Sexiest Bachelor top 4
Homa inapanda, mpambano ni mkali kuelekea kumpata staa wa kiume mwenye mvuto wa kimahaba, Ijumaa Sexiest Barchelor. Mpango mzima upo kwenye hatua ya Top Four, hiyo ikiwa ni baada ya wapiga kura kumuonesha mlango wa kutoka, mwanasoka, Jerry Tegete.
Mzigo bado unawahusu Steven Kanumba, Hemed Suleiman, Yusuf Mlela na Laurence Malima ‘Marlaw’, hivyo kama mmojawapo unaona anakuvutia, basi mpigie kura kwa kuandika SMS, ukiambatanisha namba yake ya ushiriki kisha unaituma kwenda namba 15551.
Kumbuka kwamba kura yako ndiyo kila kitu katika shindano hili ambalo limedhaminiwa na maduka ya Zizzou Fashion.
Wiki ijayo, mmoja kati ya mastaa hao wanne, atatoka na kubakiza watatu ambao kati yao, atakuwepo The Ijumaa Sexiest Bachelor 2009-2010.
Ni wakati wako kupiga kura nyingi kadiri unavyoweza, kwani mpaka sasa, sura ya shindano inaelekea kumbeba mshiriki mmoja, kwani mpaka sasa amekwishajikusanyia kura nyingi mno kuliko wenzake.
Kutoka pande za Marekani kwa Obama, kuna ‘kesi’ mpya imedondoka kunako mtandao mmoja unaodili na ishu za mastaa wa kiwanja ikimhusu mkali wa muziki wa R&B, Fantasia Barrino ambaye anadaiwa kugonga ‘lavu’ na mume wa mtu, ShowBiz imeidaka.
Mtandao huo uliweka wazi kuwa kutokana na kukolea kimapenzi kwa mwanaume huyo Fantasia ambaye aliingia kunako ustaa wa muziki kupitia shindano la Pop Idols ameamua kuchora tattoo ya jina la mume wa mtu huyo mwenye jina la Antwaun Cook.
Jarida la Honey la huko, lilipomsomea mashitaka yake alisema kuwa hata yeye amekuwa akizisikia habari hizo kwa watu tu. “Namfahamu mwanaume huyo anayetokea T-Mobile, ni mzuri na mwenye mvuto lakini nafikiria kutafuta wa kwangu, sina mpango na na mume wa mtu. Kwa sasa nafikiria zaidi kazi yangu, sihitaji mpenzi hata hivyo ananipotezea muda wa kazi,” alisema Fantasia.
Baada ya kukana mashitaka hayo, Fantasia alikuwa hana la kusema tena pale picha zake zenye tatoo ya jina la mwanaume huyo zilipochukua nafasi kunako mtandao, huku Cook akikiri mbele ya waandishi kuwa ni kweli alikuwa na uhusiano na mwanamuziki huyo.
Daz nundaz Hili ndilo kundi la kwanza, lilipigwa ‘laana’?
Ishu mpya ambayo imedondoka ndani ya ShowBiz inachana kwamba kumbe kundi la Daz Nundaz ambalo hivi karibuni lilikutanishwa kunako tamasha la Fiesta ‘One Love’ lilianzishwa na vichwa vitatu na baada ya mafanikio dogo mmoja akapigwa chini, wakachukuliwa washikaji wengine watatu na kulisongesha kabla ya kusambaratika.
Kama bado haujafahamu vizuri dogo aliyeachwa ni Scout Jenta na washikaji waliomtosa ni Ferouz na Daz Baba ambao waliwachukua Sajo, La Rumba na Critic na kusima misha ngoma kama Maji ya Shingo, Kamanda, Barua na nyingine kabla hawajaanza kutoka mmoja mmoja kisha kupotea katika ramani ya muziki.
Akipiga stori na Showbiz, Scout Jenta ambaye hivi juzi ameachia video ya ngoma yake mpya, ‘Sera ya Mapenzi’ alisema kwamba yeye, Ferouz na Daz Baba (kama wanavyoonekana pichani) ndiyo waasisi wa Kundi la Daz Nundaz, lakini baadaye washikaji walimtosa. “Waliponiacha mimi na washikaji zangu wengi tulianzisha kundi la Scout Jenta ambalo lilidumu kwa muda kabla ya kusambaratika,” alisema Scout.
Mchizi aliweka wazi kwamba inawezekana kinyongo alichokuwa nacho moyoni baada ya Daz kumtosa ndicho kilicholifanya kundi hilo kupotea kwa kuwa mchango wake ulikuwa mkubwa, lakini pamoja na yote hayo hana bifu na kina Ferouz. Swali linakuja kwako msomaji, Je, inawezekana ‘laana’ ya Scout ilichangia kupotea kwa kundi hilo? tuma SMS 0715 110173.
R.O.M.A Aingiwa ana hofu
Mchizi anayesumbua kunako anga ya muziki wa kizazi kipya na ngoma zake mbili, Tanzania na Mr. President, Ibrahimu Mussa a.k.a R.O.M.A kutoka pande za TA a.k.a Tanga alisema na ShowBiz hivi karibuni kwamba kupitia meseji zilizomtoa za kuwachana baadhi ya viongozi wasiokuwa waadilifu kwenye nyimbo zake, ameanza kuingiwa na hofu ambayo itamfanya asigonge video.
R.O.M.A ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua Computer Science alisema kwamba pamoja na kufanya kazi hizo ambazo zimetokea kuwavutia Wabongo wengi, hatogonga video ya wimbo wa Mr. President kwa kuhofia kutochezwa kupitia vituo kadhaa vya televisheni.
“Nimeingiwa na wasiwasi huo kwa sababu video ya kwanza ya wimbo wa Tanzania kuna baadhi ya vituo vya televisheni viliogopa kuucheza, sikujua sababu hasa ni nini, inawezekana kwa sababu nimewachana mafisadi.
Ndiyo maana nikajiuliza kama video hiyo waliogopa kucheza hii ya Mr. President siyo ndiyo hawatotaka hata kuiona kwakuwa nimeongea uwazi zaidi nikiitetea jamii ya Watanzania ambayo asilimia kubwa ni masikini?” alisema mchizi ambaye pia ana mpango wa kubadilisha topiki katika ngoma zake zitakazofuata.
compiled by mc george
Homa inapanda, mpambano ni mkali kuelekea kumpata staa wa kiume mwenye mvuto wa kimahaba, Ijumaa Sexiest Barchelor. Mpango mzima upo kwenye hatua ya Top Four, hiyo ikiwa ni baada ya wapiga kura kumuonesha mlango wa kutoka, mwanasoka, Jerry Tegete.
Mzigo bado unawahusu Steven Kanumba, Hemed Suleiman, Yusuf Mlela na Laurence Malima ‘Marlaw’, hivyo kama mmojawapo unaona anakuvutia, basi mpigie kura kwa kuandika SMS, ukiambatanisha namba yake ya ushiriki kisha unaituma kwenda namba 15551.
Kumbuka kwamba kura yako ndiyo kila kitu katika shindano hili ambalo limedhaminiwa na maduka ya Zizzou Fashion.
Wiki ijayo, mmoja kati ya mastaa hao wanne, atatoka na kubakiza watatu ambao kati yao, atakuwepo The Ijumaa Sexiest Bachelor 2009-2010.
Ni wakati wako kupiga kura nyingi kadiri unavyoweza, kwani mpaka sasa, sura ya shindano inaelekea kumbeba mshiriki mmoja, kwani mpaka sasa amekwishajikusanyia kura nyingi mno kuliko wenzake.
************************************************
Fantasia na skendo ya mume wa mtu!Kutoka pande za Marekani kwa Obama, kuna ‘kesi’ mpya imedondoka kunako mtandao mmoja unaodili na ishu za mastaa wa kiwanja ikimhusu mkali wa muziki wa R&B, Fantasia Barrino ambaye anadaiwa kugonga ‘lavu’ na mume wa mtu, ShowBiz imeidaka.
Mtandao huo uliweka wazi kuwa kutokana na kukolea kimapenzi kwa mwanaume huyo Fantasia ambaye aliingia kunako ustaa wa muziki kupitia shindano la Pop Idols ameamua kuchora tattoo ya jina la mume wa mtu huyo mwenye jina la Antwaun Cook.
Jarida la Honey la huko, lilipomsomea mashitaka yake alisema kuwa hata yeye amekuwa akizisikia habari hizo kwa watu tu. “Namfahamu mwanaume huyo anayetokea T-Mobile, ni mzuri na mwenye mvuto lakini nafikiria kutafuta wa kwangu, sina mpango na na mume wa mtu. Kwa sasa nafikiria zaidi kazi yangu, sihitaji mpenzi hata hivyo ananipotezea muda wa kazi,” alisema Fantasia.
Baada ya kukana mashitaka hayo, Fantasia alikuwa hana la kusema tena pale picha zake zenye tatoo ya jina la mwanaume huyo zilipochukua nafasi kunako mtandao, huku Cook akikiri mbele ya waandishi kuwa ni kweli alikuwa na uhusiano na mwanamuziki huyo.
*******************************************
Daz nundaz Hili ndilo kundi la kwanza, lilipigwa ‘laana’?
Ishu mpya ambayo imedondoka ndani ya ShowBiz inachana kwamba kumbe kundi la Daz Nundaz ambalo hivi karibuni lilikutanishwa kunako tamasha la Fiesta ‘One Love’ lilianzishwa na vichwa vitatu na baada ya mafanikio dogo mmoja akapigwa chini, wakachukuliwa washikaji wengine watatu na kulisongesha kabla ya kusambaratika.
Kama bado haujafahamu vizuri dogo aliyeachwa ni Scout Jenta na washikaji waliomtosa ni Ferouz na Daz Baba ambao waliwachukua Sajo, La Rumba na Critic na kusima misha ngoma kama Maji ya Shingo, Kamanda, Barua na nyingine kabla hawajaanza kutoka mmoja mmoja kisha kupotea katika ramani ya muziki.
Akipiga stori na Showbiz, Scout Jenta ambaye hivi juzi ameachia video ya ngoma yake mpya, ‘Sera ya Mapenzi’ alisema kwamba yeye, Ferouz na Daz Baba (kama wanavyoonekana pichani) ndiyo waasisi wa Kundi la Daz Nundaz, lakini baadaye washikaji walimtosa. “Waliponiacha mimi na washikaji zangu wengi tulianzisha kundi la Scout Jenta ambalo lilidumu kwa muda kabla ya kusambaratika,” alisema Scout.
Mchizi aliweka wazi kwamba inawezekana kinyongo alichokuwa nacho moyoni baada ya Daz kumtosa ndicho kilicholifanya kundi hilo kupotea kwa kuwa mchango wake ulikuwa mkubwa, lakini pamoja na yote hayo hana bifu na kina Ferouz. Swali linakuja kwako msomaji, Je, inawezekana ‘laana’ ya Scout ilichangia kupotea kwa kundi hilo? tuma SMS 0715 110173.
*****************************************
R.O.M.A Aingiwa ana hofu
Mchizi anayesumbua kunako anga ya muziki wa kizazi kipya na ngoma zake mbili, Tanzania na Mr. President, Ibrahimu Mussa a.k.a R.O.M.A kutoka pande za TA a.k.a Tanga alisema na ShowBiz hivi karibuni kwamba kupitia meseji zilizomtoa za kuwachana baadhi ya viongozi wasiokuwa waadilifu kwenye nyimbo zake, ameanza kuingiwa na hofu ambayo itamfanya asigonge video.
R.O.M.A ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua Computer Science alisema kwamba pamoja na kufanya kazi hizo ambazo zimetokea kuwavutia Wabongo wengi, hatogonga video ya wimbo wa Mr. President kwa kuhofia kutochezwa kupitia vituo kadhaa vya televisheni.
“Nimeingiwa na wasiwasi huo kwa sababu video ya kwanza ya wimbo wa Tanzania kuna baadhi ya vituo vya televisheni viliogopa kuucheza, sikujua sababu hasa ni nini, inawezekana kwa sababu nimewachana mafisadi.
Ndiyo maana nikajiuliza kama video hiyo waliogopa kucheza hii ya Mr. President siyo ndiyo hawatotaka hata kuiona kwakuwa nimeongea uwazi zaidi nikiitetea jamii ya Watanzania ambayo asilimia kubwa ni masikini?” alisema mchizi ambaye pia ana mpango wa kubadilisha topiki katika ngoma zake zitakazofuata.
compiled by mc george
No comments:
Post a Comment