*AZUNGUMZA NA MO BLOG
NA KUWEKA WAZI MIKAKATI YAKE IJAYO.
* ASHAURI ABIRIA
KUFAHAMISHWA MBINU ZA KUJIOKOA
MO BLOG: Nini
kitakuwa tofauti na vipindi vingine vya TV ambavyo umewahi kufanya.?
MUSSA HUSSEIN: Kitu
ambacho kitakuwa tofauti na show nyingine ambazo mimi nimewahi kufanya ni
kwamba hapa nitakupa stori za ajali za kuzama kwa meli sio ya Nungwi pekee bali
hata zilizopita nikikuonyesha matukio yenyewe yalivyokuwa tofauti na unaposoma
kwenye gazeti au kusikia redioni. Kwa mfano katika taarifa ya habari
utaonyeshwa kwa sekunde 30 tu mchezo umekwisha.
Hivyo huwezi kugundua haya matukio ni makubwa au ni madogo
kiasi gani.
MO BLOG: Nini
kimekufanya ufikie maamuzi ya kufanya kipindi cha namna hii kinachoonyesha
matukio halisi au huridhishwi na jinsi taarifa za majanga zinavyotolewa?
MUSSA HUSSEIN: Kwanza
watanzania hatuna utamaduni wa kusoma, ila ninachoshukuru Mungu kwa sasa hivi
kuna ongezeko kubwa la watanzania wanaotazama TV au mitandao hii mingine
iliyopo, kwa kutokea hapo nikaona kwa
sababu kila siku tunatoa lawama kwa serikali wakati mwingine tunalaumiana
wenyewe kwa wenyewe ipo haja ya kupeana elimu wenyewe kuhusiana na majanga
yanayotokea kila mara ikiwemo kwenye maji, barabarani au popote pale.
Kwa sababu kila siku anayeandika anasema Ajali za Barabarani
zitatumaliza, Ajali za angani zitatumaliza, Ajali za majini zitatumaliza kila
siku ni hivyo hivyo. Na ukiangalia hizi ajali za sijui meli, treni, mabasi
zinaua mamia ya watu.
No comments:
Post a Comment