Wednesday, February 8, 2012

NENO LA SHUKRANI

Khadija Abdul  - 1972 – 2012

SHUKRANI
 Familia  ya Ndugu Abdallah Mrisho Salawi - Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, inachukua fursa  hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja au nyingine, katika mazishi na maziko ya mpendwa mkewe, Khadija Abdulhussien, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamis Feb 2, 2012, katika  hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam.

Shukrani za pekee ziwaendee wafanyakazi wote wa Global Publishers na hususani Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Eric Shigongo, ambaye alikuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo ya afya ya marehemu tangu mwanzo na kutoa ushauri kila mara, alijitolea kwa hali na mali ili kuokoa maisha ya mpendwa wetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.

Shukrani pia ziwaendee Dk. Wayi wa Kinondoni Hospital, Dk. Hirji wa Ebrahim Hajji Hospital na Dk. Nyawawa wa Aga Khan Hospital kwa jitihadi walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Khadija.

Familia inawashukuru pia majirani, jamaa na marafiki wote wa Mrisho waliyoko nchini na nje ya nchi  ambao wamekuwa wakimfariji kwa njia mbalimbali za mawasiliano na kumtia moyo katika kipindi hiki kigumu.

Familia haina  cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (khadija) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!

Mungu ampumzishe Khadija katika moja ya viwanja vya peponi – Amen!   

3 comments:

Unknown said...

Amen...Pole sana Abby.
Punzika kwa amani dada Khadija.

Anonymous said...

Ni kweli tunapaswa kumshukuruMungu kwa kila jambo na kumtanguliza katika kila tulifanyalo hakika amempumzisha kwa amani.

Tuzidi kuombeana kila iitwapo leo.

God be with u.

g.l.

Lubatiko Seme said...

Pole sana uncle cool and familia yako.. mimi binafsi nimesikitishwa sana na msiba wa mke wako mpenzi.. Mungu wa reheme na faraja aendelee kuwajibia kila swali mulilonalo katika kipindi hiki kigumu.. Mimi na familia yangu tunawaombea sana .. AMEN.