Monday, July 14, 2014

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MKOANI MWANZA

Meneja  Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na  Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  kwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani..
Upakuaji ukiendelea.
Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu (kushoto) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael wakisaidizana kufanikisha shughuli hiyo ya makabidhiano. 
Mafuta kwa  Kituo.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na wadau wa Airtel. 
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda" Kauli ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema.
Twaha bin Bakari Utari ambaye ni Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  ambao ni wamiliki na kituo  ameshukuru kwa msaada huo toka Aitel huku akihamasisha wadau wengine kuiga mfano huo kwa ustawi wa jamii ya Watanzania. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

Sambamba na kuzibainisha changamoto wanazokabiliana nazo kama vitabu, madaftari,magodoro na sehemu za kulala,  msimamizi wa kituo Al-Hajji Hussein pia naye alikuwa na yake ya kusema. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Ahmad Mustapha ni mmoja kati ya vijana wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Shumbana Hassan ni mmoja kati ya watoto wa kike wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Licha ya kuushukuru uongozi wa kituo kwa makaribisho mazuri Meneja  Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi amesema kuwa msaada huo ni utaratibu wa Kampuni ya Airtel kurejesha kwa jamii yake. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza, kilianzishwa mnamo tarehe 3/07/ 2012 kina jumla ya watoto 50 kinachowalea, wa kike wakiwa 14 na wakiume 36.

Watoto wa kiume wanaishi katika nyumba maalum msikitini hapo, nao mabinti wakiishi kwenye hisani ya nyumba za majirani waliojitolea.
Shukuran...Aksante!!

No comments: