Sunday, June 16, 2013

Leo Tunapigania Safari Mbili; Ya Brazil Na Morocco!

Ndugu zangu,
Leo Taifa Stars yetu inashuka tena uwanjani kwenye moja ya mechi muhimu sana kuwahi kuchezwa. Kimsingi, leo tunapigania safari mbili; ya Brazil na Morroco kwenye Afcon. Ni kwa vile Morocco inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mnichuano hiyo 2015.
Mshindi wa pili kwenye safari ya kwenda Brazil anaingia moja kwa moja kwenye michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika. Mara ya mwisho Tanzania kushiriki fainali hizo ilikuwa mwaka 1980.
Tafsiri yake?
Leo tunalazimika kushinda ili tuwe na matumaini ya  kwenda Brazil na hata kushika nafasi ya pili na kwenda AFCON. Tukifungwa leo ina maana ya hata safari yetu ya AFCON 2015 kuwa ngumu pia.
Kama ninavyosema mara nyingi, kuwa kandanda ina miujiza yake na imetokea zaidi ya mara elfu moja.  Leo tikiwafunga  Ivory Coast . Kisha Ivory Ciast wakafungwa na Morocco, na sisi tukawafunga Gambia kwao,  basi, ina maana tunakwenda Brazil.
Cha kujiadhari?
Tuukubali ukweli, kuwa Ivory Coast ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa na wenye uzoefu. Kimsingi ina wachezaji ambao, wanaweza kufanya lolote lile na wakati wowote ule wakiwa uwanjani. Hivyo, ni timu ya kuiheshimu lakini si kuigopa. Ivory Coast wanafungika, lakini lazima wachezaji wetu wajitume kwa dakika zote za mchezo.
Kila la Heri Taifa Stars Yetu!
Maggid,
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com

No comments: