Monday, December 5, 2011

Pima-Maji Ya Mjengwablog: Kipyeenga Pyeee- Kimeshapulizwa!


mjengwablog.com inaendelea na mchakato wa kumpata kiongozi bora kijana kwa mwaka 2011 kutoka kundi la wabunge. Kinachopimwa ni mchango wao katika jamii na uwezo wao wa kujenga hoja zenye kutetea maslahi ya taifa ndani na nje ya Bunge.

Ni wewe utakayeshiriki kuwapima na kuwachuja kwa kura yako. Lengo hasa ni kuhamasisha vijana kwenye ushiriki wa masuala ya uongozi. Kujenga Utaifa na Uzalendo na kujenga misingi ya demokrasia na utawala bora.


Washiriki watachujwa na kubaki sita watakaoungana na sita wengine kutoka kundi la wabunge vijana wanawake ambao tayari wameshapatikana kwa njia ya mchakato kama huu kwenye Mjengwablog.com.

Hatua hii ikikamilika tutaingia katika kile kitakachoitwa 'Mjengwablog Young Leadership Awards'. Hivyo basi, tutampata mbunge bora kijana wa mwaka 2011. Kigegezo cha kushiriki: Umri wa Mbunge usizidi miaka 40.

Hatua hii ya mchujo inawahusisha washiriki hawa;

1.January Makamba

2.David Kafulila

3. Zitto Kabwe

4. Felix Mkosamali

5. John Mnyika

6. Joseph Sugu Mbilinyi

7. Steven Masele

8. Mohammed Dewji

9. Moses Machali

10. Ezekiel Wenje

11. Hamis Kingwangwalah

12. Livingstone Lusinde
13. Godbless Lema
14. Highness Kiwia
15. David Silinde
16. Mwigulu Nchemba
17. Peter Serukamba
18. Vicent Nyerere
19. Deo Filikunjombe

Utaratibu wa kupiga kura:

Piga kura yako kwenye kisanduku hapo juu kulia. Kompyuta moja kura moja. Mpiga kura unaweza kubadilisha kura yako lakini huwezi kupiga kura mbili kwenye kompyuta moja. Matokeo unayona moja kwa moja. 100% hakuna Kuchakachua.



Matarajio ya baadae:
Mchakato huu ukikamilika , Mjengwablog.com itaratibu mchakato wa kumpata kiongozi kijana bora kwa mwaka 2011. Ni kutoka nje ya Bunge na anatotakana na kundi la viongozi vijana wanaokuja kwa kasi na michango yao kuonekana kwenye jamii. Ni vijana wenye kusimamia na kutetetea maslahi ya taifa.



Na mwisho itakuwa mchakato wa kumpata kiongozi bora kijana wa mwaka 2011 kwenye sekta ya uchumi na biashara. Mchakato utafanana na huu. Nao watatunukiwa tuzo kwenye ’ Mjengwablog Young Leadership Awards 2011’ ambayo itatolewa katika categories totauti kama inavyoonekana hapa. Na majina ya washiriki yatatokana na kupendekezwa na watembeleaji wa Mjengwablog na mitandao mingine kama huu wa JF. Tunakaribisha ushauri na mawazo hata yenye kushutumu.


Naam, ukisikia "Pyeeee! " - Kimeshapulizwa!- Nenda kapige kura yako!

Maggid Mjengwa,


Mratibu
.

Iringa.

http://mjengwa.blogspot.com

No comments: