Friday, October 23, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!


MB Dog

Mb Dog: Nafanya mpango wa kuishi na mzazi mwenzangu. Hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Baada ya kuondokewa na mwanawe mpendwa Suu, miezi kadhaa iliyopita na kufanikiwa kumaliza arobaini salama, mwana Bongo Flava Mohamed Mbwana a.k.a MB Dog amesema na ShowBiz kwamba kitakachofuata ni kumchukua jumla msichana (aliyemkumbatia mtoto pichani) aliyezaa naye mtoto huyo na kupiga naye maisha kama mke na mume.

MB alisema kwamba kabla ya zoezi hilo anafanya mishemishe za kukamilisha video za nyimbo mpya mbili kisha kumsogeza ndani maiwaifu wake huyo mtarajiwa kwa ndoa halali ambayo itawapa shavu baadhi ya mastaa wa Kibongo.

“Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, hivi sasa nipo kwenye mishemishe za kugonga video zetu mbili, moja ya kwangu nimewashirikisha Yakuza Mobb, nyingine ya kwao wamenipa shavu. Ngoma hizo ambazo bado hatujazipa majina tulizifanya Nairobi, Kenya. Baada ya hapo nitamsogeza waifu ndani tuendeleze harakati za kupambana na maisha,” alisema Dog ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake, Saga Plasher.
**********
One Love T.A kesho
Tanga ndiyo kituo kinachofuata baada ya Kanda ya Ziwa kulipuka na ‘One Love’ yaani Fiesta 2009, kesho Jumamosi shughuli hiyo itadondoka ndani ya Uwanja wa Mkwakwani kuanzia saa 4 asubuhi hadi 12 jioni ambapo wasanii kama Fid Q, Prof. Jay, Marlaw, Chegge na wengine kibao watasimama stejini.

Godfrey Kusaga ambaye ndiye mratibu wa tukio hilo alisema na ShowBiz kwamba, wakali wengine watakaopendezesha shoo hiyo ni pamoja na Chegge Chigunda kutoka Kiumeni, Juma Nature na wengine. “Pia tutatafuta vipaji vya utangazaji kwa ajili ya kumpata ‘prezenta’ wa Clouds TV,”.


compiled by mc george

1 comment:

Anonymous said...

uamuzi ulio amua wa kuishi na mzazi mwenzio ni mzuri,ni mfano mzuri kwa vijana wengine mapenzi ya mtoto ni baba na mama pole kwa kufiwa na mtoto wako. mie ni mshabiki wako toka uk.