Wednesday, December 16, 2009

Ukweli kuhusu Saratani na lishe- 2


Ukweli kuhusu Saratani na lishe- inaendelea kutoka wiki iliyopita..

Kama vile mlo wenye nyama, ambayo pia ina kiasi fulani cha ‘anti biotics’ kwa ajili ya wanyama na homoni za ukuzaji ambazo zote zina madhara, hasa kwa mgonjwa wa saratani.

Mlo wenye asilimia 75 ya matunda, mboga za majani na nafaka halisi, husaidia kujenga mwili kuwa katika mazingira ya ‘alkaline’ ambayo ni mazuri kwa mgonjwa wa saratani. Juisi ya matunda na mboga hutengeneza ‘enzymes’ ambao husambaa mwilini kirahisi ndani ya dakika 15 tu na huenda kuimarisha na kustawisha seli nzuri za mwili.

Ili kupata ‘enzymes’ hai kwa ajili ya kujenga seli zenye uhai na afya nzuri kupambana na zile za kansa, pendelea kunywa supu ya mboga, ikiwemo supu ya maharagwe, mara 2 hadi 3 kwa siku. Epuka kunywa kahawa, chai nyeusi na chokoleti ambazo zina kiwango kikubwa cha ‘caffeine. Badala yake kunywa CHAI YA KIJANI ambayo ina virutubisho vyenye uwezo wa kupamba na seli za saratani.

Ili kujiepusha na sumu pamoja na asidi iliyomo kwenye maji, kunywa maji safi na salama (purified water) na usinywe maji yenye kemikali (distilled water).

Ili kuimarisha kinga yako ya mwili, unaweza pia kula vidonge lishe (food supplements) vya aina mbalimbali, vikiwemo vya Vitamin E ambavyo huuwa seli zinazosababisha saratani au zile zilizokwisha kufa.

Aidha, inaelezwa kuwa saratani ni ugonjwa wa kiakili, kimwili na kiroho pia. Kuwa na matumaini, furaha na uchangamfu wakati wote, husaidia sana mgonjwa wa saratani kuendelea kuishi kwa muda mrefu bila kusumbuliwa na maradhi. Jifunze kupumzika na kufurahia maisha.

Mwisho inaelezwa kuwa, Seli za saratani haziwezi kuishi katika mazingira yenye hewa ya oksijeni ya kutosha, hivyo kwa kufanya mazoezi ya viungo kila siku na kufanya mazoezi ya kuvuta pumzi mara kwa mara, husaidia upelekaji wa hewa ya oksijeni ya kutosha mwilini. Hivyo tiba ya kuvuta pumzi nayo hutumiwa sana katika kukata makali ya saratani.

Kama wewe tayari ni muathirika wa saratani, zingatia muongozo huu wa ulaji vyakula na utaona nafauu na kama hujaupata, basi ni vizuri kuzingatia suala la lishe bora kama tunavyoeleza mara kwa mara kwenye makala zetu na Mungu atakusaidia kukuepusha na saratani.


No comments: