
WAKURUGENZI WA SERENGETI FREIGHT WAKITOA MCHANGO WAO

WADAU KUTOKA PANDE ZOTE ZA LONDON WAKIWA KATIKA HARAMBEE

MR & MRS KAMWANO SABUNI WAKIKABDHI MCHANGO WAO

MDAU FREDDY MACHA ALKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUCHANGIA

MDAU ALI HAMISI NA RAFIKI YAKE WAKIKABIDHI MCHANGO WAO

MDAU ABUU FARAJI AKIPEWA MKONO WA ASANTE

LEMNA NA WATOTO WAKE WALIKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUCHANGIA
Salaams,
Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote waishio LONDON UK walioweza kufika jana jioni AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT kuchangia waathirika wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa mda wa masaa mawilitumeweza kukusanya Jumla ya pesa taslim Pounds £600, pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na vifaa vingine mbali mbali.
Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, NA Utawala wa AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT LONDON kwa kusaidia na kuwezesha kufanikiwa kwa zoezi la jana.
Mungu Ibariki AfriKa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni