Wednesday, June 29, 2011

TIBA YA KISUKARI

Writen By:
John Haule – Dietist
Phone +255 768 215 956   Email: rotion@live.com

Hivi hakuna tiba rahisi ya Kisukari? Hili ni swali ambalo kila mtu nadhani amechoka kulisikia midomoni mwa wagonjwa wa ugonjwa huu hatari duniani na ambao hauna tiba. Kitu cha msingi unachoweza kumsaidia mgonjwa huyu ni kumwelekeza namna ya kudhibiti uzito wa mwili wake usiongezeke na kwa wakati huo huo ukamwelewesha namna ya kupunguza kiwango cha sukari mwilini mwake.

Kisukari ni ugonjwa hatari ambao ni vigumu kuugundua na kuutibu pia. Siri kubwa ya ugonjwa huu ni tabia yake ya kuzibana “pancreas” zisizalishe insulin.

Kuna aina kubwa mbili za Kisukari.
1.    Aina ya kwanza ni kisukari ambayo inaanza utotoni wakati insulin ndio zinahitajika kwa wingi mwilini.
2.    Aina ya pili ni kisukari ambayo hugundulika wakati mtu ameshakuwa na Vilevile huwa anahitaji insulin pia kwa afya njema.

Wakati aina zote za kisukari zinahitaji kwanza kabisa ushauri wa dakitari pamoja na madawa ya hospitalini, wewe mwenyewe tu unaweza ukaidhibiti sukari mwilini mwako na ukaishi kwa raha kana kwamba huna maradhi hayo kabisaaa.. tena utakuwa ukitumia dawa toka jikoni na pengine bustani inayoizunguka nyumba yako tu bila gharama za kutisha kama yalivyo madawa ya hospitali na waganga wa kienyeji ambao dawa zao nyingi ni sumu mwilini kwa kutofanyiwa tafiti za kisayansi, na chache zinakuwa za ukweli na zina uwezo wa kutoa majibu sahihi.

Tikiti chungu (Bitter Melon)
Tikiti hili ni mara chache sana kuliona katika bustani zetu, masokoni, nk. Unaweza kulipata tikiti hili kwa kupita katika masoko ya uhindini au ukawauliza marafiki wa kihindi maana hili tikiti ni zao lenye asili ya Asia hasa uhindini.
Ukila tikiti hili chungu basi ujue kuwa litakusaidia kuongeza uzalishaji wa chembechembe za nguvu za insulini katika “pancreas” zinazojulikana kitaalamu kama “beta cells” halafu kwa wakati huohuo tikiti hilo litakuwa likidhibiti sukari katika damu kwa kufanya ucheleweshaji wa makusudi wa ufyonzaji wa glucose katika damu.
 
Katakata tikiti hilo, tia katika blender na ulisage halafu ongeza maji upate juice. Weka ndani ya friji na unywe mara kwa mara kutwa nzima. Kitaalamu Unatakiwa uwe umekunywa walau glasi mbili kwa kutwa moja. Zoezi hili likifanyika ndani ya wiki nne basi utagundua kuwa umetoka katika utumwa mbaya wa gonjwa hili.

Mdalasini (Cinnamon)

Wengi wetu tunajua mdalasini ni nini. Kwa wale wasiojua mdalasini ningewashauri wakaulize sokoni popote pale wataona magamba ya mti yenye rangi ya kahawia. Mdalasini imegundulika kuwa na uwezo mkubwa sana wa kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa haraka mno kushinda chochote. Moja ya njia nafuu na rahisi kupata nafuu ya ugonjwa huu wa kisukari ni kunywa maji yaliyochemshwa na mdalasini na baking soda kwa dakika 20 halafu yakaachwa yakapoa na kuhifadhiwa katika friji yakapoa. Maji haya ukinywa walau glasi mbili kwa siku unaweza ukaidhibiti kabisa sukari mwilini.

Kitunguu maji & Kitunguu swaumu (Garlic & Onion)

Kitunguu maji (Allium Cepa)
Kwa kawaida hivi ni viungo tu pale jikoni na wengi wanajua hivyo. Viungo hivi vikifika pale tunapohitaji tiba basi hata majina yake hubadilika ambapo kitunguu maji hutwa Allium Cepa na kitunguu swaumu huitwa Allium Salivum.
Viungo hivi ni vya ajabu! Vimeshatoa majibu kibao katika tiba na hasa pale linapokuja suala la Kisukari (Diabetes) kwa kasi yake ya kushusha kiwango cha sukari katika damu. Ndani ya kitunguu maji kunasadikika kuwepo tiba muhimu iitwayo kitaalamu kama Allyl Propyl Disulphide (APDS) na Diallyl Disulphide Oxide (Allicin) na mchanganyiko wa flavonoids ambazo ni “Mpango mzima” katika kutibu maradhi na huku zikiihakikishia damu mtiririko unaotakiwa kusambaa mwilini kwa uhakika zaidi.
Kitunguu maji hiki ni chanzo kikubwa cha madini ya chromium ambayo yanahitajika sana katika kazi ya kurekebisha kiwango cha sukari katika damu kwa kuziwezesha insulini kufanya kazi yake vizuri. Tafiti za karibuni zimebainisha kuwa kitunguu maji kiwe kimepikwa au ni kibichi kinapofika kazini uwezo wake kiutendaji unabaki kuwa ni uleule japo kinapungua nguvu kidogo kikipikwa kwa vile baadhi ya ubora hupotea jikoni. Kwa hiyo watafiti waliridhika na kukipa hadhi ya kuwa tiba kwa wagonjwa wa diabetes.

Kitunguu Swaumu (Allium Salivum)
Hiki kinasaidia kuzuia uharibifu kwenye figo, mishipa ya damu, macho na ngozi ambapo ni maeneo ambayo kisukari kisipodhibitiwa basi huaathiri sana sehemu hizi za mwili. Hivyo magonjwa ya moyo, na kiharusi (Paralysis) ni magonjwa ambata ambayo kwa kula tu kitunguu swaumu huwa yanajitibu yenyewe, na hatari itakuja baadaye kwa mtu anayeumwa kisukari halafu hakutumia kitunguu swaumu pale magojwa hayo yatakapoungana na kisukari na kusababisha kifo kwa mgonjwa kwa kuwa magonjwa hayo hayakudhibitiwa….Ndiyo, Hayo ni magonjwa nyemelezi kwa mgonjwa wa kisukari.

Mambo ya kuzingatia mgonjwa wa kisukari.

Yapo mambo mengi ambayo mgonjwa wa kisukari anatakiwa ayakwepe ili kuinusuru afya yake. Kutozingatia mambo hayo kunaweza kusababisha hali ya mgonjwa kuwa mbaya na pengine kifo. Mambo hayo ni kama yafuatayo:
1.    Kula matunda mengi yenye maji kwa mwingi. Hii itamsaidia mgonjwa kupambana vilivyo na kiwango cha sukari inayomsumbua mwilini kwa kuwa matunda yenye maji mengi yana dawa inayowezesha kufanya mwili ujisafishe na kutoa kwa njia ya mkojo uchafu mwingi kama vile toxins, sugars, impurities, na cholesterol na kuleta nafuu kwa mgonjwa wa kisukari.
2.    Matunda hasa kwa wakazi wa mijini ni ghali na hivyo si watu wote wanaweza kuyanunua. Kama wewe ni mgonjwa au una mgonjwa ndani basi kama huna hela za kumudu kununua matunda itakubidi uongeze kiasi cha maji ya kunywa kila siku kama mbadala wa matunda yenye maji ambayo ni bora zaidi.
3.    Kula mboga za majani hasa yale majani mapana. Mboga za majani ni dawa. Hii nitaeleza siku nyingine MUNGU akituweka hai, Lakini tia akilini tu haraka haraka leo kuwa hata wanyama mwituni huwa wanapata lishe na dawa pale wanapokula majani porini bila ya wao wenyewe kujua kinachoendelea. Majani mapana yana dawa inaitwa “Magnesium” nyingi sana ya kumwondolea mlaji hofu, wasiwasi, shaka, woga na vitu vinavyofanana na hayo.
4.    Usile sukari na wanga kwa wingi. Vyakula vyenye wanga kama ugali, wali, makande, Chipsi yai nk vikiliwa kwa wingi na mgonjwa wa kisukari vinaenda kuanzisha kiwanda cha kuzalisha sukari kwa wingi mwilini halafu ni mateso kwa mgonjwa na pengine kifo endapo hatajieleza kwa dakitari wake mapema. Hivyo mgonjwa wa kisukari anatakiwa awe Veggie’s – (Mla mboga na matunda sana)
5.    Usile vyakula vyenye mafuta mengi ni hatari kwa afya yako….Unaweza kufa!
6.    Kwa kuwa tafiti zimeonyesha kuwa maumivu ya njaa ni maumivu ya usafishaji taka-mwili kwa ujumla, basi maji yanarudiwa tena kuwa unywe mengi ili usikie njaa zaidi halafu ule zaidi kwa kuilinda afya yako.

Nitajitibuje?

Kama utafuatilia habari hii kwa ujumla wake utagundua kuwa sijaelekeza vizuri namna ya kufanya vipimo vya tiba nilizoorodhesha. Hii nimeiacha makusudi ili nionane kwanza na wagonjwa wa kisukari ili tukae na kupeana mkakati wa kupona kwa vile tiba za ugonjwa huu zinahitaji uangalifu mkubwa na nidhamu ya kutosha huku wagonjwa wa ugonjwa huu wakiwa wamekata tama kutokana na kuteseka kwa muda mrefu bila nafuu. Wengi wamedanganywa sana. Wengi wamepoteza pesa sana. Hivyo kuna hali ya kuchanganyikiwa na kutojiamini inajichora usoni mwa mgonjwa ukiongea naye, hivyo kama hutakuwa makini na kumwelewa utajikuta unamwacha bila kumsaidia ukiamini hahitaji msaada wa tiba yako.

Kama nilivyojieleza hapo awali kuwa mimi ni Dietist. Nazichambua dawa zilizopo katika bustani za maua na droo za jikoni tu kutoa tiba sahihi kabisa kwa familia nzima. Hivyo nikifika tu kwa mgonjwa nakagua bustani ya maua, nakagua jikoni, nakagua mlo wa mgonjwa, umri na afya ya mgonjwa, halafu napata jibu la dawa gani nimpe na kwa kiasi gani.
Pengine ilinibidi kuacha shughuli zangu zote na kumtengenezea diet mgonjwa halafu tukala naye kwa wiki sita! Ni kazi kubwa sana nadhani hii…

Lakini nawakaribisha wote wenye matatizo na naahidi kuwasaidia. Wanachotakiwa kufanya ni kujipatia NO SICK SCHEME card ambayo itawawezesha kupata huduma zangu bure mwaka mzima. Huduma zangu hazijumuishi gharama za dawa na tiba, ila ni ushauri na maelekezo ya kupata dawa ambazo hazipatikani kirahisi (hata kama dawa inapatikana nje ya nchi) pamoja na kufuatilia afya yako kwa ujumla kwa mwaka mzima bila kujali upo wapi ndani ya Tanzania.

NO SICK SCHEME inapatikana kwa kulipia shilingi mia tatu tu kwa siku. Malipo hayo yanafanywa kwa jumla ya mwaka mmoja (Tshs.109,500/=) na yanapitia NBC Industrial Branch – John Haule Acc. No. 033201074778
Mimi ni mtafiti wa kujitegemea. Sina chanzo chochote cha mapato ila toka kwa wanachama wa NO SICK SCHEME. Hivyo hiki ni kiwango cha chini cha ada ya uanachama kwa mwaka, ila unaweza pia kulipa zaidi na kuwa mwanahisa katika tafiti hizi.

Ukishalipa unanitumia risiti ya benki uliyolipia kwa kuituma kwa rotion@live.com au piga simu no 0768 215 956 na huduma zinaanza ikiwemo kukuchunguza afya na kukupa ushauri wa kitaalamu ili upone. Huu ni utaratibu wa kufanya kwa watu wanaoumwa maradhi ya aina zote na wanahitaji tiba sahihi toka kituo chetu.

Maradhi ninayotibu kirahisi ni:

1.    Kisukari – Diabetes
2.    Stroke & Paralysis – Kiharusi
3.    Wazee na Ajali – Bone&Joints pains
4.    Pumu – Asthma
5.    Vidonda tumbo – Intestinal Parasites
6.    Ukimwi – AIDS
7.    Cancer – Kansa
8.    Kidney Stones – Mawe ya Figo
9.    Fangasi – Fungus & Bacteria
10.    Meno – Rapid toothache relief

Na mengineyo mengi tu yanatibika kwa urahisi sana kitengo changu cha tafiti za kisayansi za tiba asilia (Kitchen&Garden Remedies)

Najua ungependa watu wengine wapone au wajue wakiumwa watapataje tiba sahihi. Hata sisi hapa tungependa kuona ubabaishaji katika sekta ya afya unaishia kabisa hivyo tunakuomba uitume hii article kwa watu wote katika contact list yako ili taarifa isambae haraka iwezekanavyo tujenge taifa tajiri lenye watu wenye afya njema daima.

Asante sana kwa kunisoma na karibu sana.

No comments: