Omotola Jalade,
Nyota
wa Filamu wa Nigeria, Omotola Jalade, anatarajiwa kutua nchini leo
akitokea Nigeria ambapo usiku pia atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya
uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu iitwayo Super Star.
Omotola
ambaye ataambatana na Meneja na mpiga picha wake maalum anatarajia
kutua nchini leo kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia. Omotola
ambaye pia ni mwanamuziki, ni mmoja kati ya wasanii wanaolipwa kiasi
kikubwa cha fedha katika soko la filamu nchini Nigeria. Kwenye orodha
hiyo wapo poa Genevive Nnanji, Inni Edo na Ritha Dominick
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, mwenyeji wa msanii huyo, Wema Sepetu alisema kuja
kwa Omotola ni kufungua njia kwake katika soko la kimataifa la medani
ya sanaa kwani lengo lake kubwa sasa ni kusonga mbele.
“Mikakati
yangu ni kuingia soko la kimataifa nah ii ni njia ya kwanza ya kufanya
hivyo, yapo mambo ambayo tutazungumza na kuangalia jinsi ya kufanya,
suala si kuzindua SuperStar tu lakini pia kuona kiwango chetu,” alisema.
Katika
onyesho la Giraffe, kiingilio kitakuwa sh 30000 kwa watu wazima ambapo
watoto watalipiwa sh 5000 huku wakishuhudia filamu hiyo ya superstar,
muziki utakaoporomoshwa na THT BAND, Onyesho la mavazi pamoja na nafasi
kupiga picha na nyota huyo wa Nigeria.
Omotola
ni mama wa watoto wanne ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16. Mumewe ni
rubani na ndoa yao ilifungwa kwenye ndege ikiwa angani. Omotola alikuwa
nchini Uingereza wiki iliyopita kwenye ziara za kikazi ambapo anakuja
kwa uzinduzi wa SuperStar na kuelekea Marekani ambako kuna filamu
anaenda kutengeneza.
Taasisi
yake imeingizwa kwenye kinyang’anyiro cha kushindania tuzo bora ya
kusaidia jamii. Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52,
zikiwemo, Ties That Bind (2011), A Private Storm Ije (2010), My Last
Ambition (2009), Beyonce & Rihanna (2008), Temple of Justice (2008),
Tomorrow Must Wait (2008) na nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment