Monday, October 26, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!



Zahir Zorro: "Nikipiga mzigo na Banana najiona ‘bwa mdogo"
Galacha wa muziki wa dansi nchini, Zahir Ally Zorro (pichani juu) amesema kuwa anapenda kufanyakazi na vijana wanaofanya muziki wa kizazi kipya kwa sababu wanampa challenge kimuziki na mazoezi. Zorro ambaye ni baba mzazi wa wanamuziki, Banana na Maunda, alisema kupitia kipindi cha Planet Bongo wiki iliyopita kwamba anapofanyakazi na vijana hujiona ana umri mdogo.

“Japokuwa nina zaidi ya miaka 50, huwa najihisi kama nina miaka 20, ninapokuwa jukwaani na Banana kwenye bendi yake (B-Band), pia nakuwa kama nafanya mazoezi, kwasababu wao vijana wakiimba kwa kasi mimi hufanya hivyo ili kwenda nao sambamba,” alisema Zorro.

Kwa sasa, Zorro anafanyakazi na Kampuni ya Zizzou Entertainment na siku chache zijazo anatarajia kuachia ngoma inayokwenda kwa jina la Barua Pepe, huku akiwa kwenye maandalizi ya kuifufua bendi yake ya Mass Media.
*************************

Soulja Boy: Alivyojichanganya kitandani na Lil Mama
Ni safu yenye kionjo cha aina yake, kupitia hapa unakuwa unajua ni staa gani amepumzika na nani. Ebwana Dah! Leo tunaye Soulja Boy, rapa ‘bwa mdogo’ lakini mwenye kiwango cha juu, hapa inawekwa orodha ya wanyange ambao kwa nyakati tofauti, ameweza kupanda nao kitandani.

Kwa mujibu wa very busy website katika kuandika issuez za uhusiano wa mastaa, mwana Hip Hop wa kike, Lil Mama ndiye mrembo wa kwanza kutajwa kudondoka on bed na Soulja Boy. Inaelezwa kuwa Soulja alianza kucheki na Lil Mama mwaka 2007 na kudumu kwa mwaka mmoja tu, kwani ilipofika mwaka 2008 kila mmoja aliangalia ustaarabu wake.

Hivi sasa, Soulja yupo na Meagan Good na penzi lao limeanza kuchukua nafasi mwaka huu. Jina lake kamili ni DeAndre Cortez Way, majina yake mengine ni Soulja Boy Tell `Em, ana umri wa miaka 19, alizaliwa Julai 28, 1990, Chicago, Illinois, Marekani.
*************************************

BBA Revolution: Kelvin ang’ang’ania penzi la Eliza
The most beuatifu girl kwenye mjengo wa Big Brother Revolution, Queen Elizabeth Gupta (pichani juu) bado yupo majaribuni kimapenzi na sasa Kelvin ameongeza kasi ya kumng’ang’ania kama luba.

Wiki iliyopita Kelvin baada ya kushauriwa na baadhi ya washiriki Big Brother Revolution, aliweka dhamira ya kumtega Queen Eliza mpaka aanze kumfikiria kimapenzi.

Hata hivyo, Emma alimshauri Kelvin kuwa si vema kumtega Eliza, kwani penzi lao halitodumu kwa sababu watakuwa mbalimbali, ushauri ambao aliukataa na kusema kwamba yeye hayupo ‘komitedi’ kwahiyo hashindwi kufunga safari hadi Tanzania, kufuata penzi la Eliza.
*****************************

Penzi la Emma, Jerremy lapamba moto
Penzi la washiriki wa shindano la Big Brother Revolution, Mkenya Jerremy na Emma wa Angola limezidi kupamba moto na hivi sasa wakiwa mjengoni, hawaachi kupigiana ‘signo’ mbalimbali kuonesha kwamba kila mmoja amekolea kwa mwenzake.

Hivi karibuni washiriki hao walionekana wakicheza muziki wenye mahadhi ya Salsa, huku taswira ya wazi kwa yeyote aliyewaona ni kwamba walikuwa wakitamaniana na kila mmoja alikuwa huru kushikwa popote na mwenzake. Emma alionekana kuvutiwa na Jerremy, hivyo akamuachia kijana huyo wa Kenya kumshika popote alipotaka.
************************

Ijumaa Sexiest Barchelor: Top 5
Shindano nambari wani la kumtafuta kijana mwenye mvuto wa ukweli kunako eneo la mahaba, linaloratibiwa na gazeti la Ijumaa, Ijumaa Sexiest Bachelor lipo kwenye nafasi nzuri kuelekea kumtaja mshindi wa mwaka 1999.

Hivi sasa, Ijumaa Sexiest Bachelor limebakiwa na vijana watano ambao wanakidhi vigezo vya kuingia fainali kabla ya kumpata mshindi, baadaye mwaka huu. Mratibu wa shindano hilo, George Alphonce ‘MC’ amewataka Watanzania kuendelea kuwaunga mkono mastaa wanaowavutia na kuwapigia kura ili kudumisha ushindani. MC George alisema:

“Hili ni shindano ambalo mshindi wake huwa anapatikana bila longolongo kwa sababu anayebeba taji ni yule anayepigiwa kura nyingi.” Mratibu huyo alikumbusha kuwa shindano hilo lilifanyika mwaka juzi na mshindi alikuwa ni Steven Kanumba, wakati Juma Kaseja alikuwa wa pili, wakati Aboubakar Shaban Katwila ‘Q Chillah’ aliondoka namba tatu.

Kujua wasifu wa walioingia Top 5, MC amewataka Watanzania kutolikosa gazeti la Ijumaa, Ijumaa hii.
************************
Hussei Machozi arudi na Johmakini
Baada ya kusumbua na traki inayopendwa kitaani, “Kwa ajili yako”, mkali mwenye vocal laini, anayeimba bila kutumia nguvu, Hussein Machozi yupo hewani tena, safari hii yupo wima na Balozi wa A-Town, Johmakini.

Hussein amemshirikisha Johmakini kwenye wimbo Utaipenda ambao umefanyika kupitia studio za Tetemesha & AB Recordz kabla ya kufanya video Visual Lab kwa Adam. Kwa mujibu wa prodyuza wa Hussein, Sandu George Mpanda ‘Kid Boy’, video ya Utaipenda imerokodiwa Dar, Septemba 24, 25 na 27 na ilianza kukatiza kitaani Jumatatu ya Oktoba 5, 2009. Kid Boy a.k.a Rude Boy alisema: “Huo ni wimbo wa pili kutoka kwenye albamu ya Hussein ambayo inaitwa Kwa ajili yako.”
************************
compiled by mc george

No comments: