Tuesday, June 8, 2010

Unajua kwanini tunaugua mara kwa mara? - 2

Wiki iliyopita tulianza makala haya yenye lengo la kujua sababu za watu kuugua mara kwa mara. Tumeanza kwa kuona kuwa mwili una kanuni zake ambazo ni lazima zifuatwe na zisipofuatwa huleta maradhi. Vile vile tumeona kuwa maradhi hayaji ghafla, bali huanza kwa kutoa ishara ambazo watu wengi, ama hawazijui au huzipuuzia…….. Sasa endelea.

Unapoacha kunywa maji kiwango kinachotakiwa kwa siku, mwili wako utatoa ishara yake kupitia mkojo. Utakapoenda haja ndogo, rangi ya mkojo wako itakuwa ya njano na wenye harufu mbaya. Tabia ya kutokunywa maji ikiendelea kwa muda mrefu, siyo tu utakuwa unakojoa mkojo wa njano, bali mwekundu ukiambatana na damu.

Siyo hilo tu, dalili nyingine utakayoiona kutokana na kutokunywa maji, ni kukosa choo kwa siku kadhaa na hata unapokipata, kinakuwa kidogo na kigumu. Kwa kawaida binadamu anatakiwa kupata chooo kikubwa angalau mara moja kila siku, kama siyo mara 2 au tatu, kutegemeana na idadi na aina yam lo anaokula kwa siku.

Madhara ya kuwa na tabia ya kutokupenda kunywa maji kama inavyotakiwa, hayaishii kwenye kukojoa mkojo wa njano au damu na kukosa choo, bali huende mbele zaidi. Matatizo mengine yanayoweza kujitokeza kwenye mfumo wa haja ndogo, ni pamoja na kuziba kwa kibofu cha mkojo na kushindwa kukojoa kabisa.

Halikadhalika, madhara ya kutokunywa maji mengi hayaishii kwenye kukosa choo au kupata choo kigumu, bali hali hiyo ikiendelea husababisha madhara mengine mwilini. Uchafu unapokaa tumboni kwa muda mrefu, hugeuka na kuwa sumu ambayo husambaa katika mfumo wa damu na kudhoofisha kinga ya mwili.

Mtu akisha kuwa katika hali hiyo, anakuwa amejiweka katika hatari ya kupatwa na magonjwa nyemelezi ambayo hutokea wakati wowote. Mwili unapokuwa umejaa sumu, unakuwa sawa na yumba ambayo haijafagiwa siku nyingi ambayo huwezi kushangaa kuona mende, panya, nyenyele, n.k. Mtu mwenye mwili wa aina hii, kuumwa mara kwa mara itakuwa ni jambo la kawaida kwake.

Ulaji chakula
Kwa kawaida, binadamu tunaruhusiwa kula vyakula vyote, lakini kila chakula kina kiasi chake. Mwili una kanuni yake ambapo kuna aina ya vyakula inahitaji kwa wingi kila siku na kuna aina nyingine inahitaji kidogo sana. Eneo hili ndilo linalowashinda watu wengi na kujikuta wanakula vyakula bila mpangilio na mwisho wa siku hukatazwa kuvila kabisa baadhi ya vyakula.

Kula bila kufuata kanuni ya ulaji husababisha mwili kukosa uwezo wake wa asili wa kujilindi. Mungu ameonesha uwezo wake mkubwa katika uumbaji. Aliuumba mwili kisha akauwekea ulinzi wake wa asili dhidi ya wavamizi wa kila aina.

Ndani ya miili yetu kuna kinga za asili ambazo zinapambana na ‘wavamizi’ kila siku bila sisi wenywe kujijua. Binadamu wote hatuko salama dhidi ya maradhi kutokana na mazingira tunayoisha ya kuvuta hewa chafu, kula vyakula visivyo salama, kunywa maji yasiyo salama, hivyo tunahitaji ulinzi wa kutosha, vinginevyo kila siku tutakuwa kitandani wagonjwa.

Ili walinzi wako wa asili waweze kufanya kazi ya kukulinda vizuri, wanahitaji kuwezeshwa.

Itaendelea wiki ijayo...

3 comments:

Anonymous said...

SAMAHANI SANA KAKA HIYO FOOD PYRAMID TUNAKUOMBA WADAU WAKO IWEKE KWA UKUBWA HAPO NI NDOGO SANA HAIONEKANI

Anonymous said...

Pia your not right at the point "binadamu tunaruhusiwa kula vyakula vya aina zote"

PLease kuna kitu kinahusu EATING ACCORDING TO YOUR BOOLD TYPE" with that you can find that not all kind of food is good to every one!!!

Interested-let me know i will send a copy of the book!

Mrisho's Photography said...

Nakubaliana na wewe msomaji wangu wa June 12 kuwa at some point sikuwa sahihi kwa kusema kuwa 'binadamu tunaruhusiwa kula vyakula vya aina zote'. Kimsingi mtu anapougua maradhi yatokanayo na staili ya maisha aliyonayo kama vile presha, kisukari, vidonda vya tumbo, n.k hupewa masharti ya kula na kutokula aina ya vyakula fulani, lakini kama hana matatizo hayo huwa hana mpaka wa vyakula, linabaki suala la mtu kuwa anapenda au hapendi chakula fulani kwa matakwa yake binafsi hicho ndicho nilichoamanisha hapo...but scientifically can also be different according to someone's blood type, ningependa kukisoma nami hicho kitabu...Thx!.