Khadija Abdul - 1972 – 2012
SHUKRANI
Familia ya Ndugu Abdallah Mrisho Salawi - Meneja Mkuu
wa Global Publishers Ltd, inachukua fursa
hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja
au nyingine, katika mazishi na maziko ya mpendwa mkewe, Khadija Abdulhussien,
aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamis Feb 2, 2012, katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam.
Shukrani
za pekee ziwaendee wafanyakazi wote wa Global Publishers na hususani Mkurugenzi
Mtendaji, Ndugu Eric Shigongo, ambaye alikuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo
ya afya ya marehemu tangu mwanzo na kutoa ushauri kila mara, alijitolea kwa
hali na mali ili kuokoa maisha ya mpendwa wetu bila kuchoka hadi dakika ya
mwisho neno la Mungu lilipotimia.
Shukrani
pia ziwaendee Dk. Wayi wa Kinondoni Hospital, Dk. Hirji wa Ebrahim Hajji
Hospital na Dk. Nyawawa wa Aga Khan Hospital kwa jitihadi walizozifanya za kujaribu
kuokoa maisha ya Khadija.
Familia
inawashukuru pia majirani, jamaa na marafiki wote wa Mrisho waliyoko nchini na
nje ya nchi ambao wamekuwa wakimfariji
kwa njia mbalimbali za mawasiliano na kumtia moyo katika kipindi hiki kigumu.
Familia
haina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea
kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea
thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi
kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (khadija) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!
Mungu
ampumzishe Khadija katika moja ya viwanja vya peponi – Amen!
3 comments:
Amen...Pole sana Abby.
Punzika kwa amani dada Khadija.
Ni kweli tunapaswa kumshukuruMungu kwa kila jambo na kumtanguliza katika kila tulifanyalo hakika amempumzisha kwa amani.
Tuzidi kuombeana kila iitwapo leo.
God be with u.
g.l.
Pole sana uncle cool and familia yako.. mimi binafsi nimesikitishwa sana na msiba wa mke wako mpenzi.. Mungu wa reheme na faraja aendelee kuwajibia kila swali mulilonalo katika kipindi hiki kigumu.. Mimi na familia yangu tunawaombea sana .. AMEN.
Post a Comment