Monday, August 10, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Ngoma ya Hip Hop inayochangamsha masikio kwa sasa, Msela ambayo imegongwa na machizi wa kitambo kwenye game, Wateule inaweza kuibua maswali hasa kwa upande wa video.

Iko hivi, ngoma hiyo ambayo imefanywa na wakongwe, Taikun Ally ‘Mox’, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Jafari Msham ‘Jafarai’ na Msafiri Kondo ‘Solo Thang’ inasikika kamili ikiwa na verse nne katika audio wakati kwenye video zipo tatu.

Tofauti kubwa ni hii, kwenye audio magalacha hao wamesimama wote, wakati katika video Solo hayumo, yaani hajauza sura wala sauti yake haisikiki. Why? Jafarai anajibu: “Ilibidi tufanye hivyo mzee, Solo yupo bize sana kwahiyo tulimkata kwenye video ili kuiwahi ngoma kabla haijapotea kwenye game.

“Wakati tunafanya video Solo alikuwa anakabiliwa na mitihani, tukaona tumkate kwa sababu alikuwa bado hajarekodi video na kutuma clip zake tuziunganishe, lakini no sweti, kuna dude lingine tumelifanya, ‘Mtaani kuna njaa’ humo Solo ataonekana kideoni.”

**********************************************

THE DIRECTOR YA KANUMBA KITAANI
TEARS ON VALENTINE DAY NI LEVO YA HOLLYWOOD
Wakati filamu ya The Director ambayo imefanywa kijanja na Ijumaa Sexiest Bachelor 2007, Steven Kanumba, na wakali wengine kutoka TZ na Nigeria ikiwa inafanya vizuri kitaani, kuhusu muvi ya Tears on Valentine Day mambo yako levo kimataifa kama Hollywood.

Abby Cool & MC George over the weekend, imefanya tathmini kitaani na kushuhudia jinsi wajanja wanavyoigombania The Director ambayo ni moja kati ya muvi za kiwango cha juu iliyowahi kuzalishwa Bongo, pia ikazama kambini na kuwaona wasanii wanaofanya mazoezi kwa ajilia ya Tears on Valentine Day.

Tulichokinyaka ni kwamba Tears on Valentine Day ni kiwango cha juu sana, wasanii walivyo siriaz katika mazoezi na uwezo wao, hadhi ya kambi kwenye Hoteli ya The Atriums, Sinza Afrikasana, Dar pamoja na mambo mengine, ni vitu ambavyo vinaifanya filamu hiyo iwe inaandaliwa kisasa zaidi kama vile Hollywood, USA.

***************************************************

TONI BRAXTON AMESHAJIKUNJA NA KASUKU WANNE TU!
Ni mwanamama ambaye amekwenda eji lakini katika muonekano bado anayumbisha hisia za new generation kutokana na mvuto alionao. Ni Toni Braxton ambaye leo ndiye anayeangazwa na Ebwana Dah!

Amekwishajikunja kimahaba na wanaume wangapi? Ni katika kipindi gani? Amedumu nao vipi? Cheki majibu hapa chini!

Kwa mujibu wa tovuti inayofuatilia ishuz za mastaa hususan uhusiano wa kimapenzi, inawekwa wazi kwamba Toni aliwahi kubiliguana na jamaa anayekwenda kwa jina la Curtis Martin katika kipindi ambacho hakijawekwa wazi.

Inabainishwa pia kuwa baadaye mwanamama huyo alijiweka kwa Frankie Beverly, pia haiwekwi wazi ni wakati gani na kati ya mwaka 1994-95, alifanya sanaa ya utu uzima na Shemar Moore.

Tangu mwaka 2001, amejituliza kwa Prodyuza Keri Lewis ambaye ndiye mumewe halali wa ndoa na inaonekana hana mpango na kasuku wa pembeni. Hii inaleta mshangao, kwani kwa sifa za Toni anavyochukuliwa kama mwanamke kicheche, wengi walidhani angekuwa amejikunja na wanaume wengi zaidi ya hapo.

Jina lake kamili ni Toni Michelle Braxton, umri wake ni miaka 42, alizaliwa Oktoba 7, 1966, Severn, MD, Marekani. Ana urefu wa futi 5.2, alibukua Chuo Kikuu cha Bowie State, Marekani
*********************************************


MADHILA 2: BADO SIKU 14 TU!
Muvi ya ukweli ambayo inatajwa kusheheni characters wenye akili, amazing pictures & sound pamoja na ujumbe mzito unaoigusa moja kwa moja jamii ya Kitanzania, Madhila Part II ipo tayari na baada ya siku 14 itapakuliwa kitaani.

Ofisho ripoti kutoka kampuni mkombozi wa vipaji nchini, Tollywood Movies ambayo ndiyo yenye authority ya kusambaza filamu hiyo Bongo, inaweka wazi kwamba kila kitu kinakwenda sawasawa, kwahiyo bado siku 14 ili utamu uingie sokoni.

Ndani ya dude hilo utaona jinsi Salim Mbwana a.k.a Salu ambaye anabeba uhalisia wa watu wenye ulemavu, anavyofanyiwa kila aina ya hujuma, wafanyakazi wenzake wanamtenda umafia lakini mwisho wa siku Mungu alifanya yeye kuwa mshindi. Alishindashindaje? Hii si ya kukosa!

Ndani ya Madhila part II, utakutana na mtaalamu wa kucheza na kamera, Riyama Ally, staa wa tangazo la Haki Elimu, Nuru Njaidi (Huba) na wengineo kibao.

COMPILED BY MC GEORGE

No comments: