Mkali
wa muziki wa hip hop kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya hapa
nchini,Mflame wa Rhymes ,Simba Mzee,Afande Sele akiwarusha vilivyo
wakazi mbalimbali wa jiji la Mbeya,waliojitokeza kwa wingi kwenye
uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel,Airtel Money uliofanyika leo kwenye
uwanja wa mpira wa miguu wa Sokoine.
Wakazi
wa jiji la Mbeya kutoka vitongoji mbalimbali wakishangilia vilivyo
jioni ya leo kwenye tamasha hilo la Airtel Money,lililofanyika katika
uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Jaffarai akitumbuiza jukwaani jioni ya leo
kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya kutoka kampuni ya simu ya
Airtel,ijulikanayo kwa jina la Airtel Money.
Ilikuwa shangwe mwanzo mwisho,wakazi wa Mbeya wameipokea vyema huduma ya Airtel Money.
Palikuwa hapatoshi leo kwenye uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
Kundi
la muziki wa kizazi kipya kutoka Temeke,Wanaume Halisi likiongozwa na
kinara wao Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani
ya uwanja wa Sokoine,kwenye uzinduzi wa huduma mpya itolewayo na
kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel,ijulikanayo kwa jina la Airtel
Monye,ambapo wakazi wa jiji la Mbeya wameipokea kwa shangwe.
Jukwaani
ni wakali wa miondoko ya hip hop katika muziki wa kizazi kipya,kulia ni
Jaffarai pamoja na Jay Mo wakikamua vilivyo jukwaani kwenye tamasha la
Bongo 50,lililodhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,kupitia
huduma yao mpya ya Airtel Money.
No comments:
Post a Comment