Monday, May 21, 2012

MWANAMITINDO FLAVIANA MATATA AKABIDHI MSAADA WA MABOYA 500 JIJINI MWANZA LEO

Mwanamitindo Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la Usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service, Kapten Obadia Nkongoki, Igoma jijini Mwanza leo.

Flaviana akionesha moja ya maboya yenye nembo ya foundation yake aliyokabidhi katika kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya MV Bukoba ikiwa ni kampeni yake ya kupunguza ajali za majini hapa nchini.
Flaviana Matata akishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo yaliyopi Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza pia mama yake mzazi.

Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo.

Flaviana na wageni wakiweka  mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo leo Igoma jijini Mwanza.

No comments: