Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Hassan Majaar Trust Bi. Zena Maajar Tenga akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Duka la Hisani la Taasisi hiyo litakalojulikana kama “Hassan Majaar Charity Shop” lililopo maeneo ya Mikocheni katika Jengo Arcade jijini Dar es Salaam. Bi. Tenga ametoa wito kwa Wadau nchini kote kupeleka vitu mbalimbali kuchangia chochote ikiwemo nguo hata zilizotumika, viatu, vitu ya watoto, vitabu, kama mchango kwa ajili ya kuuzwa katika duka hilo na fedha zitakazopatikana zitatumika kununua madawati kwa shule za umma za msingi na sekondari ili kuboresha elimu nchini.
Mjumbe wa Kamati ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zuhura Sinare Muro akifafanua Jambo na kuwataka Watanzania kuijenga nchi yetu kwa kufanikisha kampeni ya dawati kwa kila mwanafunzi.
Wageni waalikwa wakichagua viwalo katika duka la Hisani la Hassan Maajar Trust.
Mtoto Elias Lema wa shule ya DIS akitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakipata kifungua kinywa.
No comments:
Post a Comment