Scheduled downtime maintenance on all Ning Networks is beginning now and will last for approximately 4 hours. During this time, your Ning Network will be inaccessible and display a branded maintenance page. We’ll have another update for you here when the maintenance is completed. ************************************************ Usione kimya, kwenye mtandao wako wa www.globalpublisherstz.com, kwani kuna maintainence inafanyika kwenye main server ambao ni Ning.Com na baada ya muda watakuwa hewani, hii ni katika kuboresha mitandao yote ya Ning
>>Wakutanishwa kwenye steji moja, kambi moja!
Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, Yusuf Mlela na aliyekuwa mshindi wa pili, Hemed Suleiman ambao hawapikiki chungu kimoja wamekutanishwa kwenye steji moja na kupiga shoo ya nani zaidi, Richard Bukos anashuka nayo.
Mwanzoni mwa wiki hii ShowBiz ilidondoka pande za Club Billicanas, Dar na kuwakuta na mastaa hao wa muvi wakirekodi mpambano huo wenye jina la Selebuka ambao hurushwa hewani kupitia kituo cha televisheni cha TBC 1 kila siku ya Jumapili.
Katika mpambano huo mastaa hao walionekana kuwagawa mashabiki waliohudhuria kwa wingi siku hiyo kama wageni waalikwa huku ishu zaidi zikisema kwamba wasanii hao hukutana katika kambi moja ya mazoezi kabla ya kurekodi. Mbali na Hemed na Mlela, mastaa wengine kibao kama Chegge, Angie, Jini Kabula na wengine kibao wanawania kitita cha shilingi milioni 25 za Kibongo.
XXXXXXXXXXXXXXXX
Lady Jaydee
Lady Jaydee ametajwa kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike 2009/ 10
VISIT the Harusi Trade Fair, Tanzania First Annual Wedding Fair on 9 and 10 April from 10 AM onwards at Diamond Jubilee Hall, in Dar Es salaam, 52 Exhibitors from cakes to catering to cards... All under one ROOF.....Your support Shall highly be appreciated...
Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011
Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote.
Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 280 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jose Chameleone, Samba Mapangala, Saida Karoli, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate,Banana Zorro & the B Band, Joh Makini, Nako2Nako Soldiers, Nyota Ndogo,Thandiswa, Culture Musical Club na wengineo wengi.
MWISHO wa kupokea maombi
31 July 2010
Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri , malazi,chakula na matumizi madogo madogo.Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri
Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa
Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi kutoka kwako kabla ya MWISHO wa kutuma maombi. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:
form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
nakala moja au mbili ya kazi zako (CD au DVD)
picha moja au mbili( JPG au karatasi)
Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo chini.
Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.
Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu.inga dhidi ya magonjwa ya moyotaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.
Wiki mbili zilizopita tumeona vyakula kama karanga, korosho vinvyoweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, wiki hii pia tunaona papai nalo limo kwenye orodha ya vyakula vinavyotoa kinga ya ugonjwa huo.
Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.
HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.
KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.
KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya Ć¢€˜beta-caroteneĆ¢€™ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k
NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.
TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.
Jamie Foxx Fataki aliyeonja penzi la Oprah Kiumri anazidiwa na Oprah Winfrey kwa miaka 14 lakini hakuona soo kukwea on bed na mwanamama huyo anayeheshimika duniani ambaye pia ni roho ya kampeni za Rais Barack Obama katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2008, Ebwana Dah!
Ni staa wa Hollywood, Jamie Foxx mbali na Oprah, pia ana rekodi ya kutoka na warembo mastaa kibao katika idadi ambayo Kibongo bongo anatosha kuitwa fataki.
Adrian Kelle anatajwa wa kwanza, hii ni kwa mujibu wa site inayodili na ishuz za mastaa wa mbele katika ile pointi ya nani kamrukia nani, lini na kwa staili gani.
Haielezwi ni lini Adrian alikuwa na Jamie na waliachanaje ila Debbie Allen anatajwa wa pili kisha Dolicia Bryant, Dominique Simone, Eva Pigford, Nikki Giavasis, Sofia Vergara, Stacy Kiebler, Vivica Fox ambao nao hawana maelezo ya wakati.
Mwaka 1996, alijikunja na Garcelle Nilon, 2002 hadi 2004 akabinuka kwa Iliana Fischer, 2003-06, akatuliza kasuku wake kwa Meagan Good, 2004-05, akafanya kweli na Leila Arcieri, 2004 pia alichangamsha damu na Victoria Schweizer.
Mwanamama Oprah alinasa kwenye tundu bovu mwaka 2005 kisha akaunga listi na Christina Milian mwaka huo huo, 2006, Jamie alijichuja kwa Fantasia Barrino kabla ya Lil’ Kim mwaka 2007 na Claudia Jordan mwaka huo huo. Ashley Scott alikwenda sawa na Jamie mwaka 2008 na mwaka huo huo akamcheki, Stacy Keibler.
Jina lake kamili ni Eric Marlon Bishop, Jamie Foxx ni a.k.a. Alizaliwa Desemba 13, 1967, Terrell, Texas, Marekani. Ana umri wa miaka 42. Tuambie, wiki ijayo tutoke na staa gni kupitia hapa Ebwana Dah? Simu zetu ni 0715 110 173.
**************************************
XXL Teen Xtra Awards 2010 Johmakini, Chid Benz, Ngwea, Fid Q, Belle 9, Marlaw, Chege vitani Mastaa saba wenye alama A katika muziki wa kizazi kipya, wamepambanishwa katika kumsaka mkali zaidi ambaye atabeba tuzo katika category Msanii Bora wa Kiume (Male Artist of the Year).
Wakali hao, John Simon ‘Johmakini’, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, Albert Mangwea ‘Ngwea’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Belle 9, Lawrence Malima ‘Marlaw’ na Said Juma ‘Chege’ wapo kundi M ambalo ndilo la Msanii Bora wa Kiume.
Kila msanii amepewa namba yake ya ushiriki, Johmakini (M1), Chid Benz (M2), Ngwea (M3), Belle 9 (M4), Marlaw (M5), Fid Q (M6) na Chege (M7) na ili kumpigia kura msanii unayempenda, unatakiwa uandike ujumbe katika simu ya mkononi (SMS), ukiandika neno TN unaacha nafasi, kisha unaandika namba ya msanii halafu unatuma kwenda namba 15551.
Tuzo hizo za Kituo cha Radio Clouds FM, zinatolewa kupitia kipindi cha XXL na zinajulikana kwa jina la XXL Teen Xtra Awards 2010 ambazo zimepambanisha category 16 yaani (A) Sport Star of the Year (B) TV King of the Year (C) TV Queen of the Year (D) Music Website of the Year (E) Hottest Dance Video of the Year (F) Sizzling Video of the Year (G) Video Producer of the Year.
Nyingine ni (H) Group of the Year (I) Stage & Live Performance of the Year (J) Brandy New Artist of the Year (K) Music Producer of the Year (L) Most Addictive Track of the Year (N) Female Artist of the Year (O) Lyricist of the Year na (P) Hottest Collabo of the Year.
Rapa mahiri wa Twanga, Khalid Chokoraa, akiwapandisha mdadi mashabiki wake wakati wa onesho lao usiku wa kuamkia leo pale maskani Mango Garden ikiwa ni raha za Pasaka
..malovee
Mzee wa Full Shangwe John Bukuku, Asha Baraka na Khadija Kalili (kulia)
Mastaa wa Bongo, Steve Kanumba (kushoto) na Ray wakiwa na Said Mdoe, bosi wa Screen Masters