Ala, Kumbe Baby J na Wolper ni ndugu!
Kama haujapata bahati ya kuwa karibu na mastaa wawili waliyo katika tasnia tofauti, Jackline Wolper anayefanya Bongo Muvi na Jamila Abdallah ‘Baby J’ aliyeajiriwa na game ya muziki wa kizazi kipya, huwezi kujua kinachoendelea kati yao zaidi ya kudhani ni mashosti wa kawaida tu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na safu hii kwa muda mrefu, ShowBiz inakua ya kwanza kukufahamisha kwamba, wasanii hao ni ndugu wa damu a.k.a wa kufa na kuzikana japokuwa mmoja anaishi Zanzibar mwigine Dar es Salaam.
Wakipiga stori na safu hii huku wakionesha ‘love’ ya nguvu, wasanii hao kwa nyakati tofauti walisema kwamba, wao ni mtoto wa mjomba na shangazi na siyo undugu wa kukutana kwenye ustaa tu kama ilivyo kwa wengine.
“Mimi ni mtoto wa mjomba, Jack ni mtoto wa shangazi yangu japokuwa sisi tunaishi Zanzibar wao wako hapa Dar na Pwani, watu weaelewe hivyo,” alisema Baby J ambaye hivi sasa anafanya vizuri kupitia ngoma yake, Mpenzi wangu aliyompa shavu Banana Zorro.
Kwa upande wa Wolper hakuwa na cha kuongeza zaidi ya kusisitiza kuwa undugu wao ni wa kwenye shida na raha.
Mastaa ‘vichwa’ kutoka ndani ya game ya muziki wa dansi Bongo, waliotengeneza umoja wenye jina la Mapacha Watatu, Khareed Chuma ‘Chokoraa’, Joseph Michael ‘Jose Mara’ na Junior Hamza ‘Kalala Junior’, wako tayari kusimama stejini na kuwaambia mashabiki wao kuwa ile albamu yao waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu imeishakamilika.
Ndani ya ShowBiz meneja wa wakali hao, Hamisi Dakota alisema kwamba albamu hiyo yenye ‘mawe’ sita inayokwenda kwa jina la ‘Jasho la Mtu’ itatambulishwa kunako Ukumbi wa Hoteli ya Travertine uliopo Magomeni, Dar Ijumaa ya wiki ijayo.
“Tumejiandaa kwa muda mrefu kufanya mambo makubwa, nawaomba wapenzi wa burudani waje waone vitu tofauti, huku tukisindikizwa na ndugu zetu wa African Stars International ‘Twanga Pepeta’ na kiongozi wa Kundi la Jahazi Mordeln Taarab, Mzee Yusuf,” alisema Dakota.
Picha ya staa wa muziki wa Pop pande za Obama, Rohan Rihanna Fenty ‘Rihanna’ iliyopo kwenye kava la albamu yake mpya, Loud inayotarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu imezua utata kwa mashabiki wake.
Kwa mujibu wa mtandao wa hhh.com, mashabiki wengi wa mwanamuziki huyo mzaliwa wa Visiwa vya Barbados, wameonyesha kutokubaliana na picha hiyo wakiamni kwamba haina ubora wa kumshawishi mtu kununua albamu hiyo zaidi ya kushusha mauzo ya mzigo huo pale utakapondoka kitaani.
“Si aina ya picha ambazo zinafaa kutumiwa kwenye kava, kwanza haina mvuto na zaidi haikuwa katika uhalisia wa kava za muziki wa Pop, hivyo tunamtaka kuibadili mara moja,” ilisema taarifa katika mtandao huo ikunukuu maoni ya shabiki mmoja raia wa Canada.
Fleva ya ShowBiz ni kijisehemu ambacho kitakuwa kikishirikiana na wewe msomaji na kuangalia matatizo yaliyopo katika sanaa za Kibongo kama muziki, muvi na nyingine ambayo kwa kiasi fulani yamekuwa yakisabisha tasnia hizo ziendelee kupiga ‘maktaim’ hapa hapa TZ badala ya kuvuka mipaka na kwenda kimataifa.
Tukija katika ishu yetu ya leo, tangu muziki wa kizazi kipya ulivyoanza kuota mizizi hapa Bongo na kuwa ajira kwa baadhi ya wasanii, vijana wengi wamejitokeza na kuonyesha vipaji vyao na kuifanya game hiyo iendelee kupokea wafanyakazi wengi zaidi kila kukicha huku wengine wakidiriki hata kujenga majumba na kumiliki aseti mbalimbali kupitia mradi huo wa ‘voko na biti’.
Lakini jambo la ajabu ambalo limekuwa likiwaacha watu wengi vinywa wazi ni juu ya mwenendo mzima wa sanaa hiyo na muziki huo ambao watoto wa mjini wameupa jina la Big G, yaani ngoma nzuri inapotoka inapendwa na mashabiki wengi na baada ya muda mchache inapotea, hata kama ikichezwa watu wanakuwa hawana ‘taimu nayo’.
Na siyo ngoma peke yake inayopotea, hata msanii aliyefanya kazi hiyo pia anapotea na inawezekana ukikutana naye miezi miwili baadae utamuhurumia kwa jinsi alivyochoka, utakapomuuliza jibu lake litakuwa “Nimeibiwa”. Wapo wasanii wengi wa muziki huo ambao pamoja na uwezo waliokuwa nao kwenye game wamepotea wala hakuna anayeuliza wako wapi.
Kila shabiki wa burudani hiyo anafahamu uwezo na ukali wa kuimba alionao Ferouz Mrisho ‘Ferouz’ ambaye tangu alipokuwa na kundi lake la Daz Nundaz alikuwa anakimbiza ukija kwenye ngoma yake, Starehe ndiyo balaa kwakuwa alionekana kuwa tishio kwa wasanii wengine kiasi kwamba walitamani kufanya naye kolabo ili kujiongezea nguvu kunako sanaa hiyo, lakini leo hii baadhi ya watu wameishamsahau.
Huu ni mfano tu wa wasanii wengi ambao thamani yao kwenye muziki imekuwa kama ‘Big G’ ambayo inakuwa na utamu pale unapoanza kuitafuna lakini baada ya muda hutapenda kuendelea kuwa nayo mdomoni. Wakati bado tukiendelea
kutafuta mchawi wa hilo huku ikiwa halijafahamika tatizo ni nini hasa, shutuma nyingi zimekuwa zikirushwa kwa baadhi ya watangazaji wa vituo vya redio na televisheni wenye tabia ya kutanguliza pesa mbele bila kujali ubora wa kazi au kipaji cha kweli kabla ngoma hazijaenda hewani.
Lakini wasiwasi mwingine uliopo ni kuwa inawezekana uwezo mdogo wa kufikiri walionao baadhi ya wasanii katika kuandika mashairi yao na kutofanya utafiti wa kutosha ili kufahmu mashabiki wanahitaji kitu gani kwa wakati huo kabla ya kuingia kwenye sanaa hiyo vinanawafanya washindwe kutambua njia sahihi za kuwawezesha kubaki juu.
Pia wakati tunaendelea kurusha tuhuma hizo kwa watangazaji wasanii wetu pia wanatakiwa wajiulize mbali na muziki wao kuzimika kama ‘Big G’ kwanini hauvuki kwenda mbali zaidi, kwa mfano kuuza albamu Uingereza, Amerika na mataifa mengine ya Ulaya kama ilivyo kwa wenzetu Afrika Kusini, Nigeria, Congo, Uganda, Botswana, Senegal na nchi nyingine za Afrika?
Uchunguzi uliofanywa na ShowBiz umegundua kwamba, mbali na matatizo yote yanayotajwa bado kuna kila sababu kwa wasanii wetu kuumiza vichwa ili kutafuta aina ya muziki ambao utaenda mbali. Mashabiki wengi wamekuwa wakilalamika juu ya aina ya muziki ambao wasanii hao wanaufanya kuwa unaonekana kama ni wa kuiga badala ya wao kutafuta mtindo kutoka tamaduni za Kitanzania, jambo ambalo pengine lingewafanya kuwa juu kitaifa na kimataifa siku zote.
Huenda hili likawa jibu la moja kwa moja juu ya kile kinachowakuta wasanii wetu na kufananishwa na Big G, ni wazi kuwa mashabiki bado wana kiu kubwa ya kusikia kazi za kweli kutoka kwa akina Ferouz, Daz Baba, O-ten, Dataz, Pig Black, Crazy GK, Pico Kikongwe, Suma G, Mpaki, Mabaga Fresh, Sister P na wengine wengi katika kuusongesha muziki wetu.
Imeshushwa na Hemed Kisanda
Ishu mpya iliyodondoka pande hizi wakati tukijiandaa kuelekea mitamboni inasema kwamba, mtayarishaji muziki, Sandu George Mpanda ‘Kid Bwoy’ aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando,jijini Mwanza baada ya kupigwa kwa kitu kizito kichwani na mtu asiyejulikana ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo akiwa na ahueni tele.
Akipiga stori na ShowBiz kwa njia ya simu juzi kati, rafiki wa karibu na Kid, Phillbert Kabago alisema kwamba, jamaa ameruhusiwa kutoka jana (majuzi) na hivi sasa yuko nyumbani kwao Lumala akijipanga kabla ya kurudi tena kwenye game.
Bamiza Top 20 za MAGIC FM 92.9
1. Teja - Lady JD (2ND WEEK ON NO.1)
2. Karibu tena - Joh Makini
3. Mama ntilie - Jerry/Ray c/AT (2 WEEKS ON NO.1)
4. Chembaverment-Noorah/Ngweair
5. Sina raha-Sam
6. Unikimbie-Amini
7. Bado tunapanda – Tip Top Connection (3 WEEKS ON NO.1)
8. Ngosha the swaga Don-Fid Q
9. Salasala - Godzila
10. Tamaa mbaya – 20%
11. Kisiwa cha malavidavi – Z-Anto
12. Nauza kura yangu - Bonta
13. Shoga - Shaa (3WEEKS ON NO.1)
14. Mechi za ugenini – Roma
15. Budget – LWP
16. Iveta - Sajna
17. Demu wangu - Jaffaray/TID (2 WEEKS ON NO.1)
18. Hello – Hussein Machozi
19. Dakika moja – Ay,Mwana faa ft Hardmad (NEW)
20. Mama Halima – Linex (NEW)
Kama haujapata bahati ya kuwa karibu na mastaa wawili waliyo katika tasnia tofauti, Jackline Wolper anayefanya Bongo Muvi na Jamila Abdallah ‘Baby J’ aliyeajiriwa na game ya muziki wa kizazi kipya, huwezi kujua kinachoendelea kati yao zaidi ya kudhani ni mashosti wa kawaida tu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na safu hii kwa muda mrefu, ShowBiz inakua ya kwanza kukufahamisha kwamba, wasanii hao ni ndugu wa damu a.k.a wa kufa na kuzikana japokuwa mmoja anaishi Zanzibar mwigine Dar es Salaam.
Wakipiga stori na safu hii huku wakionesha ‘love’ ya nguvu, wasanii hao kwa nyakati tofauti walisema kwamba, wao ni mtoto wa mjomba na shangazi na siyo undugu wa kukutana kwenye ustaa tu kama ilivyo kwa wengine.
“Mimi ni mtoto wa mjomba, Jack ni mtoto wa shangazi yangu japokuwa sisi tunaishi Zanzibar wao wako hapa Dar na Pwani, watu weaelewe hivyo,” alisema Baby J ambaye hivi sasa anafanya vizuri kupitia ngoma yake, Mpenzi wangu aliyompa shavu Banana Zorro.
Kwa upande wa Wolper hakuwa na cha kuongeza zaidi ya kusisitiza kuwa undugu wao ni wa kwenye shida na raha.
*************************************************
Mapacha wa 3: Wako tayari kwa utambulishoMastaa ‘vichwa’ kutoka ndani ya game ya muziki wa dansi Bongo, waliotengeneza umoja wenye jina la Mapacha Watatu, Khareed Chuma ‘Chokoraa’, Joseph Michael ‘Jose Mara’ na Junior Hamza ‘Kalala Junior’, wako tayari kusimama stejini na kuwaambia mashabiki wao kuwa ile albamu yao waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu imeishakamilika.
Ndani ya ShowBiz meneja wa wakali hao, Hamisi Dakota alisema kwamba albamu hiyo yenye ‘mawe’ sita inayokwenda kwa jina la ‘Jasho la Mtu’ itatambulishwa kunako Ukumbi wa Hoteli ya Travertine uliopo Magomeni, Dar Ijumaa ya wiki ijayo.
“Tumejiandaa kwa muda mrefu kufanya mambo makubwa, nawaomba wapenzi wa burudani waje waone vitu tofauti, huku tukisindikizwa na ndugu zetu wa African Stars International ‘Twanga Pepeta’ na kiongozi wa Kundi la Jahazi Mordeln Taarab, Mzee Yusuf,” alisema Dakota.
**********************************************
Rihanna: Picha yake yawaboa mashabikiPicha ya staa wa muziki wa Pop pande za Obama, Rohan Rihanna Fenty ‘Rihanna’ iliyopo kwenye kava la albamu yake mpya, Loud inayotarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu imezua utata kwa mashabiki wake.
Kwa mujibu wa mtandao wa hhh.com, mashabiki wengi wa mwanamuziki huyo mzaliwa wa Visiwa vya Barbados, wameonyesha kutokubaliana na picha hiyo wakiamni kwamba haina ubora wa kumshawishi mtu kununua albamu hiyo zaidi ya kushusha mauzo ya mzigo huo pale utakapondoka kitaani.
“Si aina ya picha ambazo zinafaa kutumiwa kwenye kava, kwanza haina mvuto na zaidi haikuwa katika uhalisia wa kava za muziki wa Pop, hivyo tunamtaka kuibadili mara moja,” ilisema taarifa katika mtandao huo ikunukuu maoni ya shabiki mmoja raia wa Canada.
**************************************************
Mastaa wetu na thamani ya Big GFleva ya ShowBiz ni kijisehemu ambacho kitakuwa kikishirikiana na wewe msomaji na kuangalia matatizo yaliyopo katika sanaa za Kibongo kama muziki, muvi na nyingine ambayo kwa kiasi fulani yamekuwa yakisabisha tasnia hizo ziendelee kupiga ‘maktaim’ hapa hapa TZ badala ya kuvuka mipaka na kwenda kimataifa.
Tukija katika ishu yetu ya leo, tangu muziki wa kizazi kipya ulivyoanza kuota mizizi hapa Bongo na kuwa ajira kwa baadhi ya wasanii, vijana wengi wamejitokeza na kuonyesha vipaji vyao na kuifanya game hiyo iendelee kupokea wafanyakazi wengi zaidi kila kukicha huku wengine wakidiriki hata kujenga majumba na kumiliki aseti mbalimbali kupitia mradi huo wa ‘voko na biti’.
Lakini jambo la ajabu ambalo limekuwa likiwaacha watu wengi vinywa wazi ni juu ya mwenendo mzima wa sanaa hiyo na muziki huo ambao watoto wa mjini wameupa jina la Big G, yaani ngoma nzuri inapotoka inapendwa na mashabiki wengi na baada ya muda mchache inapotea, hata kama ikichezwa watu wanakuwa hawana ‘taimu nayo’.
Na siyo ngoma peke yake inayopotea, hata msanii aliyefanya kazi hiyo pia anapotea na inawezekana ukikutana naye miezi miwili baadae utamuhurumia kwa jinsi alivyochoka, utakapomuuliza jibu lake litakuwa “Nimeibiwa”. Wapo wasanii wengi wa muziki huo ambao pamoja na uwezo waliokuwa nao kwenye game wamepotea wala hakuna anayeuliza wako wapi.
Kila shabiki wa burudani hiyo anafahamu uwezo na ukali wa kuimba alionao Ferouz Mrisho ‘Ferouz’ ambaye tangu alipokuwa na kundi lake la Daz Nundaz alikuwa anakimbiza ukija kwenye ngoma yake, Starehe ndiyo balaa kwakuwa alionekana kuwa tishio kwa wasanii wengine kiasi kwamba walitamani kufanya naye kolabo ili kujiongezea nguvu kunako sanaa hiyo, lakini leo hii baadhi ya watu wameishamsahau.
Huu ni mfano tu wa wasanii wengi ambao thamani yao kwenye muziki imekuwa kama ‘Big G’ ambayo inakuwa na utamu pale unapoanza kuitafuna lakini baada ya muda hutapenda kuendelea kuwa nayo mdomoni. Wakati bado tukiendelea
kutafuta mchawi wa hilo huku ikiwa halijafahamika tatizo ni nini hasa, shutuma nyingi zimekuwa zikirushwa kwa baadhi ya watangazaji wa vituo vya redio na televisheni wenye tabia ya kutanguliza pesa mbele bila kujali ubora wa kazi au kipaji cha kweli kabla ngoma hazijaenda hewani.
Lakini wasiwasi mwingine uliopo ni kuwa inawezekana uwezo mdogo wa kufikiri walionao baadhi ya wasanii katika kuandika mashairi yao na kutofanya utafiti wa kutosha ili kufahmu mashabiki wanahitaji kitu gani kwa wakati huo kabla ya kuingia kwenye sanaa hiyo vinanawafanya washindwe kutambua njia sahihi za kuwawezesha kubaki juu.
Pia wakati tunaendelea kurusha tuhuma hizo kwa watangazaji wasanii wetu pia wanatakiwa wajiulize mbali na muziki wao kuzimika kama ‘Big G’ kwanini hauvuki kwenda mbali zaidi, kwa mfano kuuza albamu Uingereza, Amerika na mataifa mengine ya Ulaya kama ilivyo kwa wenzetu Afrika Kusini, Nigeria, Congo, Uganda, Botswana, Senegal na nchi nyingine za Afrika?
Uchunguzi uliofanywa na ShowBiz umegundua kwamba, mbali na matatizo yote yanayotajwa bado kuna kila sababu kwa wasanii wetu kuumiza vichwa ili kutafuta aina ya muziki ambao utaenda mbali. Mashabiki wengi wamekuwa wakilalamika juu ya aina ya muziki ambao wasanii hao wanaufanya kuwa unaonekana kama ni wa kuiga badala ya wao kutafuta mtindo kutoka tamaduni za Kitanzania, jambo ambalo pengine lingewafanya kuwa juu kitaifa na kimataifa siku zote.
Huenda hili likawa jibu la moja kwa moja juu ya kile kinachowakuta wasanii wetu na kufananishwa na Big G, ni wazi kuwa mashabiki bado wana kiu kubwa ya kusikia kazi za kweli kutoka kwa akina Ferouz, Daz Baba, O-ten, Dataz, Pig Black, Crazy GK, Pico Kikongwe, Suma G, Mpaki, Mabaga Fresh, Sister P na wengine wengi katika kuusongesha muziki wetu.
Imeshushwa na Hemed Kisanda
Ishu mpya iliyodondoka pande hizi wakati tukijiandaa kuelekea mitamboni inasema kwamba, mtayarishaji muziki, Sandu George Mpanda ‘Kid Bwoy’ aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando,jijini Mwanza baada ya kupigwa kwa kitu kizito kichwani na mtu asiyejulikana ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo akiwa na ahueni tele.
Akipiga stori na ShowBiz kwa njia ya simu juzi kati, rafiki wa karibu na Kid, Phillbert Kabago alisema kwamba, jamaa ameruhusiwa kutoka jana (majuzi) na hivi sasa yuko nyumbani kwao Lumala akijipanga kabla ya kurudi tena kwenye game.
*******************************
Bamiza Top 20 za MAGIC FM 92.9
1. Teja - Lady JD (2ND WEEK ON NO.1)
2. Karibu tena - Joh Makini
3. Mama ntilie - Jerry/Ray c/AT (2 WEEKS ON NO.1)
4. Chembaverment-Noorah/Ngweair
5. Sina raha-Sam
6. Unikimbie-Amini
7. Bado tunapanda – Tip Top Connection (3 WEEKS ON NO.1)
8. Ngosha the swaga Don-Fid Q
9. Salasala - Godzila
10. Tamaa mbaya – 20%
11. Kisiwa cha malavidavi – Z-Anto
12. Nauza kura yangu - Bonta
13. Shoga - Shaa (3WEEKS ON NO.1)
14. Mechi za ugenini – Roma
15. Budget – LWP
16. Iveta - Sajna
17. Demu wangu - Jaffaray/TID (2 WEEKS ON NO.1)
18. Hello – Hussein Machozi
19. Dakika moja – Ay,Mwana faa ft Hardmad (NEW)
20. Mama Halima – Linex (NEW)
No comments:
Post a Comment