Saturday, October 8, 2016

MSANII CHEGE AADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUTOA MSAADA KWA HOSPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR

 Msanii wa Muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akiweka sawa baadhi ya zawadi alikuwa ameziandaa kwa ajili ya Wagonjwa Temeke Hospitali.
 Msanii wa Muziki kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akizungumza jambo na mmoja ya wauguzi wa
Temeke Hospitali jijini Dar.
 Chege na Temba wakiteta jambo mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Temeke
 Chege Chigunda akizungumza na Waandishi wa habari
 Chege Chigunda na baadhi ya Wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakielekea wodini
 Chege Chigunda akiwasiliana na baadhi ya watu kabla ya kuingia wodini
 Msanii wa Muziki wa Bongofleva Mheshimiwa Temba  akitoa zawadi kwa wagonjwa
 Chege Chigunda akitoa baadhi ya Zawadi kwa wagonjwa
 Mh Temba akiingia wodini  kupeleka zawadi kwa Wagonjwa
 Mhe. Temba akigawa zawadi kwa wagonjwa
 Baadhi wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe akitoa zawadi kwa wagonjwa
 Chege Chigunda akiwa amembeba mtoto Hadija Abdalah akiwa na Mama yake Mwanahawa Juma.
Na Humphrey Shao, blog ya Jamii MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka kundi la Wanaume Family Chege Chigunda , leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea hospitlai ya Rufaa ya Temeke na kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya Watoto waliozwa hapo kutokana na matatizo mbalimbali. Akizungumza na Mwandishi wa blog hii Mapema leo Hospitalini hapo chege alisema kuwa imekuwa tofauti sana kwa watu kupenda kusheherekea katika nyumba za starehe lakini yeye ameamua kukaa na watoto hao wagonjwa hili kurudisha kile ancho kipata kwa jamii. “Chege Chigunda aezaliwa leo hivyo ndio maana nipo hapa motto wa Mama Said kushherekea siku yangu ya kuzaliwa na wagonjwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kama mnavyoziona Pampers , Dawa za Mswaki na Dawa kwa ajili ya wagonjwa ambao awana uwezo wa kujijinunuli a hivyo katika siku ya leo wamepata fursa ya kununuliwa madawa na mimi” anasema Chege. Anasema kuwa maisha yamebadilika sana na inapaswa watu kurudi nyuma na kufanya yale yaliyoa mazuri yanayompendeza Mungu kwa kusheherekea siku zao za kuzaliwa na watu ambao wanamatazo na wenye uhitaji hili kuweza kuwapa faraja ambayo wakuwa wameikosa kwa muda kutokana na matatizo yaliyowakuta. Alimaliza kwa kutoa wito kwa wasanii na watu maharufu kuwa na utamaduni wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mablimbali kila wanapopata nafasi na kiasi kidogo kwani kutoa akuhitaji kuwa na utajiri mkubwa bali ni moyo tu.
Attachments area Click here to Reply, Reply to all, or Forward

No comments: