Makamu Mwenyekiti Simba SC , Geofrey Nyange (Kaburu) akipeana mikono
na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga mara
baada ya makubaliano yao ya kufanya kazi pamoja mbele ya wanahabari
(hawapo pichani),yaliyofanyika leo kwenye hotel ya Belimonte jijini Dar.
Makamu Mwenyekiti Simba SC , Geofrey Nyange (Kaburu) wa tatu kulia akizungumza
mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na KLABU ya soka ya
Simba kuingia mkataba na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd
unaohusiana
na Promosheni na Masoko (Promotion and Marketing) kwa ajili ya mechi ya
Kombe
la Shirikisho (CAF) kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda. Kulia ni
Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions,Bw.Godfrey Mkama,Joseph
Kusaga na shoto ni Katibu Mkuu wa Simba Bw.Evodius Mtawali
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group/Prime Time Promotions Bw.Joseph Kusaga
akizungumza machache kuhusiana na mkataba huo kati ya Prime Time
Promotions Ltd na Klabu ya Simba SC,kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa
kampuni ya Prime Time Promotions, Bw.Godfrey Mkama na watatu kulia ni
Makamu Mwenyekiti Simba SC , Geofrey Nyange (Kaburu) pamoja na Katibu
Mkuu wa Simba SC,Bw.Evodius Mtawali.
====== = ==== ====== ====== ==========
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
KLABU ya soka ya Simba ina furaha kubwa kuutangazia umma wa
Watanzania kwamba imeingia mkataba na kampuni ya Prime Time Promotions/Clouds Media Group unaohusiana
na Promosheni na Masoko (Promotion and Marketing) kwa ajili ya mechi ya Kombe
la Shirikisho (CAF) kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda.
Ushirikiano huo wa namna ya kipekee una lengo la kuhakikisha
kuwa Watanzania wengi wanafahamu juu ya pambano hilo
na wanahudhuria pambano hilo
la kimataifa lakini pia kuweka mazingira ya kuvutia kwa makampuni na
wafanyabiashara ili wawekeze katika mchezo huu kipenzi cha Watanzania.
Ingawa mkataba huu wa sasa baina ya Simba na Clouds unahusu
mechi hii moja pekee, kuna kila dalili kuwa huu utakuwa mwanzo wa kampuni hizi
mbili kufanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu kwa lengo la kuhakikisha mchezo wa
soka unakua kwa faida ya taifa letu.
Kwa kuanzia tu, pamoja na mechi hii ya Kiyovu, Simba SC leo pia
inatangaza kuanzisha kwa luninga ya klabu, Simba TV, ambayo lengo lake kubwa
litakuwa ni kuonyesha shughuli za kila siku na matukio mbalimbali yanayohusiana
na klabu yetu.
Clouds Media Group kupitia Clouds TV ndiyo watakaokuwa
wakionyesha vipindi hivyo vya Simba mara moja kwa wiki mwanzoni lakini lengo ni
kuwa na televisheni ambayo itakuwa inaonyesha habari za Simba saa 24 kila siku.
Ndiyo maana basi, sisi katika Simba, tunaamini kuwa
ushirikiano huu baina ya Simba na Clouds unafungua njia ya maendeleo anuai
katika kila nyanja inayohusiana na mchezo wa soka hapa nchini.
Simba SC inapenda kutumia fursa hii kukaribisha
makampuni na wafanyabiashara kujitokeza kudhamini mchezo wa soka hapa nchini
kwa vile uzoefu unaonyesha kuwa kuwekeza katika soka kunalipa.
Wenu Katika Mapinduzi ya Soka Tanzania
Geofrey Nyange
Makamu Mwenyekiti
Simba SC
No comments:
Post a Comment