Sunday, December 7, 2014

BELLA AITIKISA DAR LIVE USIKU WA NANI KAMA MAMA

Mfalme wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ akifanya yake usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Nyomi ya mashabiki walijitokeza katika uzinduzi wa albamu yake mpya ya Nani Kama Mama ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Madansa wa Malaika Music bendi wakifanya yao.
Mashabiki wakicheza na Christian Bella ‘Obama’.
Mashabiki wakiwa wamepagawa na shoo ya mfalme wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ (hayupo pichani).
Christian Bella ‘Obama’ akizidi kuwapagawaisha mashabiki wake.
Madansa wa  Christian Bella wakifanya yao.
Mashabiki wakicheza na kuimba wimbo wa Nakuhitaji wa Bella.
Bella na wacheza shoo wake wakifanya yao.
Christian Bella akiimba wimbo wa Nani Kama Mama akiwa na shabiki wake.
BENDI ya muziki wa Dansi ya Malaika chini ya Christian Bella ‘Obama’ usiku wa kuamkia leo iliutikisa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar baada ya kuwapagawisha mashabiki kwa shoo ya nguvu.
Onyesho hilo lililoanza saa tatu usiku ambapo Malaika bendi walikuwa wakiwapa ladha mashabiki kwa kupiga kopi mbalimbali ya nyimbo za Kikongo zinazobamba.
Ilipofika saa nne na nusu ukumbi ulilipuka kwa shangwe baada ya kiongozi wa bendi hiyo Christian Bella kupanda jukwaani kwa wimbo wake wa Yako Wapi Mapenzi ambao ulisababisha mashabiki kuinuka katika viti vyao na wale ambao walikuwa wakinyemelewa na usingizi kuamka.
Bella alizidi kuwapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo kali mfululizo ambazo zinatamba katika redio na vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo Nani Kama Mama, Yako wapi Mapenzi, Msaliti, Usilie na nyingine kibao.
(PICHA/HABARI: ISSA MNALLY/ GPL)

No comments: