Bi.
Harriet Macha kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
akifafanua lengo la ziara hiyo ambapo amesema ni muhimu kwa wanafunzi na
vizazi vijavyo kujua historia na madhara yaliyotokana biashara ya
utumwa. Katika kuadhimisha kumbukumbu ya biashara ya utumwa duniani
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kimegharamia ziara ya wanafunzi
kutoka shule tatu jijini Dar es Salaam kwenda kutembelea kituo cha
Kihistoria cha Kaole kilichopo Bagamoyo.
Mtaalamu wa Mambo ya Kale Bw. Jumanne Majige akitoa maelezo kwa wanafunzi.
Wanafunzi
wakishangaa kisima cha maajabu. Ksima hicho kiliaminika kuwa cha
maajabu baada Serikali kuwahi kuchota takribani Lita 10,000 za maji
lakini kiwango cha maji hayo hakikupungua.
Bw.
Jumanne Majige akitoa maelezo kwa wanafunzi kuhusu Kaburi la wapendanao
waliokufa siku moja kwenye bahari ya Hindi na kuzikwa pamoja lililopo
Kaole Bagamoyo.
Wanafunzi
wakinawa maji ya katika kisima cha maajbu kwa imani ya kuwa ni yenye
baraka. Kisima hichi hakikauki maji wala kuongezeka tangu enzi za
ukoloni na kinaaminika kuwa ni cha maajabu.
Mti wa Mbuyu unaosadikiwa kuwa na miaka 500.
Stella
Vuzo kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa akizungumza na
waanafunzi kutoka shule za Benjamini Mkapa, Kibasila, Lugalo na Mbezi .
Katika mazungumzo hayo akizungumzia lengo la Umoja wa Mataifa kuwa ni
pamoja na kuhakishasha biashara ya Utumwa inatokomezwa kabisa na kuwaasa
vijana wajijengee utamaduni wa kusoma vitabu na kuzijua haki zao za
msingi na kujitambua.
Bi.
Vuzo alitoa changamoto hizo katika ziara hiyo ambapo pia alitoa fursa
hiyo kuwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliutoa
katika maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya utumwa
duniani inayodhimishwa kila mwaka tarehe 25 mwezi Machi.
IMG_6622:
Kiongozi wa msafara
kutoka Kitengo cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo akibadilishana
mawazo na Mwanafunzi Nuru wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa. Kwa
picha zaidi Bofya hapa
No comments:
Post a Comment