Tuesday, November 29, 2011

AKINA TWENTY PER WALIVYOZINGUA ARUSHA

 Msani wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Kinzasa ‘20%’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha hilo.

Waimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege na Christina Shusho wakitoa burudani jukwaani kwenye tamasha hilo.

vijana wa Dot Com Generation
Baadhi ya wasanii wa kundi la Glorious Singers wakitoa burudani  kwenye tamasha hilo.
 Sehemu ya umati uliohudhuria tamasha hilo.
Askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie (kushoto), mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa miongonbi mwa wageni waalikwa waliohudhuria tamsaha la Street University jijini Arusha. Kulia ni Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema. Chini ni msafara wa askof ukiingia uwanjani
Tamasha kubwa la ujasiriamali la Street University lililofanyika kwa kishindo ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Jumapili iliyopita, limeweka rekodi kwa kulifanya jiji hilo litingishike kwa burudani kabambe kutoka kwa wasanii kibao waliokamua jukwaani pamoja na mada motomoto za ujasiriamali zilizotolewa.

Mtandao huu ulikuwepo kwenye uwanja huo na kushuhudia jinsi umati uliofurika, wakiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema na askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie walivyoyafurahia mafunzo ya ujasiriamali na burudani ya kukata na shoka iliyoporomoshwa na wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo, Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa ‘20%’ , Glorious Singers, Dot Com Generation na Pastor Wambura.


“Tumepata mwitikio mkubwa kuliko hata tuliuvyotegemea. Tunawashukuru sana wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kwa kutuunga mkono na kujitokeza kwa wingi kusikiliza tulichowaandalia. Tunaamini maisha ya wengi yatabadilika kwani tumepandikiza mbegu za ushindi na mafanikio maishani.


“Tunawashukuru sana wadhamini waliowezesha kufanyika kwa tamasha letu, Kampuni ya Global Publishers Ltd, Airtel, Malta guiness, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA), Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha, Tripple A Radio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM), Sauti ya Injili Radio (92.2/96.2 FM)  na Radio 5 (105.7FM), zote za jijini Arusha,” alisema Mwang’amba ambaye ndiye aliyekuwa mratibu wa tamasha hilo.

No comments: