Alichokifanya Kidumu na prodyuza wake Kenya, Hermy B afungua kinywa!
Madai ya Wabongo kuporwa kazi zao yanaendelea kuchukua nafasi, ilizungumzwa mno ishu ya Jose Chameleon kudaka kinyemela bits za wimbo Nikusaidieje wa Prof. Jay, lakini sasa hivi kuna topic mpya ambayo character wake ni Harmy B ambaye analalamikia alichotendwa Kenya.
Habari ambazo tumezipata kwa msaada wa blogu ya DJ Choka, zinasema kuwa Hermy B, aliandika email kuelezea mchezo mzima ambao unachambuliwa hivi; Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy B ambaye alikutana naye Project Fame, Nairobi, Kenya.
Wakakutana na kufanya kazi pamoja, katika mantiki kwamba muziki ulitengenezwa na Hermy halafu Kidumu akatumbukiza sauti. Kidumu aliporudi Nairobi akakutana na prodyuza anayeitwa Rkay (mtayarishaji wa nyimbo za Wahu kama vile Sweet Love na Running Low) ili amtengenezea video. Kilichofanyika, Rkay kabla ya kutengeneza video aliamua kutengeneza upya wimbo huo lakini akatumia bits na vionjo vya Hermy bila idhini yake.
Mbaya zaidi ni kuwa Kidumu anadaiwa kutembea vituo vya Kenya kuomba wimbo uliofanywa na Hermy B usichezwe badala yake air play ifanyike kwa nakala iliyotengenezwa na Rkay. Unajua wimbo unaolalamikiwa ni upi? Unaitwa Nitafanya ambao Kidumu amemshirikisha malkia wa Afropop Afrika Mashariki, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’.
Ray C Anarudi Japo Suna tu!
Yalipozungumzwa hakujibu, badala yake akawa very busy kufanikisha malengo yake ya kimaisha, lakini sasa anathibitisha kuwa kipaji kipo na hakichakai!
Super Beautiful wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ anarudi sokoni kwa kasi. Akiwa ana-shine na ngoma ya Mama Ntilie ambayo ametupiwa featuring, Ray C, anajiwinda kurudi upya na hivi sasa kama hujui ratiba yake ni kwamba anapiga mzigo studio usiku na mchana ili kukamilisha albamu yake ambayo ameamua kuiita Japo Suna.
Ray alisema na Abby Cool & MC George over the weekend kuwa siku hizi hana muda wa kusikiliza nani anasema nini na kwanini, badala yake anafanya kuthibitisha ubora wake kupitia sauti na tungo zake. “Hakuna mtu ambaye hajui kama sisi wasanii tunaibiwa, kwahiyo inabidi tufanye kazi nzuri na jamii ituunge mkono ili tufike mbali, na ndiyo maana nipo serious,” alisema Ray C na kuwataja watayarishaji wake kuwa ni Marco Chally, Allan Mapigo, Enrico wa Sound Crafters na wengine.
Muktadha ni ule ule, kwamba ni staa gani yupo na nani kimapenzi na aliwahi kusuguana na akina nani? Headliner wa leo ni mwanamuziki Leona Lewis.
Ebwana dah! Wakati mastaa wengi wa kike walipowekwa hapa na ku-make headline, waliweka rekodi ya kutoka na wapenzi wengi, kwa Leona ni tofauti! Ni mmoja tu ambaye ameweza kujulikana na kuwekwa wazi kwamba amewahi kutoka naye.
Lou Al-chamaa ndiye anayetajwa kwamba kuanzia mwaka 2002 mpaka sasa, wamekuwa pamoja na hakuna mwanaume yeyote aliyewahi kuweka chata zaidi ya jamaa huyo.
Hata hivyo, hivi karibuni kuna uvumi ulichukua nafasi kwamba wawili hao wameachana, ingawa hakuna kati yao aliyejitokeza na kuzungumzia taarifa hizo kama zina ukweli au ni longolongo. Jina lake kamili ni Leona Lewis, umri wake ni miaka 25, urefu wake ni futi 5.7. Alizaliwa Aprili 3, 1985, Islington, London, Uingereza.
Pacho Mwamba: Wife ana wivu, simuachii kilongalonga!
Mwanamitindo na mwanamuziki anayetoa huduma yake kwenye Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Patcho Mwamba ameona siyo kosa kusema ukweli kwamba yeye na wife wake hawaaminiani hasa linapokuja suala la simu, inashushwa na Hemed Kisanda.
Patcho on straight talk to Abby Cool & MC George over the weekend, wiki iliyopita alisema kuwa mke wake ana wivu wa kupitiliza ndiyo maana huwa anashindwa kumuamini na kumuachia kilongalonga.
Aliongeza kuwa kutokana na tabia hiyo ya wivu, mara nyingi anapokaribia kurudi nyumbani, hutumia msemo wa heri nusu shari kwa kuzima simu kabisa.
“Napigiwa simu na watu wengi, wengine siwajui basi kwa hili napata tabu sana kwa mke wangu, kwani tunagombana mara kwa mara. “Wakati mwingine nalazimika kuizima kila ninapoingia nyumbani au kuificha ninapokwenda kuoga, mke wangu ana wivu mno na huwa anaikagua mara kwa mara,” alisema Patcho.
Ilianza Big Brother Africa mwaka 2003, ikaja Big Brother Afrika II (2007), ikaja Big Brother III (2008), baadaye Big Brother Revolution (2209), hata hivyo, zote zinatajwa ni tisa, 10 na itakayofunika ni ya 2010 ambayo inakwenda kwa jina la Big Brother All Stars.
Sababu ambayo inatajwa kuifanya Big Brother mwaka huu kuwa ya kipekee ni uamuzi wa kuwachukua mastaa waliong’ara kwenye fainali zilizopita na kuwapa nafasi ya kuingia tena mjengoni ili kushindana tena.
Tanzania imeshiriki mashindano hayo mara zote, na kufanya vizuri zaidi mwaka 2007, pale Ricahrd Bezuidenhout aliponyakua taji na kujibebea kitita cha Dola za Kimarekani 100 ambazo kwa ‘chenji’ ya wakati huo zilikuwa shilingi 130,000,000. Mwanga wa mafanikio kwa Tanzania kwenye mashindano hayo, ulioneshwa mapema mwaka 2003, pale Mwisho Mwampamba ‘Mr. Morogoro’ aliposhika nafafasi ya pili, nyuma ya Cheris Makubale wa Zambia.
Mwaka 2008, Tanzania iliwakilishwa na Latoya Lyakurwa ambaye aliifanya Tanzania kuwa wa kwanza kutolewa mjengoni kwa awamu hiyo, na Elizabeth Gupta ‘Queen’ alijitahidi mwaka 2009 lakini hakufika mbali, akawa amechomolewa.
Kionjo kikubwa mwaka huu, ni watazamaji kuwaona tena wale mastaa wao waliowakubali kwenye fainali mbalimbali zilizopita, hivyo kuifanya awamu hii ya 2010 kuwa tishio zaidi kuliko zilizotangulia.
Dogo anayelelewa na bendi ya nyumbani, Msondo Music, Hassan Shaaban Mhoja TX Moshi Jr, Ijumaa iliyopita alibambwa red-handed na safu hii, akidai kwa nguvu mchango wa harusi.
TX Jr ambaye ni mwana wa galacha wa muziki wa dansi, marehemu Shaaban Mhoja ‘TX Moshi William’, alibambwa akimdai mchango mwanamuziki wa Top Band, Allawi Junior. Kama hujainyaka ni kuwa dogo huyo ametangaza ndoa na mrembo ‘flani’ wa Mikocheni, Dar, anayeitwa Rehema.
TX alimkaba koo Allawi ambaye ni mshenga wake katika ndoa hiyo baada ya kukutana naye ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Dar es Salaam ambapo bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ walikuwa wakifanya makamuzi. “Namdai Allawi shilingi 200,000 ambazo aliahidi kunipa kama mchango wake kwenye harusi yangu,” alisema TX Jr alipozungumza na gazeti hili. Mzigo umeletwa na Richard Bukos.
Madai ya Wabongo kuporwa kazi zao yanaendelea kuchukua nafasi, ilizungumzwa mno ishu ya Jose Chameleon kudaka kinyemela bits za wimbo Nikusaidieje wa Prof. Jay, lakini sasa hivi kuna topic mpya ambayo character wake ni Harmy B ambaye analalamikia alichotendwa Kenya.
Habari ambazo tumezipata kwa msaada wa blogu ya DJ Choka, zinasema kuwa Hermy B, aliandika email kuelezea mchezo mzima ambao unachambuliwa hivi; Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy B ambaye alikutana naye Project Fame, Nairobi, Kenya.
Wakakutana na kufanya kazi pamoja, katika mantiki kwamba muziki ulitengenezwa na Hermy halafu Kidumu akatumbukiza sauti. Kidumu aliporudi Nairobi akakutana na prodyuza anayeitwa Rkay (mtayarishaji wa nyimbo za Wahu kama vile Sweet Love na Running Low) ili amtengenezea video. Kilichofanyika, Rkay kabla ya kutengeneza video aliamua kutengeneza upya wimbo huo lakini akatumia bits na vionjo vya Hermy bila idhini yake.
Mbaya zaidi ni kuwa Kidumu anadaiwa kutembea vituo vya Kenya kuomba wimbo uliofanywa na Hermy B usichezwe badala yake air play ifanyike kwa nakala iliyotengenezwa na Rkay. Unajua wimbo unaolalamikiwa ni upi? Unaitwa Nitafanya ambao Kidumu amemshirikisha malkia wa Afropop Afrika Mashariki, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’.
******************
Ray C Anarudi Japo Suna tu!
Yalipozungumzwa hakujibu, badala yake akawa very busy kufanikisha malengo yake ya kimaisha, lakini sasa anathibitisha kuwa kipaji kipo na hakichakai!
Super Beautiful wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ anarudi sokoni kwa kasi. Akiwa ana-shine na ngoma ya Mama Ntilie ambayo ametupiwa featuring, Ray C, anajiwinda kurudi upya na hivi sasa kama hujui ratiba yake ni kwamba anapiga mzigo studio usiku na mchana ili kukamilisha albamu yake ambayo ameamua kuiita Japo Suna.
Ray alisema na Abby Cool & MC George over the weekend kuwa siku hizi hana muda wa kusikiliza nani anasema nini na kwanini, badala yake anafanya kuthibitisha ubora wake kupitia sauti na tungo zake. “Hakuna mtu ambaye hajui kama sisi wasanii tunaibiwa, kwahiyo inabidi tufanye kazi nzuri na jamii ituunge mkono ili tufike mbali, na ndiyo maana nipo serious,” alisema Ray C na kuwataja watayarishaji wake kuwa ni Marco Chally, Allan Mapigo, Enrico wa Sound Crafters na wengine.
********************
Leona Lewis Penzi lake alitoa kwa huyu tu!Muktadha ni ule ule, kwamba ni staa gani yupo na nani kimapenzi na aliwahi kusuguana na akina nani? Headliner wa leo ni mwanamuziki Leona Lewis.
Ebwana dah! Wakati mastaa wengi wa kike walipowekwa hapa na ku-make headline, waliweka rekodi ya kutoka na wapenzi wengi, kwa Leona ni tofauti! Ni mmoja tu ambaye ameweza kujulikana na kuwekwa wazi kwamba amewahi kutoka naye.
Lou Al-chamaa ndiye anayetajwa kwamba kuanzia mwaka 2002 mpaka sasa, wamekuwa pamoja na hakuna mwanaume yeyote aliyewahi kuweka chata zaidi ya jamaa huyo.
Hata hivyo, hivi karibuni kuna uvumi ulichukua nafasi kwamba wawili hao wameachana, ingawa hakuna kati yao aliyejitokeza na kuzungumzia taarifa hizo kama zina ukweli au ni longolongo. Jina lake kamili ni Leona Lewis, umri wake ni miaka 25, urefu wake ni futi 5.7. Alizaliwa Aprili 3, 1985, Islington, London, Uingereza.
***************************
Pacho Mwamba: Wife ana wivu, simuachii kilongalonga!
Mwanamitindo na mwanamuziki anayetoa huduma yake kwenye Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Patcho Mwamba ameona siyo kosa kusema ukweli kwamba yeye na wife wake hawaaminiani hasa linapokuja suala la simu, inashushwa na Hemed Kisanda.
Patcho on straight talk to Abby Cool & MC George over the weekend, wiki iliyopita alisema kuwa mke wake ana wivu wa kupitiliza ndiyo maana huwa anashindwa kumuamini na kumuachia kilongalonga.
Aliongeza kuwa kutokana na tabia hiyo ya wivu, mara nyingi anapokaribia kurudi nyumbani, hutumia msemo wa heri nusu shari kwa kuzima simu kabisa.
“Napigiwa simu na watu wengi, wengine siwajui basi kwa hili napata tabu sana kwa mke wangu, kwani tunagombana mara kwa mara. “Wakati mwingine nalazimika kuizima kila ninapoingia nyumbani au kuificha ninapokwenda kuoga, mke wangu ana wivu mno na huwa anaikagua mara kwa mara,” alisema Patcho.
********************************
BBA All Star Ni habari nyingineIlianza Big Brother Africa mwaka 2003, ikaja Big Brother Afrika II (2007), ikaja Big Brother III (2008), baadaye Big Brother Revolution (2209), hata hivyo, zote zinatajwa ni tisa, 10 na itakayofunika ni ya 2010 ambayo inakwenda kwa jina la Big Brother All Stars.
Sababu ambayo inatajwa kuifanya Big Brother mwaka huu kuwa ya kipekee ni uamuzi wa kuwachukua mastaa waliong’ara kwenye fainali zilizopita na kuwapa nafasi ya kuingia tena mjengoni ili kushindana tena.
Tanzania imeshiriki mashindano hayo mara zote, na kufanya vizuri zaidi mwaka 2007, pale Ricahrd Bezuidenhout aliponyakua taji na kujibebea kitita cha Dola za Kimarekani 100 ambazo kwa ‘chenji’ ya wakati huo zilikuwa shilingi 130,000,000. Mwanga wa mafanikio kwa Tanzania kwenye mashindano hayo, ulioneshwa mapema mwaka 2003, pale Mwisho Mwampamba ‘Mr. Morogoro’ aliposhika nafafasi ya pili, nyuma ya Cheris Makubale wa Zambia.
Mwaka 2008, Tanzania iliwakilishwa na Latoya Lyakurwa ambaye aliifanya Tanzania kuwa wa kwanza kutolewa mjengoni kwa awamu hiyo, na Elizabeth Gupta ‘Queen’ alijitahidi mwaka 2009 lakini hakufika mbali, akawa amechomolewa.
Kionjo kikubwa mwaka huu, ni watazamaji kuwaona tena wale mastaa wao waliowakubali kwenye fainali mbalimbali zilizopita, hivyo kuifanya awamu hii ya 2010 kuwa tishio zaidi kuliko zilizotangulia.
*****************
TX Junior Adai mchango wa harusi kwa nguvu!Dogo anayelelewa na bendi ya nyumbani, Msondo Music, Hassan Shaaban Mhoja TX Moshi Jr, Ijumaa iliyopita alibambwa red-handed na safu hii, akidai kwa nguvu mchango wa harusi.
TX Jr ambaye ni mwana wa galacha wa muziki wa dansi, marehemu Shaaban Mhoja ‘TX Moshi William’, alibambwa akimdai mchango mwanamuziki wa Top Band, Allawi Junior. Kama hujainyaka ni kuwa dogo huyo ametangaza ndoa na mrembo ‘flani’ wa Mikocheni, Dar, anayeitwa Rehema.
TX alimkaba koo Allawi ambaye ni mshenga wake katika ndoa hiyo baada ya kukutana naye ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Dar es Salaam ambapo bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ walikuwa wakifanya makamuzi. “Namdai Allawi shilingi 200,000 ambazo aliahidi kunipa kama mchango wake kwenye harusi yangu,” alisema TX Jr alipozungumza na gazeti hili. Mzigo umeletwa na Richard Bukos.
****************************
Compiled by mc george/ijumaa wikienda
No comments:
Post a Comment