Sunday, August 30, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Sara Kaisi 'Shaa'
AY kupimana ubavu na Jigga, Shaa naye kuumana na mastaa kibao wa nje

Stadi wa Bongo Flava mwenye heshima ya kutosha, Ambwene Yesaya ‘AY’ anaona mzuka kupimana ubavu na mtu mzima Sean Cutter a.k.a Jay Z au Jigga.

Kama haujainyaka hii ni kuwa AY, amependekezwa kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop katika Tuzo za MTV Africa Music Awards. Katika category hiyo, AY anakamuana na nominees wengine kama Jay-Z, Kanye West wa Marekani, MI wa Nigeria na Zulu Boy wa Bondeni.

AY alisema kuwa anaona mzuka bin poa kupambana na Jigga pamoja na Kanye kwa sababu kitendo cha MTV kuwapambanisha kwenye category moja maana yake viwango vinalingana. “Hata nikishindwa, bado heshima itabaki kwangu, pia nimeteuliwa kufanya shoo siku ya event, kwahiyo nitapata nafasi ya kujitangaza zaidi kimataifa,” alisema AY. Mbali na AY, katika tuzo hizo, Mtanzania mwingine aliyekula shavu awamu hii ni Sara Kaisi ‘Shaa’ (kwenye picha kubwa juu) ambaye yupo ndani ya katika category ya Msanii Bora anayechipukia ambako anang’atana meno na nominees wengine kama MI, STL, Bigiano na Rhythimic Element.

Taratibu za kuwapigia kura AY na Shaa ili waweze kuibuka kidedea, zinatarajiwa kutajwa leo katika mkutano na waandishi wa habari kati ya wahusika wakuu na washiriki hao. Washindi watatajwa Oktoba 10, 2009, Nairobi, Kenya. Unaweza kutembelea website kama www.mama.mtvbase.com au www.mtvmama.mobi 4 more details.
*****************************

Mama’ke Chris Brown atoa sentensi yake kuhusu hukumu
Limesemwa hili na lile kuhusiana na staa wa R&B na Pop anayeminya kwenye himaya ya Obama, Chris Brown lakini mama yake alikuwa hajanena kitu kuhusiana na hukumu ya mwanaye.

Wiki iliyopita, mama wa Chris, Joyce Hawkins alitoa sentensi kadhaa kuhusiana na matatizo ambayo mwanaye ameyapata. Joyce aliviambia vyombo vya habari kuwa anawashukuru mashabiki wote wa Chris kwa kumfariji katika kipindi hiki kigumu.

Alisema: “Nasema kutoka moyoni, nashukuru kwa kuwa karibu na mwanangu, nilishindwa kulisema hili kwa sababu kesi ilikuwa bado inaendelea. Labda niseme tu kwamba tatizo hili limenisumbua na kuniumiza mno katika maisha yangu.” Hivi karibuni, Chris alihukumiwa kifungo cha nje miezi sita, kufanya kazi za kijamii kwa muda wote huo, pia akatakiwa na mahakama kuwa mbali na Rihanna kwa miaka mitano.

Hukumu hiyo ilimfika Chris baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Robyn Rihanna Fenty na kumuumiza. Hata hivyo, inaelezwa kuwa Chris hajutii kosa wala hajaumizwa na hukumu hiyo kwa sababu mara kwa mara anaonekana kiwanja akijirusha bila wasiwasi.

****************************
LL Cool J: Jamaa kacheki na watatu tu!
Ana jina kubwa na heshima tele katika kona za muvi na muziki hasa Hip Hop. Ni Ladies Love Cool James a.k.a LL Cool J.

Mtandao wa kimbeya ambao ume-specialize katika kufunua uhusiano wa mastaa umeambulia orodha kiduchu ya babies waliokwishajikunja naye on the bed. Ni warembo watatu tu ambao wametajwa ku-shear urojo na LL Cool J. Debbie Allen anatajwa wa kwanza lakini hakuna maelezo ya kutosha ni lini alichizika naye.

Simone Johnson anatajwa kuwa alichangamsha damu na mchizi huyo mwenye umbo la miraba minne mwaka 1995. Wakati Kidada Jones yeye alikuwa naye kati ya mwaka 2002 – 03. Kwa mujibu wa mitandao mingine Simone ndiyo mke halali wa LL Cool J ambaye amefanikiwa kuzaa naye watoto kadhaa.

Hii ni orodha fupi kutokana na staili ya mastaa kupenda kubadili wapenzi kama disposable instrument. Inawezekana pia akawa si msafi kihivyo, ila anajificha kwa sana. Jina lake kamili ni James Todd Smith, alizaliwa Januari 14, 1968, Queens New York, Marekani. Ana umri wa miaka 41. Ana urefu wa futi 6 1½. Je, wewe msomaji unapenda kujua uhusiano wa staa gani wa kiwanja? Tuandikie ujumbe mfupi 0715-110 173.
*************************
compiled by mc george

Friday, August 28, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Madee
Inawezekana ishu kubwa iliyopo kunako game ya muziki wa kizazi kipya hivi sasa ni kuendelea kubomoka kwa Kundi la Tip Top Connection la akina Madee(pichanij uu), kitu ambacho kimewafanya baadhi ya wadau wa burudani Bongo watutumie meseji nyingi wakitaka kufahamu mdudu gani hasa ambaye anatishia amani ndani ya umoja huo.

Kwa kumbukumbu za ShowBiz, alianza kuchomoka MB Dog huku mkononi akiwa na faili la sababu ikiwemo kuambulia mkwaja kiduchu kwenye mauzo ya albamu yake, akafuatiwa na Deso aliyekuwa akipiga kazi sambamba na Pingu ambaye pia aliitaja sababu kubwa ni kuambulia ankara za kitoto kwenye mauzo ya kazi yao.

Kabla watu hawajasahau, mwezi uliyopita ‘dogo’ Z-Anto naye alichomoka na kudai kwamba mkataba wake na familia hiyo umeisha hivyo ameamua kugeukia upande mwingine kwa kupiga kazi chini ya uongozi mpya ambao hajautaja hadi hii leo. Vile vile msanii Pingu ambaye alisimama vyema kwenye kolabo ya ngoma ya ‘Binti Kiziwi’ naye ameonesha nia ya kusepa kwani tangu alipochomoka Z-Anto hajawahi kutokea kunako maskani ya umoja huo wala kuambatana kwenye shoo yoyote ya Tip Top.

Hivi juzi msanii Spark aliyesimama vyema kwenye ngoma ya Nipe Ripoti na Tunda aliendelea kuipunguza kasi ngome hiyo kwa kuachia ngazi huku akiwa na sababu kibao, zikiwemo kutofaidika na umoja huo na kwamba ameamua kupiga kazi kivyake kwakuwa uongozi wa Tip Top haukua fea kwa upande wake na anachohangaikia kwa sasa ni safari yake ya muziki baada ya kujitoa kundini humo.

ShowBiz kama mdau namba moja wa burudani za Kibongo, hususan game ya muziki wa kizazi kipya iliamua kuingia mtaani ili kupata ukweli wa yote hayo na nini chanzo za wasanii hao kuendelea kujiengua Tip Top. Kwa kuanza ilipiga stori na msanii Hamad Ally a.k.a Madee ambaye ni memba namba moja wa familia hiyo ili kujua anauzungumziaje mmomonyoko huo.

“Mimi kama muasisi wa Tip Top Connection ambaye niliitoa Manzese na kuipeleka pande za Kagera wanapoishi viongozi wetu Abdul Bonge na Babu Tale bado sijajua kwanini wasanii hao wanaojitoa, hawataki kunishirikisha mimi kwakuwa wanapokuja mtu wa kwanza kukutana naye ni mimi ambapo baada ya kuwasikiliza nawapeleka kwa uongozi kabla ya kukubaliwa na kufanya kazi.

“Kwa mfano MB Dog siku ya kwanza kabisa alikuja na Cheleaman nikawasikiliza, baada ya kuona wako fiti nikawapeleka kwa kina Bonge japo baadaye Chelea alijitoa akabaki Dog peke yake ambaye alikuja pale hana kitu lakini alisikika na kuwa na mafanikio, cha ajabu wakati anaamua kujitoa hakutaka hata kuniambia, nikamsikia kupitia vyombo vya habari tu.

“Vile vile kwa Pingu na Deso ilikuwa hivyo hivyo japo wao hawakupata mafanikio makubwa sana kutokana na albamu yao kufanya vibaya sokoni, lakini walimudu maisha ya kujitegemea kupitia Tip Top. Ukiachia mbali na hao, msanii kama Z-Anto kafanyiwa vitu vingi sana na Tip Top lakini mwisho wa siku hakutaka hata kuniomba ushauri mimi kabla ya kutoka.

“Kwa upande wa Spark ndiyo usiseme, alikuja pale kupitia mimi nikampeleka kwa Abdul Bonge japokuwa alionesha kumkataa, nikiwa na Babu Tale (Meneja msaidizi) tulimsimamia mpaka akafanikiwa kuwa juu kupitia umoja wetu, lakini nashangaa leo hii anajitoa bila kutaka ushauri wangu mimi kama msanii mwenzake zaidi ya kuulaumu uongozi.

“Kuhusu hayo yote mimi kama mwana Tip Top halisi napenda kuwashauri wasanii waliopo na waliojitoa kundini kwamba, wasipende kutumia njia hiyo ili kujitangza zaidi kwani kuna wengine huwa wanatoka na kurudi, muziki ni maisha yao wanachotakiwa kufanya ni kuangalia ni kitu gani hasa wanakipata katika sanaa hii, siyo baada ya miaka kadhaa inabaki historia tu kuwa fulani zamani alikuwa msanii bila kuwa na aset yoyote,” alisema Madee.

Kwa upande wake meneja msaidizi wa kundi hilo, Babu Tale ambaye ndiye amekuwa akilalamikiwa zaidi alisema kwamba hahitaji kuwazunguzia sana wasanii waliojitoa bali amegundua kwamba kufanya kazi kiushikaji bila kuwa na mikataba ya kueleweka ni tatizo, kitakachofuata hivi sasa ni kujipanga upya kwani anaamini Tip Top haitakufa kwa sababu ya wasanii waliotoka.

“Unajua mimi ningeandikishiana mkataba na msanii kama Tunda ningemfunga tu, kwakuwa asingweza kuufuata ndiyo maana nikaamua tufanye kazi kiushikaji, lakini madhara yake tumeyaona na tayari tumejifunza kitu. Siyo kwamba najisikia vibaya wasanii wakijitoa isipokuwa inanikera zaidi pale wanapokwenda kunizungumzia vibaya wakati nimewafanyia mambo mengi ambayo hawakutarajia. Zaidi nawatakia mafanikio mema katika safari ya muziki wao,” alisema Babu Tale ambaye pia alimuwakilisha Abdul Bonge.

Je, wewe mdau wa burudani una lolote kuhusiana na ishu hii, tuambie kwa meseji 0715-110 173 ili tuwarushie wahusika.
*******************************************************

Ijumaa Sexiest barchelor: Here we go!
Safari ya Ijumaa Sexiest Bachelor 2009-2010 inachukua nafasi pana kwa wakati huu. Piga kura ili jamaa unayeamini ana mvuto kuliko wengine aweze kuibuka kinara.
Mchakato wa awali umepita na sasa mbele yako yapo majina 12 ambayo mmoja wao ndiye Ijumaa Sexiest Bachelor ajaye, atashinda vipi? Kura yako ndiyo mwamuzi.
Piga kura kwa kuandika jina lake na kulituma kwenda simu namba
0787 1101173 au 0713-355 717.
******* ***************************************************************************

*********************************************************************
Ni zamu ya AY, Shaa MTV
Staa wa Bongo Flava, Ambwene Yesaya ‘AY’ anang’ara kimtindo sasa na katika hilo MTV Music Awards imemuona, Chile Kasoga anashuka nayo.

AY ametajwa kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop ambako katika category hiyo anachuana na nominees wenzake kama Jay-Z, Kanye West, M1 wa Marekani pamoja na Zulu Boy wa Bondeni.

Sara Kaisi ‘Shaa’ naye ndani ya nyumba katika category ya Msanii Bora Anayechipukia ambako anang’atana meno na nominees wengine kama M1, STL, Bigiano na Rhythimic Element. Ukipiga kura kwa Shaa na AY utakuwa umewawezesha kufikia patamu. Cheki Ijumaa Wikienda katika Abby Cool & MC George over the weekend Jumatatu ijayo, utapata maelezo ya jinsi ya kupiga kura. Washindi watatajwa Oktoba 10, 2009, Nairobi, Kenya.
************************************************

Helen aahirisha uzinduzi
Uzinduzi wa mdada anayefanya Gospel ya ukweli, Helen Njama hautochukua nafasi kesho kutwa (Jumapili) kama ratiba ilivyoongea na badala yake amewataka fans wake kungoja schedule mpya.

Helen alichek na Showbiz mapema wiki hii kwamba amelazimika kuahirisha uzinduzi huo kutokana na maombi ya mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, kufiwa.

Rekebisha mambo Helen, tunaumia kusubiri.
****************************************************

compiled by mc george

Thursday, August 27, 2009

Zijue faida za kufunga kiafya

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ndiyo umeshawadia na waislamu wako kwenye funga ya muda wa siku 30 au 29 kuanzia Jumamosi iliyopita. Kama tujuavyo, funga ni nguzo ya nne miongoni mwa nguzo tano za uislamu, ambapo ni lazima kufunga kwa mtu mzima na mwenye afya njema.

Kuna funga za aina nyingi, lakini kubwa ni ya kiroho ambayo waumini hufunga kwa ajili ya kutii maamrisho ya Mungu, ingawa ufungaji wake unatofautiani kutoka dini moja hadi nyingine. Wakati waislamu wanafunga kwa kutokula kitu chochote kuanzia asubuhi hadi jua linapozama, wakristu wao wakati wa funga huruhusiwa kula, lakini kwa kiasi na utaratibu maalum.

Tunaposikia neno kufunga, wengi tunaliangalia tendo hilo kwa upande wa kiroho kuwa ni amri ya Mungu ambayo tunapoifuata tunapata thawabu. Funga pia huchuku?iwa kama njia moja wapo ya kufanya maombi maalum kwa Muumba ili kujibiwa maombi yetu kwa namna ya kipekee.

Kama ambavyo mtu akifunga na kufuata sawasawa mafundisho yote ya funga anavyopata fadhila kutoka Mungu, ndivyo ambavyo pia mtu huyo anaweza kupata faida za kimwili kutokana na funga hiyo.
Katika ulimwengu wa sasa, funga imegundulika kuwa njia bora ya kupambana na maradhi mbalimbali na hatari mwilini, ambayo katika hali ya kawaida yameshindikana kutibika kwa kutumia tiba za kisasa.

Ingawa funga inaonek?na kama ni ibada fulani ngumu kwa baadhi ya watu, lakini Mungu bila shaka alikuwa na siri kubwa na aliamrisha tufunge kwa faida ya miili yetu na pengine kama watu wote wangekuwa wanafunga kama inavyotakiwa, bila shaka maradhi mengi yangepungua.

NINI FAIDA ZA FUNGA KIAFYA?
Faida za kufunga za kimwili ziko nyingi, zikiwemo kuponya mwili. Unapofunga una upa nafasi mwili wako kupumzika na kujitengeneza upya wenyewe. Funga inaupa nafasi mwili kuondoa sumu sehemu mbalimbali za mwili ambazo zilijijenga kwa muda mrefu.

Halikadhalika funga hufufua upya chembecheme hai za mwili, huboresha mfumo wa hewa. Tofauti na imani kuwa mtu mwenye njaa hukosa nguvu, funga huongeza nguvu za mwili na uchangamfu wa akili pia.
Baada ya wataalamu mbalimbali wa sayansi kugundua kuwepo kwa faida kubwa ?a kufunga, wamebuni funga zingine zenye lengo la kuboresha afya tu na siyo kwa mambo ya kiroho. Kuna aina nyingi za funga, kama vile kufunga kula vyakula vyote isipokuwa juisi ya matunga tu kwa siku kadhaa.

Aina nyingine ya funga ya tiba ni ile ya kufunga kula vyakula vyote, isipokuwa kunywa maji peke yake kwa muda maalum. Funga za aina hii huwa ni za muda maalumu zikiwa na lengo maalumu, ama kupunguza uzito, kutibu shinikizo la damu, kisukari ama magonjwa mengine. Hata hivyo inashauriwa mtu kujijua hali yake ya kiafya kwanza kama kabla ya kufunga.

Hivyo, ni ukweli ulio wazi kuwa waislamu au wakriostu wanapofunga ili kutekeleza amri ya Mungu, wanapata faida nyingine ya kiafya bila wao kujijua. Hata utafiti wa kawaida nchini unaonesha kuwa watu wanaofunga hali zao kiafya huimarika sana katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani na hata idadi ya wagonjwa huripotiwa kupungua hospitali.
JE, FUNGA INAFANYAJE KAZI MWILINI?
..itaendelea wiki ijayo

(Samahani sana wasomaji wangu wa makala haya, kwa kuchelewa nilighafirika, nilidhani nilishapost)

Wednesday, August 26, 2009

Chris Brown ahukumiwa!

Mkali wa miondoko ya R&B, Cris Brown wa Marekani, amehukumiwa miaka mitano kifungo cha nje katika ile kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumpiga mpenzi wake wa zamani, Rihanna. Jaji wa mahakama Kuu ya Los angeles, Patricia Schnegg, amemtaka Chriss kukaa mbali na Rihana kwa miaka mitano ijayo, umbali usiopungua mita 100, unless wawe wanahudhuria ishu ya muziki. Pia kijana huyo amehukumiwa miezi sita ya kufanyakazi za kijamii. jaji amemuonya iwapo atakiuka masharti ya hukumu hii, atatupwa 'segerea'!!

Tuesday, August 25, 2009

Friday, August 21, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

IJUMAA SEXIEST BACHELOR: Jerry Tegete, Makamua ndani ya mpambano, kura wiki ijayo
The Soccer Bongo, Jerry Tegete na vocalist wa kiwango cha juu katika eneo la muziki wa R&B nchini, Makamua a.k.a Mwana wa Sekimanga wamepigiwa kura ya kuingia katika Top 12 ya Ijumaa Sexiest Bachelor 2009.

Kama unainyaka uzuri ni kwamba wiki iliyopita, tulitoa majina ya wakali wanne, ukitakiwa kupiga kura ili kuchagua watu wawili ambao wanatosha kuingia katika Top 12 kabla ya kuchapa mwendo kuelekea kumpata mshindi wa taji.

Orodha ni hiyo, wiki ijayo tutatoa taratibu maalumu ya wewe kushiriki kunako mpambano huu kwa kupiga kura. Tuko sawa.

***********************************************



KWA SATILI HII, KANUMBA KAFUNIKA!
Wengi wamezoea kumuona Kanumba akiigiza kwa kutumia magari na nyumba za kifahari maeneo ya mijini, lakini safari hii amekuja tofauti baada ya kuigiza filamu yake ya Village Pastor akiwa katika maisha duni ya kijijini.

Wakiongea na ShowBiz, wadau wa filamu Bongo, ambao wameona picha alizopiga Kanumba akiwa anaendesha baiskeli na akiwa amaevaa nguo za kizamani kijijini, walisema kuwa filamu hii itafunika zingine alizowahi kucheza kijana huyu ambaye kwa sasa anatamba na muvi yake mpya ya The Director ambayo amewashirikisha wasanii kibao maarufu kutoka Nigeria.

Village Pastor amecheza na mwanadada Aunt Ezekiel ambaye naye ameigiza kama mpenzi wa Kanumba kijijini na kufunika vilivyo.....kaa mkao wa kula kuiona filamu hii inayotarajiwa kuingia mtaani hivi karibuni.
**********************************************






Tears on Valentine’s Day: Ni Next Level!
Muvi ambayo inaendelea kurekodiwa hivi sasa, Tears on Valentine’s Day (kama pichani juu) itakuja na vitu tofauti ambavyo waandaaji wengi wa Bongo huvikwepa wakati wa kuandaa filamu zao kutokana na kukwepa gharama.

“Tunataka kuonesha kuwa Tanzania tunaweza kuwa mbele zaidi, muhimu ni kujipanga. Wasanii tuliowachukua kwa ajili ya kurekodi ni wa kiwango cha juu sana (Next Level), mandhari inayotosheleza mahitaji ya stori ya filamu na picha za kiwango cha juu,” alisema Hamie ambaye ndiye muongozaji wa muvi hiyo.

**********************************************

Kingwendu alizwa M na nusu
Komedian aliyekwenda eji Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ ameingizwa mjini na promota mmoja jijini Mwanza.

Kingwendu spoke to Showbiz mapema wiki hii kwamba, promota huyo amemtia ndani kiasi cha fedha shilingi milioni 1.5 ambazo aliziingiza baada ya kupiga mzigo Kanda ya Ziwa.

Said: “ … (anataja jina la mtu aliyemliza) amenifanyia kitu kibaya sana, alinichukua vizuri Bongo akanipa advance, kula, kulala haikuwa na matatizo, kwahiyo nikamuamini lakini kumbe siyo mtu kihivyo.

“Baada ya kupiga shoo kwenye vijiji vya Zalagula, Kasaratu, Nyanango na Kanyala jijini Mwanza, nilikuwa nimekusanya shilingi milioni 1.5 kibindoni lakini juu kwa juu nilipata ‘dili’ kwahiyo nikaunganisha shoo.

“Promota wangu aliniomba nimpe pesa hizo ili akaniwekee kwenye akaunti yangu, mimi kwa sababu nilikuwa nimeshamuamini nilimpa lakini huwezi kuamini, baada ya hapo kila nikimpigia simu ni stori tu. Hivi sasa nimemfungulia mashataka polisi kwa kosa la wizi wa kuaminiwa.”
***********************************************
compiled by mc george

Tuesday, August 18, 2009

Chumvi na sukari: Vinaongoza kwa kuliwa, lakini ni hatari

Kama kauli mbiu ya makala haya inavyosema kila siku, Jinsi Ulivyo kunatokana na unavyokula, ndivyo ambavyo vyakula tajwa hapo juu, vinaweza kuwa mwilini mwako. Ukivila kama inavyotakiwa vina faida na ukila tofauti vina madhara kwako. Jinsi utakavyovitumia ndivyo utakavyokuwa kiafya. CHUMVI Chumvi ni miongoni mwa bidhaa muhimu ya kila siku kwa binadamu kwa upande wa chakula.

Kwa namna moja ama nyingine kila siku mtu analazimika kula chumvi, iwe kupitia mboga au vitafunwa vingine vilivyotayarishwa kabisa. Kwa bahati mbaya watu wengi wanakula kiasi kikubwa sana cha chumvi kuliko inavyohitajika na katika ulaji huo hula aina ya chumvi isiyo sahihi pia. Matokeo yake, chumvi hugeuka mwilini kuwa chanzo cha magonjwa sugu, kama ya presha.

Aina ya chumvi inayopendekezwa na wataalamu wetu kutumiwa na isiyo na madhara katika afya zetu ni chumvi asilia, kama vile chumvi bahari na kadhalika. Vile vile ni kiwango kidogo sana ambacho tunatakiwa kutumia kwa siku, ni makosa makubwa kuweka kiasi kingi cha chumvi kwenye chakula unachokula, kwa sababu tu unapenda ladha yake.

Wako watu ambao hupenda kuweka kiasi kingi cha chumvi katika milo yao ili kupata ladha aitakayo, bila kujua kiwango kinachohitajika mwilini ni kidogo, matokeo yake huwa ni kupata madhara mengine mwilini. SUKARI Kuna aina mbili kuu za sukari. Sukari Nyeupe na Sukari Nyekundu. Sukari nyeupe inaelezwa kuwa sukari mbaya na hatari kiafya kuliko kitu kingine. Lakini kinyume chake, sukari nyeupe ndiyo imekuwa chaguo la watu wengi wanapofanya ununuzi wa sukari dukani.

Inaelezwa kuwa ubaya wa sukari nyeupe unatokana na hatua inayopitia kiwandani ambayo mwisho wa siku inaondolewa virutubisho vyake vya asili na kubaki ‘makapi’ ambayo hayana faida yoyote mwilini zaidi ya kuletea ladha tamu na ya kupendeza mdomoni. Badala yake inashauriwa tutumie sukari ‘nyeusi’ (brown sugar)ambayo yenyewe inakuwa bado haijaoendolewa virutubisho vyake vya asili vinavyohitajika mwilini.

Rangi ya nje inaweza isikupendeze machoni, lakini iingiapo mwilini inaweza kuwa na faida sana. Kama itawezekana, ni bora ukaacha kabisa kutumia sukari na badala yake upendelee asali halisi. Uzuri wa asali, ambayo ina kiwango kikibwa cha sukari kisicho na madhara, unaweza kuitumia katika vinywaji na vyakula mbalimbali na kupata ladha nzuri.

Kwa kuwa bidhaa hizi mbili ni muhimu katika mahitaji yetu ya kila siku, na kwa kuwa ndiyo bidhaa tunayoitumia kwa wingi, ni vyema basi tukahakikisha tunajua kiwango na aina tunayotakiwa kuitumia kwa siku, ili tupate faida badala ya madhara kiafya.

ZOMBE AKISALIMIANA NA MAWAKILI WAKE

Monday, August 17, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

ALIKIBA KWA KULA USIPIME!
Good sound, beat and rhythm ni vitu ambavyo vinaipaisha singo mpya ya fundi wa vocal za kubembeleza Bongo, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’.

Traki inatambaa kwa jina la Napenda Kula, ndani yake ‘bwa mdogo’ hajasumbua kichwa kutoa mistari yenye meseji ila alichokifanya ni next level. Mzigo umesimama na ukiusikiliza unavunja mbavu.

Sikia; alivamia sherehe bila kualikwa, akanawa na kuanza kuchota pilau kwa mikono, tonge nyama, tonge nyama, waungwana wakaona dogo anawazingua, spidi kali wakati siyo mhusika, wakamtoa baruti.

Unadhani walipomfukuza palikalika? Alienda kununua mayai, bila shaka ni viza, sherehe ikavurugika, dogo aliwachachafya vibaya na mayai. Mzigo umesimama. Upo vizuri, chapa mwendo, one day utaitwa mfalme.

########################################################

TEARS ON VALENTINE
Itabadilisha movie industry Bongo
Filamu ambayo inarekodiwa hivi sasa, Tears on Valentine’s Day inatajwa kwamba itakuja na vitu tofauti ambavyo waandaaji wengi wa Bongo huvikwepa wakati wa kuandaa muvi zao kutokana na kukwepa gharama au kuzidiwa ujanja na teknolojia.

Mkurugenzi wa Filamu katika Kampuni ya Tollywood Movies inayoandaa filamu hiyo, Hamie Rajab amenong’ona na Abby Cool & MC George over the weekend kwamba zoezi zima la kutengeneza muvi hiyo limezingatia maeneo mengi ya kisasa.

“Tunataka kuonesha kuwa Tanzania tunaweza kuwa mbele zaidi, muhimu ni kujipanga. Wasanii tuliowachukua kwa ajili ya kurekodi ni wa kiwango cha juu sana, mandhari inayotosheleza mahitaji ya stori ya filamu na picha za kiwango cha juu,” alisema Hamie na kuongeza:

“Waandaaji wengi hukwepa vitu fulani fulani wakati wa kurekodi filamu zao kutokana na gharama au teknolojia lakini ndani ya Tears on Valentine’s Day utaona maendeleo ya kiteknolojia ambayo Tollywood inayo na tumekubali kuingia gharama kubwa ili kutoa kitu bora.”

##################################################

Samantha
Sisqo
Eminem

SAMANTHA MUMBA: KUMBE AMEWAHI KUJIKUNJA NA EMINEM!
Yupo kimya sana hivi sasa lakini Ebwana Dah! Imeona si kihivyo, that’s why ikaingia kunako intaneti na kufunua orodha ya njemba ambazo yeye amewahi kutoka nazo kimahaba.

Kwa mujibu wa kile ambacho tume-capture kwenye site inayodili na ishuz za uhusiano wa mastaa mbalimbali wa mtoni, Samantha amekwishajituliza kwa vidume watano katika mtindo unaokuijia hapo chini.

Inawekwa hivi, mwaka 1998 mpaka 2003 alikuwa amejituliza kwa Mark Henderson lakini mwaka 2000 alicheza pembeni na kujikunja na Colin Farrell, 2001 alikubali kupumzika kwa kichaa Bruce Mathers III ‘Eminem’ kabla ya mwaka 2005 kuangukia kwa Charles Porter ambaye yupo naye mpaka sasa.

Hata hivyo, mwaka 2005 aliwahi kutuliza ‘mizuka’ kwa Sisqo ambaye walichangamshana damu kwa muda.
#############################################

...coming soon

compiled by mc george

Friday, August 14, 2009

Karibu Nyumbani

Kwa moyo mkunjufu na wa heshima tele, naomba niwakukaribishe katika kauwanja kangu japo kameanza muda mrefu kidogo uliopita. Nahitaji sana maoni yenu ili kuboresha kazi hii.
Karibu sana kila mpatapo muda jamvini www.karibunyumbani.blogspot.com

UTOTO BWANA!



Kwa picha zaidi nenda; nifahamishe.com

SASA NI AUGUST..HAIJAFUNGULIWA..WHY?

IJUMAA SHOWBIZ!

washindani hawa hapa
Yusuf Mlela, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Tundaman, Hemed, Chid Benz, Ray, Kanumba, Mwisho Mwampamba, Black Rhino na AY ni majina 10 ambayo yamepata kura nyingi zaidi ili kuendelea kwenye shindano.

Hata hivyo, lengo ni kupata majina 12 ili kuchapa mwendo kuelekea kumpata mshindi. Majina yafuatayo, yamepata kura zinazolingana kwahiyo kati yao, unatakiwa kutuma sms ukitaja jina la mmoja wao ili wawili waungane na wenzao hapo juu.

Spark, Makamua, Jerry Tegete na Danny Mrwanda kati yao tuma machaguo mawili, watakaoongoza wataungana na wenzao 10. Dondosha kura kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu namba 0787-110 173, e-mail:mcgeorge2008@gmail.com, ili shindano lianze kuchapa mwendo.
*** *********************************************

Steve
Bwa mdogo mwenye vocal inayokamata, Steven William ‘Steve’ ndiye artist anayeng’ara zaidi hivi sasa Bongo na kuzidi kuiweka R&B juu ya mstari.

Traki inayokwenda kwa jina la Sogea Karibu ambayo Steve ameifanya pamoja na Dataz inabamba namba moja katika singo zote za R&B ambazo zinapasua anga kwa sasa, hiyo ni kwa mujibu wa tathmini ya ShowBiz.

Janki huyo ambaye anapatikana kwenye lebo ya Zizzou Entertainment, ameanza kukamata hapa juzi kati hasa baada ya kufanya wonderful chorus katika ngoma ya Tabasamu aliyopewa shavu na Heri Samir ‘Blu’ lakini janki amekwishafanya mengi katika industry.

Hivi sasa amekwishakamilisha mawe nane ambayo anatarajiwa kuyajaza katika albamu yake ya kwanza.

“Muda si mrefu nitaachia wimbo wangu mwingine unaoitwa Baby Girl ambao nimefanya na Ngwair, hii ni baada ya kuona Sogea Karibu umekubalika,” alisema Steve.
Do u need more from Steve? Stay tuned.
****************************************

Tears On Valentine day: wasanii waingia mzigoni kupiga picha
Ile muvi ya kijanja, itakayosheheni wasanii wa ukweli, yaani vipaji asilia imeanza kurekodiwa katika allocation za Jiji la Dar, ebwana eeh!

Showbiz imepewa mnuso huu na Mkurugenzi wa Filamu wa Tollywood Movies, Hamie Rajab kwamba mambo yanapamba moto na kuongeza kuwa staili ya kurekodi uhondo mzima ni ya aina yake.

Hamie alisema kuwa kilichomvutia zaidi ni kuona kwamba zoezi ambalo Tollywood ilifanya la kusaka wasanii wenye vipaji kwa ajili ya filamu hiyo limekuwa ni lenye faida kubwa.

“Tumepata wasanii ambao wanaonesha uwezo mkubwa, yaani hawamsumbui mwongozaji wakati wa kurekodi wakiambiwa kitendo wananasa papohapo, hayo ndiyo matunda ya vipaji,” alisema Hamie.
*******************************************
COMPILED BY MC GEORGE

Wednesday, August 12, 2009

Fungua kinywa na kilicho bora kiafya


KWa maisha ya watu wengi nchini mwetu, chakula cha kwanza kuingia mwilini huwa ni ama chai, maziwa au soda na kufuatiwa na vyakula vya kupika na mafuta kama maandazi vitumbua, n.k., vyakula ambavyo viko kwenye kundi la vyakula hatari na ambavyo hutakiwa kuliwa kwa tahadhari kubwa.

Hiyo siyo staili nzuri sana ya maisha, kwa kuanza siku yako nyingine aliyokujaalia Mungu kwa kula chakula kisichohitajika sana na mwili, siyo jambo zuri. Badala yake mwili unahitaji chakula asilia ili uweze kujijenga na kujiweka sawa kwa kupambana na maadui wapya wa siku hiyo.

Hivyo, wataalamu wetu wanatushauri kuanza siku vyema kwa kula tunda lolote salama, juisi ‘fresh’ ya aina yoyote au maji angalau tu. Vitu hivi ni bora na muhimu sana kuanza kuingia tumboni badala ya vyakula vingine vya kukaanga. Hata kama huna uwezo wa kununua matunda mengi, lakini angalau anza kwa kula hata chungwa moja au ndimu, ambayo faida yake mwilini ni kubwa kuliko sukari.

Unaweza kushindwa kununua matunda au kutengeneza juisi, lakini huwezi kushindwa kupata maji ya kunywa. Kama tunavyoambiwa kila siku, maji ni kitu muhimu sana katika mwili wa binadamu na kuanza kunywa maji asubuhi, hasa ya uvuguvugu, ni dawa kubwa sana ya maradhi mengi na ni ufagio mzuri wa kuondoa mafuta na mabaki mengine katika njia ya mfumo wa damu mwilini. Watu wengi huogopa kunywa maji asubuhi kwa kudhani wataumwa tumbo, ukweli ni kwamba huwezi kuumwa tumbo kwa kunywa maji, muhimu ni kuhakikisha yawe safi na salama.

Maji yanaweza kukutibu tumbo kwani hata kama una matatizo ya kupata choo, kwa kunywa maji mengi asubuhi choo hufunguka na kuwa laini. Hivyo baada ya kuanza siku yako kwa kutanguliza chakula asilia tumboni mwako, iwe tunda, juisi au maji, kaa angalau kwa muda wa nusu saa ndiyo ule mlo wako kamili wa asubuhi. Kama umezoea kunywa chai asubuhi, jaribu kunywa chai yenye mchanganyiko wa viungo vingine kama tangawizi au mdalasini.

Aidha, kinywaji bora zaidi kuanza nacho baada ya kufungua kinywa na matunda ni Uji, hasa wa ulezi uliotengenezwa kwa kuzingatia suala la virutubisho. Usianze kufungua kinywa asubuhi kwa kunywa soda, ambayo haiingizi kirutubisho chochote mwilini mwako, zaidi ya kukuongezea sukari ambayo inapokuwa nyingi huweza kunenepesha na kuwa chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Aidha, unywaji supu ya nyama ya ngo’mbe au mbuzi asubuhi, nao siyo mzuri sana. Vyakula vitokanavyo na wanyama vingi huwa na mafuta, ambayo tumeshaona ni miongoni mwa vyakula hatari. Ieleweke kwamba si vyakula vyote vyenye ladha ya utamu mdomoni ni vizuri tumboni, chakula kinaweza kuonekana kizuri mdomoni, lakini tumboni kibaya.

Na ni wazi kwamba ukila vizuri utakuwa na afya njema na bila shaka ukila vibaya, utakuwa na afya mbaya, maradhi yatakuwa hayakuishi. Tunapaswa kujua kula vizuri ni kupi nakula kubaya ni kupi.

Kanuni ambayo unaweza kuitumia ni ile ya kupendelea kula sana chakula asilia na hai (natural and fresh), kama vile matunda, mboga, vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, (mahindi, ngano) au mchele wa rangi ya kijani (brown) na kujiepusha na ulaji mkubwa wa vyakula vya kukaanga na kupikwa na mafuta mengi.

Kongamano

Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.

Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.

Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii (social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.

Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :
Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.
Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com. Zingatia tarehe za kujiandikisha.
Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano. UMOJA NI NGUVU!

Monday, August 10, 2009

Hatimaye Michael Jackson Azikwa


Hatimaye mwili wa mfalme wa muziki Pop, Michael Jackson aliyefariki juni 25 mwaka huu umepumzishwa kwenye nyumba yake milele.Mwili wa Michael Jackson ambaye alifariki juni 25 mwaka huu, hatimaye umepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huku familia yake ikikanusha madai ya rafiki yake wa karibu Mark Lester ambaye alidai kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa kike wa Michael Jackson, Paris. Familia ya Michael Jackson ilisubiri wiki kadhaa kabla ya kuamua kuuzika mwili wake baada ya ubongo wake kuchukuliwa kwaajili ya uchunguzi zaidi juu ya kifo chake. Ubongo wake ulirudishwa kwenye mwili wake wiki iliyopita. Michael Jackson alizikwa kwenye makaburi ya Forest Lawn Cemetery yaliyopo Hollywood Hills, huku mazishi yake yakifanyika kimya kimya na kuhudhuriwa na familia yake pekee. Hakuna shabiki yoyote wa Michael Jackson aliyealikwa kwenye mazishi hayo na familia yake ilifanya mazishi hayo kwa siri kwa kuhofia maelfu ya mashabiki wake watatembelea makaburi hayo na kusababisha hali ya usalama wa kaburi lake kuwa mashakani. zaidi: nifahamishe.com

WIKIENDA SHOWBIZ!

Ngoma ya Hip Hop inayochangamsha masikio kwa sasa, Msela ambayo imegongwa na machizi wa kitambo kwenye game, Wateule inaweza kuibua maswali hasa kwa upande wa video.

Iko hivi, ngoma hiyo ambayo imefanywa na wakongwe, Taikun Ally ‘Mox’, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Jafari Msham ‘Jafarai’ na Msafiri Kondo ‘Solo Thang’ inasikika kamili ikiwa na verse nne katika audio wakati kwenye video zipo tatu.

Tofauti kubwa ni hii, kwenye audio magalacha hao wamesimama wote, wakati katika video Solo hayumo, yaani hajauza sura wala sauti yake haisikiki. Why? Jafarai anajibu: “Ilibidi tufanye hivyo mzee, Solo yupo bize sana kwahiyo tulimkata kwenye video ili kuiwahi ngoma kabla haijapotea kwenye game.

“Wakati tunafanya video Solo alikuwa anakabiliwa na mitihani, tukaona tumkate kwa sababu alikuwa bado hajarekodi video na kutuma clip zake tuziunganishe, lakini no sweti, kuna dude lingine tumelifanya, ‘Mtaani kuna njaa’ humo Solo ataonekana kideoni.”

**********************************************

THE DIRECTOR YA KANUMBA KITAANI
TEARS ON VALENTINE DAY NI LEVO YA HOLLYWOOD
Wakati filamu ya The Director ambayo imefanywa kijanja na Ijumaa Sexiest Bachelor 2007, Steven Kanumba, na wakali wengine kutoka TZ na Nigeria ikiwa inafanya vizuri kitaani, kuhusu muvi ya Tears on Valentine Day mambo yako levo kimataifa kama Hollywood.

Abby Cool & MC George over the weekend, imefanya tathmini kitaani na kushuhudia jinsi wajanja wanavyoigombania The Director ambayo ni moja kati ya muvi za kiwango cha juu iliyowahi kuzalishwa Bongo, pia ikazama kambini na kuwaona wasanii wanaofanya mazoezi kwa ajilia ya Tears on Valentine Day.

Tulichokinyaka ni kwamba Tears on Valentine Day ni kiwango cha juu sana, wasanii walivyo siriaz katika mazoezi na uwezo wao, hadhi ya kambi kwenye Hoteli ya The Atriums, Sinza Afrikasana, Dar pamoja na mambo mengine, ni vitu ambavyo vinaifanya filamu hiyo iwe inaandaliwa kisasa zaidi kama vile Hollywood, USA.

***************************************************

TONI BRAXTON AMESHAJIKUNJA NA KASUKU WANNE TU!
Ni mwanamama ambaye amekwenda eji lakini katika muonekano bado anayumbisha hisia za new generation kutokana na mvuto alionao. Ni Toni Braxton ambaye leo ndiye anayeangazwa na Ebwana Dah!

Amekwishajikunja kimahaba na wanaume wangapi? Ni katika kipindi gani? Amedumu nao vipi? Cheki majibu hapa chini!

Kwa mujibu wa tovuti inayofuatilia ishuz za mastaa hususan uhusiano wa kimapenzi, inawekwa wazi kwamba Toni aliwahi kubiliguana na jamaa anayekwenda kwa jina la Curtis Martin katika kipindi ambacho hakijawekwa wazi.

Inabainishwa pia kuwa baadaye mwanamama huyo alijiweka kwa Frankie Beverly, pia haiwekwi wazi ni wakati gani na kati ya mwaka 1994-95, alifanya sanaa ya utu uzima na Shemar Moore.

Tangu mwaka 2001, amejituliza kwa Prodyuza Keri Lewis ambaye ndiye mumewe halali wa ndoa na inaonekana hana mpango na kasuku wa pembeni. Hii inaleta mshangao, kwani kwa sifa za Toni anavyochukuliwa kama mwanamke kicheche, wengi walidhani angekuwa amejikunja na wanaume wengi zaidi ya hapo.

Jina lake kamili ni Toni Michelle Braxton, umri wake ni miaka 42, alizaliwa Oktoba 7, 1966, Severn, MD, Marekani. Ana urefu wa futi 5.2, alibukua Chuo Kikuu cha Bowie State, Marekani
*********************************************


MADHILA 2: BADO SIKU 14 TU!
Muvi ya ukweli ambayo inatajwa kusheheni characters wenye akili, amazing pictures & sound pamoja na ujumbe mzito unaoigusa moja kwa moja jamii ya Kitanzania, Madhila Part II ipo tayari na baada ya siku 14 itapakuliwa kitaani.

Ofisho ripoti kutoka kampuni mkombozi wa vipaji nchini, Tollywood Movies ambayo ndiyo yenye authority ya kusambaza filamu hiyo Bongo, inaweka wazi kwamba kila kitu kinakwenda sawasawa, kwahiyo bado siku 14 ili utamu uingie sokoni.

Ndani ya dude hilo utaona jinsi Salim Mbwana a.k.a Salu ambaye anabeba uhalisia wa watu wenye ulemavu, anavyofanyiwa kila aina ya hujuma, wafanyakazi wenzake wanamtenda umafia lakini mwisho wa siku Mungu alifanya yeye kuwa mshindi. Alishindashindaje? Hii si ya kukosa!

Ndani ya Madhila part II, utakutana na mtaalamu wa kucheza na kamera, Riyama Ally, staa wa tangazo la Haki Elimu, Nuru Njaidi (Huba) na wengineo kibao.

COMPILED BY MC GEORGE