Bwana Harusi Adam akimvisha pete ya ndoa mkewe Matilda kwa furaha kabisa,huku akitamka maneno mazuri ya kiapo,pia vigele gele vya hapa na pale vikisikika.
\Maharusi wakiwa katika nyuso za furaha kabisa wakiwasalimia wageni waalikwa mbalimbali
Wwooooowwww....! kwa raha zaoo maharusi wakilishana keki kwa staili ya kipekee kabisa. Blog ya JIACHIE inawatakia kila lakheri na fanaka tele katika maisha yenu mapya ya ndoa,Mungu akawabariki na kuwapa amani na upendo daima,bila kusahau uvumilivu kwa kila jambo na kumtanguliza Mungu siku zote za maisha yenu.
Maharusi wakiserubuka na wapambe wao pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya mnuso huo uliofanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Land Mark,Ubungo jijini Dar.
No comments:
Post a Comment