Monday, May 21, 2012

BARCODES KUWAKOMBOA WASANII DHIDI YA WIZI WA MALI SANAA ZAO

 
Mkurugenzi wa GS1, Fatuma Makange akitoa ufafanuzi wa namna Barcodes inavyodhibiti uhalali wa kazi za
wasanii.
 
Wadau mbalimbali wa sanaa wakifuatilia mkutano huo.
 
Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego (kushoto) akizungumzia  hoja kutoka kwa wadau wa sanaa (hawapo pichani).   Kulia ni Fatuma Makange.
 
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) mwenye shati jeupe) akifuatilia mkutano na wadau mbalimbali.
Kampuni ya GS1 leo ametambulisha mfumo maalum wa teknolojia ya kompyuta wa kusaidia kuZitambua haki miliki Za kazi za wasanii unaofahamika kama Barcodes.  Utambulisho huo umefanywa na Jukwaa la Sanaa  kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) Ilala jijini, Dar.

Kama mfumo huu utafanikiwa kwa asilimia mia moja, utasaidia kupunguza wizi wa kazi za wasanii kwani kila kazi ya msanii itatakiwa kuwa na Barcode yake itakayotambulika kimataifa na kazi yake itauzwa kwa mfumo wa ‘scanner’ hivyo si rahisi kufanya udanganyifu wowote na Watanzania watatakiwa kununua kazi hizo katika maduka maalum yenye ‘scanner’ hizo maalum.

                                     PICHA ZOTE NA ERICK EVARIST/GPL

No comments: