Friday, July 23, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Q. Chief No Featuring kwa sasa
Ishu mpya kutoka kwa staa wa ngoma ya ‘Tutaonana wabaya’ Aboubakari Shaban Katwila a.k.a Q Chiller iliyodondoka pande za ShowBiz wiki hii inasema kwamba hivi sasa mchizi hataki kusikia habari za kushirikishwa (Featuring) katika ngoma za wasanii wengine.

Akipiga stori na safu hii chini ya meneja wake, Khadija Seif wa Dida Fashion UK, Chiller alisema kwamba hivi sasa hataki kusikia habari za kushirikishwa kwasababu yuko tait na ujio wake mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

“Hivi sasa nipo kwenye mishemishe za kwenda levo nyingine, sihitaji kushirikishwa na msanii yoyote, nimeshawasaidia sana kilichopo mbele yangu muda huu ni kuangalia jinsi ya kuupeleka muziki wangu mbali,” alisema.

Akiwa ametoka chimbo na ngoma yenye jina la Saba mara sabini inayofanya vizuri sasa, jamaa pia yuko tayari kulitaja jina la albamu yake mpya ambayo ni A sing of matureness kwakuwa tayari imeshakamilika kinachofuata ni video za ngoma kadhaa kabla ya kuwapelekea walaji. Kama una maoni kuhusu Chiller cheki na sisi kwa anuani zilizopo juu.
*******************************************

K-Sher Azinduka kwa dokta, Dodoma
Katika kuonesha kwamba yuko ‘andastending’ na ile kauli mbiu ya kupambana na gonjwa hatari la Malaria ‘Zinduka’, mwanadada Khadija Shaban a.k.a K-sher alijikuta amejisogeza kwa daktari ili kujua kama kinachomsumbua ni ugonjwa huo au la.


Ishu hiyo ilichukua nafasi pande za Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mwanadada huyo anayefanya game ya muziki kupitia kundi la Tip Top Connection alipokuwa kwenye ziara ya tamasha la Fiesta inayoendelea hivi sasa hapa nchini.

“Unajua nilikuwana Malaria tangu wiki iliyopita nikapima na kupata dawa, lakini baada ya kufika Dodoma nikawa sijisikii vizuri ikabidi nikapime tena kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa nikakutwa na Malaria 3, nikapewa dawa nyingine, hivi sasa nashukuru Mungu naendelea poa,” alisema K-sher. ShowBiz inampa pole msanii huyo na inamuombea apone haraka ili aendelee kuwakilisha kupitia game ya muziki wake. (Maoni kuhusu K-Sher cheki na sisi kwa anuani zilizopo juu kulia.)

Ule mpango wa kujipangusa kupitia tamasha kubwa la Fiesta 2010 utaendelea tena kesho ndani ya Uwanja wa Mkwakwani pande za Tanga kwa shangwe zilezile kama ilivyokuwa Dodoma na sehemu nyingine, huku wasanii kama Mwasiti, Diamond, Kassim, Fid Q, R.O.M.A, Chegge, Temba na wengine kibao wakipiga shoo. Rrraaaaaaaa!!
*****************************
click picture to read

Kanal Top azinguana na mashabiki, wamzomea!
Rapa wa Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Kanal Top Jumapili ya Julai 11, 2010, alizinguana na mashabiki ambao kwa kuona anawaletea za kuleta, wakajiuliza na kupata jibu kwamba dawa ni kumvunjia heshima, kwahiyo wakamzomea.

Kanal ambaye alikuwa chimbo kwa muda mrefu, akijiuguza mkono baada ya kuumizwa rapa mwenzake wa Akudo, Totoo ze Bingwa, alikutwa na masahibu hayo wakati bendi hiyo ilipokuwa inagonga bonanza kama kawa kwenye Klabu ya New Msasani Beach.

Safu hii ambayo ilikuwepo ukumbini, awali Kanal alipopanda jukwaani walimpokea kama lulu kwa sababu walimmisi kwa kitambo kirefu na kusababisha jukwaa lifurike wadau.

Hata hivyo, hali hiyo Kanal hakuipenda, kwahiyo akawa anakatisha nyimbo kabla ya kuamua kushuka chini kabisa, kitendo ambacho kiliwaudhi mashabiki ambao waliona amewadharau, hivyo wakaanza kumzomea.

Kanal alipofuatwa na safu hii ili aseme lolote kuhusu kilichomsibu aligoma kutoa ushirikiano na kuhama mahali alipokuwa amekaa, na kila alipofuatwa, aliondoka.
Mzigo umeletwa na Richard Bukos
************************************************



No comments: