziki wa Bongo Fleva Unakaribia Kupoteza Utamu Wake? Joseph Haule 'Profesa Jay' na Ambwene Yesaya 'AY' wanajibu swali hilo.

Gonga link hii kupata jibu la swali hilo: nifahamishe.com

No comments: