Saturday, August 9, 2014

MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL NDANI YA TAMASHA LA MATUMAINI

Mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal akitoa hotuba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Eric Shigongo naye akitoa neno la matumaini kwa maelfu ya Watanzania waliofurika Uwanja wa Taifa, Dar.
Mgeni rasmi Dk. Ghalib Bilal akikakua timu ya wabunge wa Simba.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wabunge wa Yanga.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo na refa wa mchezo wa mechi ya wabunge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global, Eric Shigongo.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mohamed Ghalib Bilal amelipongeza wazo la Tamasha la Usiku wa Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, jana kuwa ni zuri.
Alimpongeza Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwa kuandaa tamasha hilo kwani linaunganisha Watanzania wote.

No comments: