Monday, July 13, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!



La-Toya: Dada’ake Michael Jackson, Amewahi kupiga picha kibao za utupu na kujiachia na midume minne
Ebwana dah! Leo inamcheki dada’ke King of Pop duniani, Michael Jackson aliyefariki dunia hivi karibuni, huyu si mwingine bali ni mwanamuziki, mwanamitindo na mcheza filamu La-Toya Jackson aliyetupambia safu hii kwa picha za ukweli.
Baada ya kifo cha kaka yake, mashabiki wengi Bongo wamekuwa wakitamani kujua mengi kuhusu ndugu zake waliobaki, na ndiyo sababu iliyotufanya sisi Abby Cool & MC George over the weekend kuzama mtandaoni na kuibua ishu kibao kuhusu Latoya wakikiwemo mastaa wa kiume aliowahi kujihusiaha nao kimapenzi.

Kwa mujibu wa mtandao unaodili na ishu za uhusiano, kwa nyakati tofauti La-Toya amewahi kujiachia na wanaume wanne ambao ni mwanamuziki mkongwe Chuck Berry ambaye nyota yake ni Punda, David Gest, Jack Gordon na Prince, mwanamuziki ambaye aliwahi kudondoshewa skendo ya ushoga.

Kama ulikuwa haufahamu, La-Toya ambaye hivi sasa ameenda eji, akiwa anamiliki umri wa miaka 53 aliwahi kupiga picha kibao za utupu kwa ajili ya kupamba jarida maarufu la Marekani, Playboy la 1989 (kama anavyoonekana katika hizo ndogo hapo juu), wakati huo akiwa ni mrembo mwenye umri wa miaka 33 tu.

Katika game ya muziki, La-Toya aliweza kukamata chati mbalimbali na ngoma zake kadhaa ukiwemo ‘If You Feel the Funk’ ambao ulifunika katika Billborad kwenye miaka ya 1980, huku akidondoka na albamu kadhaa. Hadi hii leo bado anaendelea kupiga shoo za hapa na pale japokuwa siyo kivile.

Akiwa na macho na nywele zenye rangi ya Dark Brown, msanii huyo alizaliwa kwa jina la LaToya Yvonne Jackson katika eneo la Gary, Indiana, Marekani.
**************************
Papii Kocha akabidhi mikoba ya albamu yake kwa Shigongo
Aliyekuwa rapa namba moja wa Bendi ya FM Academia, Francis Nguza a.k.a Papii Kocha mtoto wa mfalme ambaye sasa anatumikia kifungo cha maisha katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam, amemwomba Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo kuwa msimamizi wa albumu yake ya Salima.

Msanii huyo ambaye alihukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kushirikiana na baba yake pamoja na ndugu wawili kuwalawiti watoto, amefikia hatua hiyo baada ya kuona hapati faida ya kazi yake hiyo kutokana na kukosa mawasiliano mazuri na msimamizi wake wa awali.

Kwa mujibu wa barua aliyoandika Papii na kupigwa mhuri wa Mkuu wa Gereza la Ukonga, msanii huyo anasema kwamba amelazimika kumwomba Shigongo asimamie kazi yake hiyo kwasababu anaamini kuwa haki yake itapatikana hasa baada ya albamu hiyo kufanya vizuri sokoni.

Mbali na ombi hilo kwa Shigongo, msanii huyo pia ameomba kupewa fedha za mauzo ya wimbo wake “Seya” ambao ulitangazwa kushika namba moja kati ya nyimbo 50 za kituo cha Radio Clouds FM.

Alimalizia kwa kumuomba msimamizi wake wa awali kumpa ushirikiano wote Shigongo ili afanikiwe kupata haki yake ambayo ameifanyia kazi.

Album ya Salima ilitoka kati ya mwaka 2003/2004 ikiwa na ngoma zilizotamba kama Salima wenyewe, Fanta, Seya na nyinginezo kibao.
******************

20%: life ya mashindano kwangu no!
Staa wa Bongo Flava asiyependa makuu, Hamisi Kinzasa a.k.a 20% amesema na safu hii kwamba baada ya kuhamishia makazi yake town (Dar es Salaam) akitokea Kimanzichana, Pwani iliko familia yake alidondoka pande za Keinyama, lakini baada ya kugundua mitaa hiyo mastaa wengi wanaishi kwa mashindano ameamua kuhamia Kigamboni.

“Kwa upande wangu maisha ya kushindano no, huwa napenda niishi nitakavyo siyo kama walivyo wengine, akimuona fulani ana staleti naye anataka awe nayo au akiona huyu ana kile naye pia anataka awe nacho,” alisema staa huyo wa Money Money, Mama Neema na ngoma nyingine kali.
******************

Hostel ya Mr. Chuzi, Aunt Ezekiel kitaani
Kutoka ndani ya indastri ya muvi za Kibongo, safu hii ilidondoshewa ishu kwamba, ile filamu ya Hostel iliyogongwa na mastaa mbalimbali wanaofanya vyema katika game hiyo tayari imedondoka kitaani kupitia Kampuni ya Tuesday Entertainment.

Ndani ya safu hii, mwandaaji wa muvi hiyo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuzi’ alisema kwamba, filamu hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa fani hiyo nchini imeingia kitaani ikiwa katika DVD, VCD na VHS.

“Baadhi ya wasanii walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Aunt Ezekiel, Ahmed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mariam Jolwa ‘Jini Kabula na wengine wengi,” alisema Chuzi.
***************

Tollywood: Usaili mikoani baadaye
Kutoka ndani ya Kampuni ya Tollywood Movies waliyosimama vyema kuitetea sanaa ya filamu za Kibongo, safu hii imeambiwa kwamba, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao wameamua kusitisha zoezi la usaili kwa wasanii wa mikoa ya Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza na Visiwani Zanzibar waliyojaza fomu kwa ajili ya kushiriki kwenye muvi mpya zinazotarajiwa kuandaliwa na kampuni hiyo ikiwemo ‘Tears On Valentine Day’.

Ndani ya safu hii Mkurugenzi wa Filamu ndani ya kampuni hiyo, Hamie Rajabu alisema kwamba kutokana na hilo wanawaomba radhi wasanii wote kwa usumbufu waliyoupata wakati wa zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kushiriki kwenye filamu hizo.

“Sisi kama Tollywood tumesikitishwa na hilo, tunawaomba radhi wale wote waliyopoteza muda wao kwa kwenda kwenye vituo vyetu kwa ajili ya kujaza fomu za ushiriki. Lakini pamoja na yote hayo tunawaahidi kwamba, tunajipanga vizuri kabla ya kuendelea na zoezi hilo kwa siku ambayo tutaitangaza kupitia vyombo vya habari yakiwemo magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers,” alisema Hamie.

Aidha, mkurugenzi huyo alisema kwamba, katika filamu hizo mbili watawatumia wasanii zaidi ya 30 watakaofanikiwa kupita katika usaili uliyofanyika, Dar es Salaam hivi karibuni.
****************************
compiled by mc george

1 comment:

Anonymous said...

Kuna sinema inaitwa "hostel" ni horror ,ilitolewa hollywood miaka ya ya hivi karibuni.Kwa mwenendo huu sijui kam tutafika.haki ya nanai Tanznaia hata mtu kufanaya research ya jina tuu, au walau ubunifu ktk kutafuta jina ni issue.
Intia kinyaa.Aaarg!
Mchoswa