Friday, January 8, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

AY
Joti
Tundaman

Mastaa waliokumbwa na kashkash za majambazi
Kupitia hapa, leo tumeona ni vema tuwacheki mastaa ambao kwa nyakati tofauti walijikuta katikati ya kashkash na majambazi, hivyo kuumia au kupata hasara.
Wakati tunagusa hili, ni vema ukawa na kumbukumbu kuwa hivi sasa Tundaman hajapona majeraha, baada ya kuvamiwa na majambazi ambao walimuibia na kumuumiza vibaya.

Tunda alikuwa safarini Afrika Kusini pamoja na Madee, aliporudi tu, usiku jamaa wakamvamia na kumpora zagazaga kibao, huku wakimuachia maumivu makali. Jamaa aliumaliza mwaka vibaya.

Mwanadada Gaidi, Zainab Lipangile ‘Zay B’ yeye mwaka jana aliumaliza kwa mtindo wa aina yake, baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na kuporwa vitu fulani fulani. Mbali na uporaji, jamaa walimlenga risasi lakini ikamkosa mwanamuziki huyo na kuingia kwenye mguu wa mdogo wake.

Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, yeye alivamiwa nyumbani kwake Mbezi miaka michache iliyopita, aliporwa zagazaga kibao, hivyo kuingia hasara kubwa.
Kati ya wasanii waliokumbwa na masahibu mwishoni mwaka jana, ni Ambwene Yesaya ‘AY’, yeye alivamiwa nyumbani kwake Sinza na kuporwa vitu kibao, na baada ya hapo jamaa akaamua kudumisha ulinzi kwa kuajiri Mmasai.

Mkali Dulayo yeye alivamiwa barabarani na kuporwa na vibaka wanaotumia silaha hatari, wakati Dully Sykes na Mr. Blu wao ilikuwa mitaa ya Tabata ambapo walitekwa na wahuni kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa. Hii iliripotiwa gazetini.

Kundi zima la Orijino Komedi liliingia kwenye kashkash ya majambazi mwaka jana, wakati memba wote walipokuwa wanaishi pamoja kwenye nyumba moja iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.

Baada ya kuvamiwa, wasanii wa kundi hilo, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Emanuel Mgaya ‘Masanja’, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Joseph Shamba ‘Vengu’, waliporwa fedha na vitu vingine vya thamani.
**************************************
**************************************

Veto ya Sugu yakubalika kitaani
Albamu mpya ya mwana Hip Hop ‘bei mbaya’ Bongo, Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ inayokwenda kwa jina la Veto, tayari imeanza kukubalika, kutokana na idadi kubwa ya Wamachinga kutoa ripoti chanya kuhusu mauzo.

Wamachinga walioripoti kwa mtu mzima Sugu a.k.a Mr. II katikati ya wiki hii, walisema kuwa jinsi wanavyosumbuliwa mtaani na wadau wanaoiulizia Veto, ni wazi kwamba inakubalika, hivyo wengi wanapenda kuipata.

Akiongea nasi juzi, Sugu alisema kuwa ameona Wadosi ambao walikuwa wanauza zamani ni wazinguaji, hivyo ameamua kubadilisha upepo kwa kuuza mwenyewe, akiwatumia Wamachinga nchi nzima ili kupata fedha yenye maelezo halisi.

“Watu wananipigia simu, wananiuliza Veto vipi? Wadosi wanatuumiza, kwahiyo tunasambaza na Wamachinga, kwahiyo popote pale mdau akimuona Mmachinga amwite amuulize Veto, atapata albamu bora ya Hip Hop,” alisema Sugu.
compiled by mc george

IJUMAA SHOWBIZ!

Akon
Cat Deluna
Fat Joe
Ja Rule
Busta Rhymes

AKON in the best kutoka kiwanja

Kupitia hapa, leo tunafanya tathmini ya jumla kuhusu mastaa wa kiwanja waliokuja nchini kufanya shoo, katika miaka ya hivi karibuni.

Katika tathmini yetu, mchizi mwenye asili ya Senegal, Akon ndiye anayeongoza kwa kupiga shoo kali akiwa Bongo kuliko yeyote yule aliyetokea kiwanja, kutokana na nyimbo zake kuwagusa wengi, pia uwezo wake wa kucheza na jukwaa na kuwadatisha mashabiki.

Kundi la vijana mapacha, P-Square, hili linastahili nafasi ya pili, uwezo mkubwa wa kucheza, kuwaimbisha mashabiki na kukubalika kwa nyimbo zao, ni vitu ambavyo vilisababisha shoo yao ivunje rekodi pale Leaders Club, Kinondoni, Dar.

Rapa aliyetikisa Bongo wakati wa shoo ya Fiesta mwaka jana, Busta Rhymes hakuna anayebisha kuwa jamaa anaweza kazi akiwa jukwaani, huyu anakamata nafasi ya tatu.

Fat Joe tunamuweka namba nne kutokana na uwezo wake mkubwa, akifuatiwa na Joe Thomas, wakati 50 Cent anabaki nafasi ya sita.

Hata hivyo, 50 anakula ‘credit’ kutokana na nyimbo zake kuchezeka, hivyo kwake anakuwa halazimiki kutumia nguvu nyingi kuwachezesha mashabiki, kwani wao wakisikia ngoma inakita, wenyewe wanaanza ‘ku-shake’ kabla mtu mzima hajamimina vocal.

Ja Rule, Shaggy, Sean Paul, Wayne Wonder, D’Banj, Eve, Jay z, Beyonce, KCI & Jojo na wengine, wao wanaingia kwenye orodha ya mastaa waliofanya shoo ya kuridhisha, wakati Cat Deluna na Brick & Lace ndiyo waliofanya vibaya zaidi.

Tuesday, January 5, 2010

SIRI YA KUISHI MAISHA MAREFU


Ili mtu ainshi maisha marefu, kuna vitu vingi vya kufanya na kuzingatia wakati wote wa maisha yake. Utafiti wa kisayansi umegundua kwamba suala la mtu kuzeeka kutokana na vinasaba (genes) alivyonavyo, linachukua nafasi ya theluthi moja tu na theluthi zingine mbili zinategemea sana staili ya maisha anayoishi.

Staili hiyo ni pamoja na jinsi ambavyo unakula na aina ya chakula unachokila. Vile vile mazoezi yanachukua nafasi kubwa katika kuimarisha afya ya mwili wako. Halikadhalika, msongo wa mawazo (stress) ni mtihani mwingine unaopaswa kujua jinsi ya kuushinda unapokupata, kwani huathiri afya kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa ripoti maalum ya Mabingwa wa Upasuaji nchini Marekani, kuhusu lishe na afya, asilimia 75 ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo, asilimia 60 ya vifo vitokanavyo na magonjwa yatokanayo na saratani ya wanawake na asilimi 40 ya magonjwa yatokanayo na saratani ya wanaume, yanasababishwa na ukosefu wa virutubisho mwilini na lishe bora.

Utafiti huo umesisitiza kuwa vifo vingi vingeweza kuepukwa iwapo watu wangejali afya zao ipasavyo. Katika hili, utaona kwamba umri wa mtu kuishi unatofautiana kati ya nchi moja na nyingine kutokana na kuwa na tofauti za kitamaduni na staili za maisha za watu wa nchi hizo.

Inaelezwa kwamba, raia wengi wa nchi za Kilatini hawaendi sana hospitali, lakini wanaishi maisha marefu na ni raia wachache sana wanaokufa kutokana na ugonjwa wa moyo, saratani au kiharusi. Hii ni taarifa njema kwa watoa huduma ya afya wengine, lakini Walatino wamewezaje kuwa hivi?

Wachambuzi wengi wa masuala ya kuishi maisha marefu wanaihusisha hali hii na tabia ya Walatini kuheshimu familia, kuzingatia maadili ya kazi, dini na mpangilio mzuri wa maisha ya kijamii.

Kuwa na familia imara na jamii yenye kuelewana huchangia kwa kiasi kikubwa mtu kuishi maisha marefu. Tunahitaji kuoanisha maisha yetu ya kila siku kati ya kazi na kujumuika na jamii kila siku. Tamaduni za kilatini zina fursa nyingi za kujumuika kati ya familia moja na nyingine na hata na wageni.

LISHE YA WALATINI
Mbali ya kuwa na maisha ya kijamii mazuri na kuzingatia suala zima la kupumzika baada ya saa za kazi, lishe ya Walatini wengi huzingatia sana mahitaji ya mwili na kanuni za afya. Walatini wanakula sana samaki, mboga mboga, jibini na mikate. Nyama nyekundi huliwa kwa kiasi kidoga sana miongoni mwao.

Hupenda kula chakula kidogo kidogo kila wakati, kiasi cha mara tano kwa siku. Katika kipindi hicho, hula aina mbalimbali ya vyakula asili vilivyotengenezwa kutokana na nafaka, matunda, mboga za majani na hupenda sana kufanya mazoezi.
Kukamilisha makala yote kwa ujumla, zingatia mambo yafuatayo ili kufikia kilele cha kufaidi maisha marefu yenye afya bora:

Epuka unene, kwani kuwa mnene siyo afya, mara nyingi unene huambatana na magonjwa ya moyo, kisukari n.k. Fanya mazoezi mara kwa mara, bila kusahau kuchua mwili mzima (body massage) ambako kumeelezwa huboresha kinga ya mwili.

Pata muda wa kupumzika, kwasababu kulala na kupata usingizi mzuri ni sehemu ya kanuni za afya bora. Sambamba na hilo, kama una nafasi, nenda safari ya mapumziko katika sehemu ambayo utapata muda wa kupumzika na kukaa katika mazingira yenye utulivu.

Mwisho kabisa, suala la kujamiina lisisahaulike. Inaelezwa kwamba, tendo la ndoa humuondolea mtu msongo wa mawazo na kumfanya aonekane kijana, kwani tendo hilo linapofanyika, hutoa kirutubisho aina ya ‘endorphins’ ambacho hushusha kiwango cha msongo wa mawazo. Hii haina maana kwamba uzini, oa mke na kama ni mwanamke olewa!

Monday, January 4, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Nelly
Kelly
Nicole

Stone
Ashanti

NELLY:...hawa ndiyo mademu aliowapitia

Bandika bandua ya ebwana dah! Mpya ya 2010, inaanza kwa speed ya ajabu kwa kukudondoshea stori ya rapa mwenye jina kubwa toka kiwanja, Brazameni, Nelly Cornell Iral Haynes Jr ‘Nelly’ na warembo aliowahi kudondoka nao kitandani.

Nelly aliyezaliwa Austi Texas, Marekani Novemba 2, 1974, ana age ya 35, pamoja na ustaa wake wote amekula ‘urojo’ na mademu wanne tu, tofauti na mastaa wengine ambao ebwana dah! iliwahi kuwaweka kwenye ‘page’ hii wakiwa na msururu wa wapenzi wasiohesabika.

Jamaa huyu mwenye asili ya black na urefu wa sentimita 185, warembo wake wanne ni pamoja na Joss Stone katika days kitambo kabla ya 2001-02 kujikuta ‘akibanjuka’na Respected nyota wa R&B toka majuu, Sistaduu, Kelly Rowland.

Baada ya Kelly, 2003 mshikaji aliripotiwa kuwa in love relation na staa mwinbgine wa R&B, Ashanti Douglas, mwenye love attraction ya kutosha iliyomfanya Nelly ajenge kibanda kabisa kwa lengo la kufanya makazi ya kudumu.

Ebwana dah! inakupa sad newz iliyomkuta Ashanti 2004 baada ya mshkaji huyo kuhamishia utamu kwa Nicole Narain, modo mwenye jina kubwa kiwanja.

Peruzi ya Ebwana dah inathubutu kukujuza kuwa baada ya Nelly kufanikiwa kumkamata Nicole hakuwahi kuripotiwa tena kuwa in love na baby mwingine labda kama itatangazwa vinginevyo hapo later.
***************************************
Mastaa wamejipangaje 2010?
Chege


Madee

Prof Jay

Mastaa wamejipangaje 2010?

Safu yako maarufu, Abby Cool & MC George Over the Weekend mwishoni mwa wiki iliyopita ilipiga stori mbili, tatu na basadhi ya Icons wa Bongo Flava na industry nyingine mbalimbali ili kujua wamejipangaje kuukabili mwaka mpya wa 2010 na mikakati yao mingine kunako game zao.

MADEE:
a.k.a Rais wa Manzese
Mwaka jana wa 2009 nilirekodi ngoma 42, nikashirikishwa 5, nikatoa albamu moja, nikafanya shoo 52 za ndani huku za nje ya Bongo zikiwa 5. Pia nikafanikiwa kuongeza idadi ya marafiki.

Kuhusu 2010 nimejipanga kufanya albamu yangu ya nne, natarajia kufanya shoo kibao zaidi ya zile za 2009 ambazo I believe kabisa kuwa zitaniongezea heshima zaidi.

“Mbali na ishu za kazi ya muziki, Mei mwaka huu natarajia kwenda kucheki angalau mechi moja kwenye michuano ya kuwania Kombe la Dunia itakayopigwa huko Sauzi.

CHEGGE:
2010 nina mikakati bomba coz baada ya kutondosha albamu yangu inayokwenda kwa jina la Chegge na kuachia ngoma kadhaa ikiwemo ‘Mambo bado’ niliyofanya na Lady Jaydee, ndani ya 2010 inakuja project moja makini nitakayoifanya na Temba ambayo kwa idea tu, nadhani itakuwa more better than ever before na mkakati kamili utakuwa on air Februari 14, siku ya wapendanao (Valentine day).”

HEMEDY:
“Mbali na ngoma mpya ambayo tayari nimerelease hivi karubuni pia najipanga kuachia video yake soon na later nitatoa albamu itakayokuwa na jina la King of Melodies. Vilele fansi wangu wategemee kunicheki katika muvi kibao za Kibongo zitakazoingia kitaa muda si mrefu ikiwemo ya kwangu mwenyewe inayoitwa Three Brothers, lakini pamoja na ishu hizo, zaidi ni kujiendeleza kielimu ndani ya 2010.”

PROF. JAY: Amlilia Kawawa
Nguzo muhimu katika industry ya Muziki wa kizazi Kipya, Joseph Haule ‘Prof. Jize’, ana machungu ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Rashid Mfaume Kawawa ‘Simba wa Vita’ kilichojiri Alhamisi last week, Hemed Kisanda anatiririka nayo.

Akipiga stori kwa masikikitiko na safu hii 2dayz after msiba huo jijini Dar, Profesa Jay alisema ishu hiyo ilimshtua na kumuumiza kinoma coz alimfahamu in and out Simba wa Vita kwa namna alivyoshiriki katika War against wakoloni na kupatikana kwa independence ya wabongo.

“Wakati mwingine unaweza kuona kama taifa linaelekea gizani kwani nguzo muhimu ndiyo zinakatika, lakini yote kwa yote ni kuacha mapenzi ya Mungu yatimie,” aliosema Jay ambaye mikakati yake kwa mwaka huu wa 2010 ni kuhakikisha anabaki juu na kwenda kimataifa zaidi kwakuwa tayari milango yake imeshafunguka kupitia MTV Africa na ishu nyingine kibao zilizomfanya ajulikane nje ya Boingo.

compiled by mc george