Wednesday, June 22, 2011

Je, Ungependa Usiumwe?


By John Haule – 0768215956
johnhaule@hotmail.com
Ni rahisi mno! Unatakiwa utafune punje moja tu ya kitunguu swaumu kila siku na hutaumwa kamwe, na pengine ukasahau hata njia ya kufika hospitali.

Ndiyo. Kuna mtu aliwahi kuishi duniani akijulikana kama Hippocrates. Hippocrates, alijulikana duniani kote kama Baba wa mitishamba yote ulimwenguni aliwahi kusema “Mtu atakaye tafuna punje moja ya kitunguu swaumu na kumeza maji yake kila asubuhi, basi huyo hataumwa magonjwa ya aina yoyote”

Kitunguu swaumu ambacho kinajulikana katika nyanja ya madawa kwa jina la Allium Salivum, ni jamii ya vitunguu na hupandwa katika bustani za mboga. Kilianza kulimwa miaka mingi sana iliyopita. Kitunguu swaumu kimeshatoa majibu yenye uhakika katika matumizi ya aina nyingi kama vile dawa ya kienyeji, chakula, mmea wa kuzalishia dawa, dawa ya usafi kwa kuua bacteria na fangasi, na pengine kama kitu muhimu katika masuala ya urembo.

Asili hasa ya kitunguu swaumu ni Asia ya kati, na kiligunduliwa nchini China miaka 3000 Kabla ya Kristo. Kwa sasa kitunguu swaumu kinalimwa sehemu nyingi tu kama vile India, Ethiopia, Philippines, Mexico, Brazil na Kenya. Hapo utagundua kuwa China na India kuna idadi kubwa sana ya watu duniani kwa vile wao hawaumwi kizembe-zembe na hawafi kijinga-jinga kwa vile matumizi ya kitunguu swaumu kwao ni kitu cha kawaida tu katika milo yao. Tena kama Watanzania watakula kitunguu swaumu kila siku, basi pia tafiti zinaoonyesha tutakuwa na afya njema, maumbile ya kuvutia hasa wanawake ambao watakuwa warembo sana, na Vilevile tutakuwa na ongezeko kubwa la uwezo wa kufikiri (Extra clear thinking capacity)

Kitunguu swaumu kina kiasi kikubwa sana cha calcium na protini, na kimetumika miaka mingi kutibu maradhi kama vile Pumu, Uziwi, Ukoma, Madonda ya koo, Maumivu ya mifupa, homa kali, Minyoo, maradhi ya ini na kibofu cha mkojo. Kitunguu swaumu kimegundulika kuwa kama rafiki wa damu mwilini kwani mara unapokula huwa kinaenda kutoa sumu zote kwenye damu na kuipa damu vitamini, halafu kinaongeza uwezo wa damu kusafiri vyema katika mishipa hivyo kumfanya mtu ajisikie ana afya njema kila siku. Kufuatia utafiti uliofanywa hivi karibuni kitunguu swaumu kimegundulika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa ya moyo kwa kupenya katika mishipa ya damu na kuvunja-vunja cholestrerol zote ili kupisha njia ya damu iwe safi na wazi.

Hiyo ndiyo nguvu ya ajabu na ya kipekee inayopatikana katika kitunguu swaumu tu duniani.

Hivyo, nawashauri Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wizara ya kilimo tukae pamoja kuangalia namna ya kuanzisha kampeni ya kupanda kitunguu swaumu, na kuhakikisha kila mtu anapata punje 365 kwa mwaka. Watu wakisikia hii habari basi wataanza kutafuna dawa hii na kitakachotokea ni upungufu wa vitunguu swaumu pamoja na kupanda bei kwa bidhaa hii. Lakini kadiri kila mtu atakavyokula ndivyo foleni katika mabenchi hospitalini itakavyopungua. Tafiti binafsi nilizofanya zimeonyesha kuwa kutatokea kupungua kwa wagonjwa hospitalini kwa asilimia 60% - 70% iwapo watu wote watatumia dawa hii kwa miezi mitatu tu, na kama wote tutakula punje hiyo kwa mwaka mmoja basi ni 20% ya watanzania wataenda hospitali kwa ajili ya magonjwa sugu tu na hivyo kuwapunguzia mzigo madaktari ambao wamezidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa. Kwa mfano idara ya OPD hospitali ya Temeke Dar Es salaam madaktari imewabidi waweke bango la kuwaomba wagonjwa msamaha kwa kuwapanga foleni ndefu kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa. Nilipoliona bango lile nilijikuta nikimpa pole Dr. Luiza na kumuahidi nitashiriki kumsaidia.

Kuna jambo ambalo linaweza kuwakatisha tamaa ya kupona baadhi ya watu watakaotumia dawa hii. Ni kwamba, tafiti zimeonyesha kuwa upo uwezekano wa baadhi ya vitunguu swaumu kutokuwa na dawa. Hii inatokea, na inahusisha sana aina ya udongo uliopo mahali kilipooteshwa kitunguu hicho. Hivyo Wamarekani kwa kujua hilo tarehe 4th October 2004 waliwatangazia Wamarekani wote kula punje moja tu ya kitunguu swaumu kwa siku na wametengeneza vidonge vya vitunguu swaumu ambavyo tayari vimepitishwa maabara kuhakiki ubora kabla ya kusindikwa na kutengezwa vidonge vyenye uhakika wa tiba. Vidonge hivyo ninavyo, na vipo hapa Dar Es Salaam na vinapatikana kwa kupiga simu namba 0768 215 956 au email – rotion@live.com

Zipo dawa nyingi mno ambazo zimegunduliwa duniani na ni muhimu kuzifanyia kazi. Hata hivyo kazi hiyo haitawezekana kama wafanyabiashara za madawa na serikali kupitia wizara ya afya hawatatoa ushirikiano katika kuwekeza katika sekta hii ya tafiti za tiba kwa kuwa kuna hitaji kubwa la kusafiri pembe nyingi za dunia kuona baadhi ya mimea ambayo Tanzania hakuna. Pia ni muhimu kutembelea vyuo vikuu duniani vinavyotafiti tiba asili kama India, China na Canada ili kubadilishana tafiti na wataalamu toka nje ambao wapo mbali sana kiutendaji na wana mafanikio makubwa mno.

KARIBUNI SANA.    

 

2 comments:

emu-three said...

Kitungu swaumu twakipenda kwenye pilau..nasikia kuwa kinatibu jino...tafuna pale jino lilipo na umia hapo kwa muda mrefu..jino litapona na wadudu kwishini!

Freddy Macha said...

Huu ni ukweli kabisa, bwana Haule... mimea mingi ina dawa (au ni dawa) na imetumika karne si kidogo kutibu kila aina ya maradhi na kuongeza siha ya maisha ya wanadamu na wanyama. Si tumezoa paka wakila majani (na wao ni wala nyama) siku wakiumwa? Paka ana maisha tisa. Mjuzi. Anafaham. Haya yamezua hata wasanii wakatunga na kusifia. Mathalan...
Moja ya nyimbo maarufu Brazil ni ule uliotungwa na Mwanamuziki gwiji wa huko Gilberto Gil... anaposema katika kibao chake cha Kireno ; "A Pilula de Alho" (Kidonge cha Kitungu Saumu)
"...ukila kimoja, wala husikii ladha yake, lakini unayaaga maradhi yako.."
Sikiliza zaidi:
http://www.vagalume.com.br/gilberto-gil/pilula-de-alho.html