Wednesday, July 21, 2010

UNAJUA MAJI NI DAWA?-2

Wiki iliyopita tuliandika tabia ya maji yanavyofanya kazi mwilini tukaelezea hatua ya kwanza hadi ya pili. Sasa endelea...

TATU: Utumbo siyo sehemu pekee inayonufaika na tiba hii ya maji, bali chembechembe hai (cells) zote za mwili huwa zimepewa uhai na nguvu mpya. Maji yanaponywewa baada ya mwili kutoingiza kitu chochote kwa kipindi cha saa 8 – 10, mwili huyapokea maji hayo kwa ‘kiu’ kubwa na kuyasambaza katika seli zote za mwili.
Vijidudu nyemelezi (free radicals) na vitu vyote vyenye sumu ambavyo huganda kwenye seli, kimsingi hushinikizwa kujiondoa vyenyewe kutoka kwenye seli hizo, hivyo kuurahisishia mfumo wa kusafisha mwili kuondoa mwilini sumu na vitu visivyotakiwa kwa urahisi.

TAHADHARI
Kwa mgonjwa anayetumia tiba hii ya maji, kuna mabadiliko au usumbufu fulani anaoweza kuupata katika siku 3 au 7 za mwanzo. Anaweza kuumwa na kichwa au mwili na kuhisi kama kichwa chake ‘kinaogolea’. Vile vile anaweza kutokwa sana jasho, kusikia kichefuchefu au kama si hivyo, anaweza asijisikie vizuri tu.

Hayo yasikutie hofu, hayo SIYO MADHARA (side effects), bali hiyo ni dalili kwamba mwili umeanza kuondoa sumu zilizoganda kwenye seli zake. Kwa kuwa tiba ya maji haina madhara yoyote, unapoona dalili hiyo usiache, endelea kama kawaida, kama utashindwa basi punguza kidogo kiasi cha maji unachokunywa.

Baada ya siku kadhaa kupita, mgonjwa hurejea katika hali yake ya kawaida na hiyo huwa ni dalili kwamba mwili umeanza kutakasika. Hali ikirejea kama kawaida, mgonjwa hana budi kuendelea na kiasi kile kile cha maji kilichopendekezwa.
ZINGATIA
Ingawa tiba ya maji ni nzuri kwa wagonjwa wengi wa figo na moyo, lakini wenye matatizo MAKUBWA ya magonjwa hayo, wanashauriwa kujaribu tiba hii baada tu ya kupata mwongozo sahihi na ruhusa ya daktari.
Wiki ijayo ndiyo tutaanza kujifunza hatua nyingine ya matumizi ya maji kwa ajili ya kusafisha utumbo mpana kwa kitaalamu inaitwa Enema, KWA WANAOJALI AFYA ZAO.

Mwisho.
Kama una swali kuhusu masuala ya ulaji sahihi au kuhusiana na makala ambazo tumewahi kuzitoa katika kolamu hii, tafadhali niandikie barua pepe kwa anuani ya uwazi@hotmail.com au nitumie ujumbe mfupi wa maneno kwa namba 0713 839363 au barua kwa anuani ya: GAZETI LA UWAZI, JINSI ULIVYO S. L. P 7534 DAR ES SALAAM. Majibu ya maswali yenu yatakuwa yakichapishwa gazetini.

1 comment:

Disminder orig baby said...

Mungu akuzidishie kaka Mrisho