Tuesday, April 17, 2012

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU DAR WAPEWA SOMO KUHUSU MADHARA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA

 Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akisoma hotuba kwa niaba ya Mshauri Mwandamizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya KImbari nchini Rwanda, ambapo amehimiza nchi washiriki kuwa na imani na mahakama ya ICTR.

 
 Wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakisikiliza
 Balozi Mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Sano Lambert akitoa neno la shukrani na pia kuasa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutetea amani na maendeleo kwa faida ya vizazi vijavyo na maendeleo ya ukanda wa Maziwa makuu kwa ujumla.

 Profesa Chris Peter Maina wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akielezea na kufafanua umuhimu wa Mahakama, akitolea mfano ya ICTR kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kijamii katika kuhakikisha haki inatendeka, haswa katika matukio kama ya uhalifu wa kivita.

 Na Mwandishi wetu.
Wananchi wa Rwanda na Afrika Mashariki kwa Ujumla wametakiwa kulinda na kudumisha amani katika eneo la maziwa makuu kwa kuwa hiyo ndio misingi ya umoja na maendeleo.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Msemaji na Mshauri Mwandamizi wa Kisheria wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda Bw. Roland Amoussouga, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vizo, amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda inasikitika na inatoa pole kwa wale walioathiririwa na vita vilivyotokea mwaka 1994na kuwa iko pamoja nao.

Aidha amesema tunapaswa kuweka kumbukumbu ya waliopoteza maisha na walionusurika , ambao kwa sasa wameathirika kimwili na kiakili.

Katika kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania.

No comments: