Zahir Zorro
Steve & Baby Boy
Tippo Athuman
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo waliokuwa chini ya Lebo ya Zizzou Entertainment, Albert Mangwea ‘Ngwair’, Steve RnB, Edson William ‘Baby Boy’, Squeezer na Mzee Zahir Zorro wamemaliza mkataba wao wa awali na kampuni hiyo na sasa wako huru kwenda lebo nyingine, Ripota wetu anashuka nayo.
Akipiga stori na Showbiz, Mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Tippo Athuman, aliweka plain kuwa mkataba na wasanii hao umeisha tangu Machi mwaka huu na kwamba hana mpango wa kuingia nao mkataba mwingine.
“Mkataba wao uliisha tangu Machi mwaka huu na hakuna mpango wa kuingia nao mkataba mpya, naangalia uwezekano wa kuibua vipaji vingine, kwa sasa wanaruhusiwa kuwa chini ya mtu au kampuni nyingine,” alisema Tippo.
Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi za wasanii hao kama kurekodi nyimbo, kutengeneza albamu, kusimamia mauzo, utengenezaji wa video na mavazi. Wakati wasanii hao wanamaliza mkataba na Zizzou Entertainment, wimbo wa Don’t Give UP waliorekodi kwa pamoja, unabamba ile mbaya katika vituo mbalimbali vya televiseni na radio nchini. Pia Ngwea, Blu na Diamond wanatarajiwa kuonekana runingani na kusikika redioni soon kwenye kazi yao ya mwisho waliyoifanya ya kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment