Monday, November 9, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Artists Bongo hawana elimu ya mikataba
Kila siku artists wanalalamika kuwa wanadhulumiwa, mara wanamtaja mdosi, wakati mwingine meneja na hata prodyuza. Abby Cool & MC George over the weekend inaweza kutoa comments kuhusu hilo.

Tulifuatilia kwa karibu sakata la Dullayo na prodyuza wake Marko Chali kuwa wamedhulumiana. Dullayo akilalamika kutiwa ndani mzigo mzima ambao waliusaini kwa mdosi, shilingi 1,000,000 keshi kama utangulizi wa nakala za albamu ambazo waligonga.

Dullayo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuwa alikwenda na Marko Chali na kusaini kopi za albamu yake, lakini baada ya kukabidhiwa M 1, prodyuza huyo alimtosa na hakumpa hata kumi.

Baada ya dogo kuharibu, Ijumaa iliyopita, Marko Chali akiwa na Mkurugenzi wa MJ Production, Joachim Kimaryo ‘Master Jay’, walitinga studio za Clouds FM na kuweka ukweli ili watu wajue.

Kilichoelezwa na Marko pamoja na MJ ni kuwa Dullayo aliingia mkataba na Marko Chali kwa ajili ya kurekodi albamu, kwahiyo M 1 iliyotolewa na mdosi, imetumika kufidia gharama ya uzalishaji wa nyimbo.

Ilielezwa kuwa Dullayo alikuwa anadaiwa shilingi 3,500,000, kwahiyo baada ya mdosi kukata milioni moja, bado anadaiwa shilingi 2,500,000. Eti, hili msanii huyo analijua na lipo kwenye mkataba.

MJ na Marko waliweka wazi kuwa msanii akiwa kwenye label, anagharimiwa kila kitu, lakini wakati wa mauzo, hukatwa kwanza fedha zilizotumika kuandaa kazi yake yote, halafu faida ndiyo hugawanywa kati ya msanii na label.

Kinachoonekana kutoka kwenye mazungumzo hayo ni kuwa Dullayo alipoona M imetolewa, alijua ni yake moja kwa moja, wakati kuna makato ya gharama za kumuandalia albamu yake ili iende soko. Hili ni tatizo na wasanii wengi wapo kwenye msafara huu.

Wasanii wengi hawajui mikataba, wanapaswa kuelimishwa kuhusu hili. Maelezo ya mkataba yanasema utaanza kuvuna mafao baada ya gharama zilizotumika kukuandaa wewe msanii kurudi, lakini saini ya kwanza tu unataka mgao, halafu unatangaza umeibiwa. Hapa tunataniana.

Hapa juzi kati, Tundaman alisaini mkataba na meneja wa Berry 9 wa kufanyakazi pamoja, lakini baadaye dogo akakana, wakati saini yake ipo. Hii ni wazi kuwa artists wetu wengi hawajui mikataba, inabidi waelimishwe.
**************************

Cassie amelegeza kwa wawili tu, P. Diddy ndani
Ni ishu ya staa gani katoka na nani, mwanamuziki Cassie ndiye yupo kizimbani leo na hapa itatajwa orodha ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti, tena kwa hiari yake alilegeza na kukwea nao on bed.

Kwa mujibu wa mtandao unaodili na ‘ishuz’ za mastaa wa kiwanja, Ryan Leslie ndiye kidume namba moja anayetajwa kupumzika na mrembo huyo, inatajwa kwamba walianza kucharukiana mwaka 2006 na kuachana 2007.

Staa mwenye fedha zisizosumbua, Sean Puffy Combs ‘P. Diddy’ au Puffy Daddy kama alivyokuwa akijulikana zamani, anatajwa nambari mbili kwamba alianza kuchetuka naye mwaka 2008.

Mrembo Cassie, jina lake kamili ni Cassandra Ventura, umri wake ni miaka 23, alizaliwa Agosti 26, 1986, New London, Connectcut, Marekani. Nyota yake ni Virgo, ana urefu wa futi 5.75.
*************************


Blu:Mimi shule sasa basi
Dogo mwenye uwezo mkubwa wa kuishi kistaa, Heri Samir ‘Blu’ amesema kuwa hivi sasa akizungumzia ishu ya shule atakuwa anadanganya kwa sababu haipo kwenye programu yake.

Blu, staa wa Bongo Flava asiyefunikika, alisema kupitia kipindi cha XXL, Clouds FM kuwa ana mambo mengi yanayomkip busy lakini ishu ya elimu haipo kwenye ratiba yake.

Dogo huyo ambaye anajulikana pia kwa jina la Kabayser, alizungumza hivyo kama jibu la swali aliloulizwa na presenta wa Clouds, Fatma Hassan ‘DJ Fetty’.

Mbali na ishu ya elimu, Blu alisema kuwa sasa hivi hayupo kwenye mikakati ya albamu, isipokuwa atakachokuwa anakifanya ni kudondosha singo kali kila mara ili kuwapa raha ‘fans’ wake.

Aidha, Blu alimpa shavu Dogo Hamidu a.k.a Nyandu Tozz kuwa ndiye mtu aliyempeleka studio kwa mara ya kwanza, MJ Record ambapo alifanya singo yake ya kwanza inayoitwa Kwa Mama.
*******************************
Eliza ampa onyo Kelvin
The Most Beautiful Girl ndani mjengo wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta ‘Queen’ amemuonya ‘best friend’ wake, Kevin kuwa kama kuna msichana anayemuumiza nje ya jengo basi aache mara moja.

Eliza, alimtolea uvivu Kevin wiki iliyopita kwa kumwambia kuwa anaona vitendo vyake kwa macho, hivyo kuendelea kumsihi aache mchezo huo.

“Kama kuna msichana ambaye unamuumiza huko nje ya nyumba tafathali acha,” alisema Elizabeth.

Kabla ya kusema hayo, Elizabeth na Emma walikuwa na mazugumzo ambayo yalichukua muda mrefu kumzungumzia Kevin.

Eliza alimwambia Emma kuwa walipokutana kwa mara ya kwanza na Kevin, alimueleza kwamba ana mpenzi.
****************
Leonel amueleza Mzamo anachopendelea faragha

Mshiriki wa Msumbiji, Leonel wikiendi iliyopita alifanya ‘wonders’ baada ya kumueleza Mzamo mitindo ya kimapenzi ambayo yeye huifurahia kiawa faragha.

Katika kile kilichoonekana kuwa alikuwa akimtega mwenzake, wakiwa wamelala kitanda kimoja kwa staili ya mzungu wa nne, Leonel alimwambia Mzamo kuwa akiwa faragha hupendelea kuangalia juu.

Aidha, Leonel pia alimuonesha kwa ishara jinsi anavyoweza kukubaliana na mtindo huo akiwa faragha.

Hata hivyo, baada ya maongezi hayo, watazamaji wengi walituma maoni, wengi wa
**********************
compiled by mc george

No comments: