Msimamizi
wa vipindi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mwanga Kirahi
akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada iliyohusu Teknolojia ya kisasa (Digital)
Katika Utengenezaji Filamu kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA wiki hii.Kulia
kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matukio BASATA, Malimi Mashili.
Mkongwe
wa Muziki wa dansi Mzee Kassim Mapili akionesha manjonjo yake baada ya
kufurahishwa na mada kuhusu Mfumo Digital iliyowasilishwa kwenye Jukwaa la
Sanaa wiki hii.
Mkuu
wa Taasisi ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma Ngalimecha Ngahyoma akichangia
mada hiyo kwenye Jukwaa la Sanaa. Alishauri Wasanii kujipanga katika
kuukabili mfumo wa Digital.
Sehemu
ya Wadau wa Jukwaa la Sanaa waliohudhuria mjadala huo wakifuatilia kwa
makini.
Wasanii nchini wameshauriwa
kujipanga katika kutumia fursa na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati
Ulimwengu ukijiandaa kuingia kwenye mfumo wa digital kutoka ule wa nalogia ifikapo mwaka 2014.
Ushauri huo umetolewa wiki
hii na Msimazi wa Vipindi vya televisheni wa Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC) Mwanga Kirahi wakati akiwasilisha mada iliyohusu Teknolojia ya kisasa
Katika Utengenezaji Filamu kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao
makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.
Alisema kuwa kuhama kutoka
mfumo wa analogia kwenda digitali kutazalisha fursa mbalimbali za kuendeleza
Sanaa nchini lakini pia ni mwanzo wa kuibuka kwa changamto nyingi ambazo kama
wasanii hawatakuwa makini basi wanaweza kupotea na kushindwa kushindana
ipasavyo.
“Mfumo wa digitali utaleta
ushindani katika kuandaa programu za televisheni, utazalisha fursa kwa kazi za
wasaniii wetu kuonekana ulimwengu mzima lakini unaweza kuwa mwanzo wa kufa kwa
ubunifu kama wasanii watategemea vifaa vya kisasa tu pasipo kuingiza ubunifu
binafsi” alisisitiza.
Katika hili aliwashauri
wasanii kutengeneza kazi zenye ubora na zisizo za kunakiri kutoka kwa wengine lakini
pia zenye ubunifu binafsi pasipo kutegemea vifaa hivi vya kisasa pekee kwani
kinyume chake ni kukataliwa kwa kazi zao na hatimaye kupwaya.
“Digital maana yake ni kazi
za Wasanii wetu kuonekana Ulimwengu mzima, sasa kama zitakuwa za kunakiri
kutoka kwa wengine na kutegemea vifaa hivi vya kisasa tu pasipo ubunifu binafsi
hatutafanikiwa. Haya pekee yanazifanya kazi zetu zisivume muda mrefu kwani
zinakuwa si original (halisi)i” alizidi kusisitiza.
Aliongeza
kuwa, wasanii
hawana budi kubadilika sasa na kuacha tabia ya wao kufanya kila kitu
kikuanzia umeneja, utunzi, uongozaji (directing), uzalishaji (producing)
na
kadhalika kwani kwa kufanya hivyo kunazifanya kazi zao kuwa na radha
moja pekee
ambayo haiwezi kudumu muda mrefu.
Wadau wengi waliofika
kupata elimu hiyo kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa waliiomba Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA) kupanga kukutana na wasanii ili kuwapa elimu juu ya
mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.
1 comment:
Kweli kabisa, maana hilo teke jipya, usipoliangalia unaweza ukang'olewa meno,tujipange na tuwe pamoja na syanasi na teke linalokujia, au sio
Post a Comment