Friday, April 9, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!


Hemed
 Mlela
>>Wakutanishwa kwenye steji moja, kambi moja!
Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, Yusuf Mlela na aliyekuwa mshindi wa pili, Hemed Suleiman ambao hawapikiki chungu kimoja wamekutanishwa kwenye steji moja na kupiga shoo ya nani zaidi, Richard Bukos anashuka nayo.

Mwanzoni mwa wiki hii ShowBiz ilidondoka pande za Club Billicanas, Dar na kuwakuta na mastaa hao wa muvi wakirekodi mpambano huo wenye jina la Selebuka ambao hurushwa hewani kupitia kituo cha televisheni cha TBC 1 kila siku ya Jumapili.

Katika mpambano huo mastaa hao walionekana kuwagawa mashabiki waliohudhuria kwa wingi siku hiyo kama wageni waalikwa huku ishu zaidi zikisema kwamba wasanii hao hukutana katika kambi moja ya mazoezi kabla ya kurekodi. Mbali na Hemed na Mlela, mastaa wengine kibao kama Chegge, Angie, Jini Kabula na wengine kibao wanawania kitita cha shilingi milioni 25 za Kibongo.
XXXXXXXXXXXXXXXX
Lady Jaydee
Lady Jaydee ametajwa kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike 2009/ 10
Compiled by mc george/for ijumaa newspaper

1 comment:

Disminder orig baby said...

Namzimia sana Mlela katika kaza zake, lakini pia anaonekana ni kijana mtaratibu sana. Hey bro don't spoil the loooooook