Wednesday, October 9, 2013

MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VILIVYOPIGANIA UHURU BARANI AFRIKA WATEMBELEA KAMBI YA IHEMI-IRINGA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiowaonyesha Makatibu Wakuu wa Vyama vilivyopigania uhuru wa nchi zao barani Afrika na ujumbe wa chama cha Kikomunisti cha China CPC eneo ambalo litajengwa Chua cha Vijana wa nchi zilizopigania uhuru na kukomboa nchi zao katika eneo la Ihemi Mkoani Iringa leo ambapo viongozi hao wametembelea na kukagua eneo hilo lenye zaidi ya hekta 1800., Katika Picha wa pili kulia ni Filipe Paunde Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO cha Mozambique na kulia ni mkalimani wake, Viongozi hao kesho watakuwa na mkutano mkubwa utakaofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea kambi hiyo leo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE IHEMI-IRINGA
1a 
Baadhi ya majengo mabweni madogomadogo yanavyoonekana kwa juu eneo lenyewe linavyoonekana 6 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribisha wageni wake mara baada ya kufika katika kambi ya Ihemi mkoani Iringa leo kutoka kulia ni Obed Papela kutoka ANC na Naibu Waziri ,Didymas Mutasa Katibu MKuu wa chama cha ZANU- PF cha Zimbabwe, kutoka kushoto ni Dino Matrose Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola na mwenye shati jeupe ni Filipe Paunde Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO cha Mozambique na mkalimani wake. 8 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimuonyesha eneo hilo Ai Ping aliyevaa kofia Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa China kutoka chama cha Kikomunisti cha China CPC ukubwa wa eneo hilo. 11 
Viongozi hao wakilitazama eneo hilo kwa upande wa pili wa barabara kuu ya Iringa- Mbeya- Tunduma. 14 
Kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Asha Rose Migiro na Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Chrstine Ishengoma pamoja na wageni wengine wakiwa katika ukumbi wa mkutano Kambi ya Ihemi. 15 
Wakiendelea kutathmaini eneo hilo. 18 
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa vijana wa mkoa wa Iringa Ahmed Asas.

No comments: