WABUNIFU wanne wa mavazi walioshiriki wiki ya mitindo Afrika Kusini wameeleza kufurahishwa kwao na ushiriki wao huo huku wakifafanua yale waliyojifunza wakiwa nchini humo.
Ziara hiyo iliyodhaminiwa na mwanamitindo mahiri Millen Magese inalenga kukuza na kutangaza tasnia ya ubunifu wa mavazi na uanamitindo wa Tanzania katika anga la kimataifa kupitia mradi wa Tanzania International Fashion Expose (TIFEX).
Wakizungumza katika nyakati tofauti wabunifu hao walifafanua kuwa onesho hilo limewafundisha mengi kwa kuwa wamekutana na wabunifu kutoka nchi mbalimbali za ndani na nje ya bara la Afrika.
Mbunifu Evelyn Rugemalira alisema kuwa ameweza kujifunza namna ambavyo wabunifu wa nje wanavyojitangaza na kutafuta soko.
Naye mbunifu Doreen Noni kupitia lebo yake ya Eskado Bird alisema kuwa mara nyingi amekuwa akishiriki katika maonesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, mwaka huu ametengeneza nguo za kuvutia zaidi.
Alisema kuwa kupitia onesho la wiki ya mitindo hapa Afrika Kusini ameshajipatia soko la kimataifa kwa kuwa onesho hilo limemtangaza zaidi.
Naye Jamira Vera Swai akishirikiana na Julie Lawrence alisema kuwa kupitia tamasha hili nguo zake zitatambulika kimataifa zaidi na kuweza kumweka katika ramani ya Afrika. Julie kupitia mradi wake wa fahari uliopo kisiwani Zanzibar aliwavalisha vidani na mikoba wanamitindo waliovaa nguo za Jamila.
Naye mratibu wa ziara hiyo Millen Magese alisema kuwa “Nimefurahi sana kufanikisha ziara hii kwani mwanzo wa kutangaza kazi zetu kimataifa umeanza vizuri kupitia fani hii ya wabunifu wa mavazi na wanamitindo, nawaamini watanzania na vipaji vyao na ninatumaini ya kuwa watatambua mradi huu ni kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment