*LEO KUIBUKA NA
KIPINDI KIPYA CHA TV CHA ‘ONGEA NA JANET’
*AITAKA JAMII KUACHA WOGA NA KUJITOKEZA KUONYESHA VIPAJI.
MO BLOG: Nini
Theme ya kipindi cha ‘ONGEA NA JANET’..?
JANET: Aah…!!
Theme ya “ONGEA NA JANET’ ni kipindi ambacho kinatoa fursa kwa mtu yeyote kuja
kuongea ili mradi awe na kitu ambacho kinaweza kuilemisha jamii. Kipindi hiki
kinazungumza na watu wa rika zote. Na katika kipindi hiki kwa kweli mimi
nazungumzia kila kitu sijajiwekea limitations. Lengo ili tufike mahali tuweze
kuzungumza hata yale mambo ambayo watu wanaogopa kuyazungumza hadharani.
Japo watu wengi wanapenda nizungumzie mambo ambayo yapo
current, lakini kwa mfano yakitokea mafuriko, ukifungua TV zote taarifa za
habari zinazungumzia mafuriko, radio zote ni mafuriko, ukisoma kila gazeti ni
mafuriko na hata misemo mitaani inakuwa kuhusu mafuriko. Sikuona tena umuhimu
wa kuongelea kitu ambacho kinaongelewa kila mahali, nataka kutoa nafasi ya
kuzungumzia mambo ambayo hatupati nafasi ya kuyazungumzia.
Kwa mfano huwezi kukuta, gazeti au TV ikizungumzia kuwa
wanawake walioko katika ndoa wanapata taabu kwa sababu ya nyumba ndogo, na hata
kama itaandikwa basi inapewa nafasi ndoogo.
Na sifikirii kipindi changu kiishe leo au kesho hiki kitaendelea siku zote.
MO BLOG:
Watazamaji watarajie nini kutoka kwako katika siku zijazo..?
JANET: Watarajie
mambo mengi mazuri na kuwa kila siku kipindi kitakuwa na kitu kipya. Nitakuwa
na season 4, hivyo kila season itakuwa tofauti na nyingine. Mfumo nitakaotumia
katika season 1 utakuwa tofauti na nitakaoutumia katika season 2 na kuendelea.
Halafu pia kitu kingine napenda watu wengi zaidi wajitokeze
kuingia katika gemu wasiogope waonyeshe talents zao ili kuwe na changamoto
zaidi. Kupata mahojiano haya kwa kina Bofya
hapa
No comments:
Post a Comment