Friday, November 20, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

IJUMAA SEXIEST BACHELOR top 04
Kupitia mpambano huu wa kumtafuta staa wa kiume mwenye mvuto wa kimahaba, Ijumaa Sexiest Bachelor wiki iliyopita tuliwataarifu kuwa leo tutashuka na Top 3, lakini kutokana na washiriki wawili kufungana kwa kupata idadi sawa ya kura huku Jerry Tegete akiambulia kura chache zaidi, imebidi wanne waingie kwenye Top 4 ambapo baadaye itatafutwa tatu bora kwa ajili ya kumpata mshindi mmoja.

Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye Top 4 ni Steven Kanumba, Hemed, Yusuf Mlela na Marlaw. Ili kumpigia kura mmoja ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi andika namba yake kisha tuma kwenda namba 15551. Kumbuka kwamba kura yako ndiyo kila kitu katika shindano hili ambalo limedhaminiwa na maduka ya Zizzou Fashion.
******

KANUMBA
Mimi kama bingwa mtetezi kwanza nawapongeza waandaaji wa shindano hili ambao wamekuwa wakijitahidi kubuni vitu mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitunufaisha sisi wasanii na zikiwemo zawadi kwa mshindi kama niliyopata mimi.

Pili nawashukuru sana wote wanaoendelea kunipigia kura mpaka kufikia hatua hii, naamini wataniwezesha kuchukua ushindi kwa mara nyingine tena.
*****

YUSUF MLELA
Shindano ni zuri, binafsi nimevutiwa nalo sana kwakuwa linatupa sapoti ya kutosha na kutufanya tuendelee kufahamika na watu wengi zaidi. Lakini shukrani za pekee ziwaendee mashabiki wote wanaoendelea kuwepo kwenye mpambano huu. Naamini nitaibuka na ushindi mkubwa kwakuwa sijaona mapungufu yoyote kwenye shindano hili.
*******

MARLWA
Nimefurahi sana kuingia kwenye hatua hii, nawashukuru mashabiki wangu walionipigia kura bila kuwasahau waandaaji wa shindano hili ambao wanatufanya sisi wasanii tuendelee kuwa juu zaidi.
Mpaka nimeingia kwenye hatua hii ni kipimo tosha kuwa mashabiki wangu wananipa sapoti ya ukweli, hiyo ni dalili ya kuibuka na ushindi.
****

HEMED
Wote waliofikia hatua hii wana vigezo ndiyo sababu iliyowafanya mashabiki wawapigie kura na kuwafikisha hapa. Nawashukuru sana wadau, wadhamini na waandaaji wa mpambano huu, bila kuwasahau mashabiki wangu nawaomba wazidi kunipa sapoti ili niibuke na ushindi, mwisho wa siku iwe ni jambo la kujivunia. Ni hayo tu.
***************************************



Mlinzi wa Jay -Z amfanyia umafia paparazi
Mlinzi mmoja wa mwana Hip Hop Jay- Z au Jigga ambaye jina lake halikudondoshwa mtandaoni mwanzoni mwa wiki hii alimfanyia ‘umafia’ paparazzi aliyekuwa akitaka kumpiga picha msanii huyo kwa kumsukuma na kumpiga chini kitendo kilichomsababishia maumivu ya nguvu mgongoni mwake.

Ishu hiyo ilitokea pande za Hollywood majira ya mchana pale Jigga alipokuwa anasepa kutoka katika baa moja maarufu, ‘Capitol City Sports iliyopo kunako jiji hilo ambayo hupenda kutembelewa na mastaa wengi.

Baada ya mchizi kutoka nje ya baa hiyo, paparazzi huyo aliyefahamika kwa jila la Rick anayepiga mzigo kunako kampuni ya ‘X17 photo Agency’ alitamani kupata picha kadhaa za Jay-Z lakini wakati akijiandaa kufanya hivyo ghafla alivamiwa na baunsa wa staa huyo ambaye alimsukuma na kumdondosha chini (kama anavyoonekana katika picha juu).


***************************************

Busta Kushuka Bongo leo, Fiesta kesho
Ile kitu iliyopewa jina la ‘One Love’ a.k.a Fiesta 2009 sasa imewadia, macho na masikio ya mashabiki wengi yanatarajiwa kuelekezwa kwa mwana Hip Hop Busta Rhymes kutoka Marekani ambaye atadondoka Bongo leo majira ya saa tisa mchana kwa ajili ya shughuli hiyo kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wadau wa burudani.

Akipiga stori na ShowBiz mmoja wa waratibu wa One Love, Godfrey Kusaga alisema kwamba, Busta atadondoka na timu ya watu kadhaa ambao watampa sapoti ya kutosha katika kila atakachokifanya kwenye tamasha hilo na kwamba, kila kitu kinakwenda sawa wakiwemo wasanii kibao wa muziki wa Bongo Flava ambao walikuwa kambini wakijifua kwa ajili ya tukio hilo.
***************************************

Jittaman aibuka!
Kutoka pande za Rock City mchizi aliyenusurika kunako ajali mbaya ya pikipiki iliyotokea huko miezi kadhaa, Liso Katama Ibrahimu a.k.a Jittaman au Nzagamba katikati ya wiki hii aliibukia ofisini kwetu, Sinza Bamaga, Dar es Salaam na kupiga stori mbili tatu na ShowBiz.

Mchizi alisema kwamba, kwanza kabisa amekuja kuwatoa wasiwasi mashabiki wake wengi kufuatia uvumi ulionea kwamba yeye alikufa katika ajali hiyo, kitu ambacho siyo kweli na ishu ni nyingine ni kwamba, amedondoka Dar kwa ajili ya kuendeleza harakati zake katika game ya muziki wa kizazi kipya.

“Kinachofuata hivi sasa ni kazi kwa kwenda mbele, kila ngoma nitakayoachia naamini itakuwa juu kwakuwa nimerudi na idea mpya kibao, ukizingatia kwamba kupitia ajali hiyo nimejifunza mambo mengi. Namshukuru Mungu nimepona kwani hakuna aliyetegea mimi kuwa hivi leo,” alisema Nzagamba.
***************************************


Septemba 11 Yafanya kweli mtaani
Sisi kama ShowBiz tumewahi kushuhudia muvi kibao za Kibongo nzuri lakini kwa upande wa Septemba 11 ambayo imeshuka kitaani hivi karibuni inaweza ikawa zaidi kutokana na kazi iliyogongwa na mastaa wengi waliopata nafasi ya kushiriki kunako mzigo huo.

Unajua nini kinachoendelea kuipa ushindi muvi hiyo? Ndani kuna vichwa ambavyo hujawahi kuviona kwenye filamu yoyote ya Kibongo, umeshawahi kumuona kocha mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo akiigiza kama bonge la daktari, au yule golikipa mzungu wa Yanga? Ndani ya muvi hiyo wanasoka hao wamecheza kama mastaa wa Hollywood, hebu icheki kisha utatuambia.

Bado hatujamaliza, ndani ya Septemba 11 kuna mastaa wengine wa soka kama Juma K. Juma na Mussa Hassan Mgosi. Ukija kwa upande mwingine utakutana na sura za watu maarufu kama Ben Kinyaiya, Jackline Wolper, Frola Mvungi na wengine kibao. Kwa kifupi ni muvi ambayo inasumbua ile mbaya mtaani.

compiled by mc george

No comments: