Salam,
Raisi wa
Bendi FM Academy na mkali wa masauti Nyoshi amejiunga rasmi kwenye
Music Academy ili kutoa fursa ya kuwafundisha wanafunzi namna ya kuimba
vizuri vilevile kuwapatia uzoefu. Nyoshi ataungana na Mzee kalala pamoja
na Mandela kutoka Twanga katika mjumuisho wa pamoja wa kutoa mafunzo
halisi ya muziki ili kuwanoa ipasavyo wana academia na hatimaye kuweza
kufanikiwa kuibua vipaji vya muziki nchini Tanzania.
Music Academy imejikita zaidi katika kutoa mafunzo na pia kutafuta
vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga,
kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika
bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili
kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo
yataendela kufanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya
ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
Asanteni,
Imeandaliwa na ASET Pamoja na URBAN PULSE CREATIVE
No comments:
Post a Comment